Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Itakumbukwa kuwa IGP Simon Siro alisema polisi wameshindwa kuendelea na uchunguzi wa kisa cha Tundu Lissu kupigwa risasi kwa sababu hakuwepo Tanzania. Lakini hata baada ya Lissu kurejea nchini bado polisi walisema hawawezi kuendelea na uchunguzi hadi dereva wake naye arejee kwa sababu ndiye aliyeshuhudia risasi zikipigwa. Lakini pia hadi leo polisi hawajafungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo la kijinai na kigaidi.
Katika mahojiano hayo Lissu amesema anaishtaki kampuni ya Tigo kwa kuhusika kwake kutoa taarifa zilizofanikisha Makonda na genge lake kumpiga risasi.
Kwa sasa Tundu Lissu amekamilisha maadalizi ya kufungua kesi hiyo na miongoni mwa watu watakaoitwa kutoa ushahidi ni polisi, Makonda na dereva. Kwa sababu hiyo ni wazi dereva ni mtu muhimu sana katika kesi hiyo na kuja kwake nchini kunaweza kusababisha ushahidi wake kupotea au kupotezwa. Nadhani imeeleweka " kupotea au kupotezwa"!