Baada ya Mahakama kusema Polisi hawajawashikilia akina Soka Malisa aandika haya

Hapa sasa tunaanza kujadili matamanio
Sio hvyo una logic za kitoto ulitaka nije na picha ya watu wamevunjika miguu ndio uamini, nimekupa linnk usome hutaki. Nifanyaje sasa ? Wewe unataka proof ipi ? Ulitaka hii ishue ni ipresent vipi mkuu ?
 
Nimesoma yote hiyo link wapi wamesema wamevunjwa miguu kwa risasi?
 
kufa kwa serikali nyingi zilianza hivi.sui uwa watanzania wanasoma vitabu au wachambuzi
Vikundi vya watekaji raia “”visivyojulikana” vinapozuka katika nchi maana yake nchi hiyo haina utawala wa sheria! Na nchi kama hakuna kuheshimu sheria maana yake ni fujo na vurugu katika jamii! Kwa mtindo huo nchi haiwezi kuwa stable.
 
Nachomkubali tajiri Rostam. Kuna wakati anasemaga ukweli
 
Matamko ya upinzani hayana impact yoyotee,tujifunze kudai haki kwa nguvu badala ya kutoa matamko yasiyo na tija kila siku.. Tujifunze hata kwa wamasai wa ngorongoro.
 
Vijana wa daslamu munajikuta wajanja kuwadhulumu watu hya sasa onjeni malipo yenu
 
Jana Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema kwamba Polisi haijawashikilia Deus Soka na wenzie wawili (Frank Mbise na Jacob Mlay) wanaodaiwa kutekwa maeneo ya Yombo Buza, na watu wenye silaha kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Wilson Dyansobera ambaye alisema Mahakama imejiridhisha kuwa vijana hao watatu hawapo Polisi na hivyo kutaka Polisi iwatafute.

Hukumu hii imeleta simanzi kubwa kwa ndugu wa vijana hawa, na wapenda haki wote nchini. Lakini pia imeset "precedence" kwa matukio ya utekwaji na watu kupotea;

1. Hukumu hii inamaanisha ukifuatwa mtaani na watu wasio na sare za Polisi, vitambulisho na arrest warranty usikubali kwenda. Pambania uhai wako, bora wakuulie hapo ulipo kuliko wakupeleke huko wanakotaka. Kwa lugha rahisi bora ufie nyumbani ndugu zako watakuzika, kuliko ukafie pasipojulikana na ndugu zako wasione hata maiti yako.

2. Hukumu hii inamaanisha baadhi ya Polisi wenye "nia ovu" wanaweza kukukamata na baadae wakakanusha sio wao na usiwe na la kufanya. Na mahakama itakosa ushahidi wa kuwatia hatiani.

3. Hukumu hii inamaanisha kwamba Tanzania kuna genge la kuteka watu ambalo sio sehemu ya jeshi la Polisi. Kama Mahakama inakubali kuwa akina Soka "walitekwa" lakini sio na polisi, it means mahakama inakubali genge la utekaji lipo. Je genge hilo limeundwa na nani? Linamtumikia nani? Kwa maslai gani?

4. Hukumu hii inamaanisha kuwa vyombo rasmi vya ulinzi vipo dhaifu kiasi kwamba raia wanaweza kutekwa kwenye nchi yao na "genge la watu wasiojulikana" na Polisi wasiweze kuzuia.

5. Hukumu hii inamaanisha usalama wa wakosoaji wa serikali upo mashakani. Hivyo basi usitembee peke yako. Kama wewe ni mkosoaji wa serikali hakikisha hukai kifala.

NB: Ni bahati mbaya haya yote yanafanyika katika nchi inayojinasibu kuheshimu uhuru wa maoni na utawala wa sheria. Ni bahati mbaya zaidi kuwa Waziri wa mambo ya ndani anajisifia kuwa nchi ipo salama wakati kuna watu wanadaiwa kutekwa na kupotezwa na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivi.!
hiyo ndiyo bongo
Na bado wasiaminike hata wakionesha vitambulisho.Wanaweza kughushi tu na kufanyia uhalifu wao.Trust nobody!
Sahihi mkuu ,,mana Tanzania kwa kughushi tupo juu
 
Wanahubiri Amani, huku wameficha mapanga. Kama polisi haihusiki, serikali haihusiki na watu kutekwa. Je ni nani anayeteka watu ndani ya nchi, yenye vyombo lukuki vya usalama?

Tuseme kuna kikundi cha watu, je si kazi ya Serikali na vyombo vyake vya usalama kulinda kila raia? Mpaka hapa imeshindwa jukumu lake.

Nilisema mwanzoni, tupazeni sauti, leo unaona ni wao. Itakuja atekwe mtu wako wa karibu, ndiyo mtaanza piga kelele. Yametokea vilevile nilivyosema.

Kwakuwa si vyombo vya Usalama vinavyoteka. Na haipewi uzito, ni jukumu la kila mtu kujilinda na kumlinda mwenzake. Huna mguu wa kuku, kuwa na kakisu ka kukunja, unatekwa ondoka na koromeo la mmoja, utaenda kufa ila unaenda na mwenzao.
 
Jana Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema kwamba Polisi haijawashikilia Deus Soka na wenzie wawili (Frank Mbise na Jacob Mlay) wanaodaiwa kutekwa maeneo ya Yombo Buza, na watu wenye silaha kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Wilson Dyansobera ambaye alisema Mahakama imejiridhisha kuwa vijana hao watatu hawapo Polisi na hivyo kutaka Polisi iwatafute.

Hukumu hii imeleta simanzi kubwa kwa ndugu wa vijana hawa, na wapenda haki wote nchini. Lakini pia imeset "precedence" kwa matukio ya utekwaji na watu kupotea;

1. Hukumu hii inamaanisha ukifuatwa mtaani na watu wasio na sare za Polisi, vitambulisho na arrest warranty usikubali kwenda. Pambania uhai wako, bora wakuulie hapo ulipo kuliko wakupeleke huko wanakotaka. Kwa lugha rahisi bora ufie nyumbani ndugu zako watakuzika, kuliko ukafie pasipojulikana na ndugu zako wasione hata maiti yako.

2. Hukumu hii inamaanisha baadhi ya Polisi wenye "nia ovu" wanaweza kukukamata na baadae wakakanusha sio wao na usiwe na la kufanya. Na mahakama itakosa ushahidi wa kuwatia hatiani.

Pia soma: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea

3. Hukumu hii inamaanisha kwamba Tanzania kuna genge la kuteka watu ambalo sio sehemu ya jeshi la Polisi. Kama Mahakama inakubali kuwa akina Soka "walitekwa" lakini sio na polisi, it means mahakama inakubali genge la utekaji lipo. Je genge hilo limeundwa na nani? Linamtumikia nani? Kwa maslai gani?

4. Hukumu hii inamaanisha kuwa vyombo rasmi vya ulinzi vipo dhaifu kiasi kwamba raia wanaweza kutekwa kwenye nchi yao na "genge la watu wasiojulikana" na Polisi wasiweze kuzuia.

5. Hukumu hii inamaanisha usalama wa wakosoaji wa serikali upo mashakani. Hivyo basi usitembee peke yako. Kama wewe ni mkosoaji wa serikali hakikisha hukai kifala.

NB: Ni bahati mbaya haya yote yanafanyika katika nchi inayojinasibu kuheshimu uhuru wa maoni na utawala wa sheria. Ni bahati mbaya zaidi kuwa Waziri wa mambo ya ndani anajisifia kuwa nchi ipo salama wakati kuna watu wanadaiwa kutekwa na kupotezwa na hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivi!
Cha kuongezea wewe kama mkosoaji wa serikali hakikisha unamiliki silaha yaani wakija bora muuane kuliko kukubali kuchukuliwa. Ila inasikitisha sana. Unajua tuendako unaweza kukuta majaji na mahakimu wataanza kutekwa na wao.
 
Back
Top Bottom