Baada ya mahojiano ya Chief Odemba na Tundu Lissu leo nimeelewa kwa nini dereva yuko Ubeligiji

Baada ya mahojiano ya Chief Odemba na Tundu Lissu leo nimeelewa kwa nini dereva yuko Ubeligiji

Sio kweli . Lisu kafungua hiyo kesi baada ya kesi ya mtumishi wa Tigo kuisha hivi majuzi tu.

Hivyo kujificha kwa dereva Ubelgiji hakuhusiani kwa namna yeyote na hii kesi.
 
Itakumbukwa kuwa IGP Simon Siro alisema polisi wameshindwa kuendelea na uchunguzi wa kisa cha Tundu Lissu kupigwa risasi kwa sababu hakuwepo Tanzania. Lakini hata baada ya Lissu kurejea nchini bado polisi walisema hawawezi kuendelea na uchunguzi hadi dereva wake naye arejee kwa sababu ndiye aliyeshuhudia risasi zikipigwa. Lakini pia hadi leo polisi hawajafungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo la kijinai na kigaidi.

Katika mahojiano hayo Lissu amesema anaishtaki kampuni ya Tigo kwa kuhusika kwake kutoa taarifa zilizofanikisha Makonda na genge lake kumpiga risasi.

Kwa sasa Tundu Lissu amekamilisha maadalizi ya kufungua kesi hiyo na miongoni mwa watu watakaoitwa kutoa ushahidi ni polisi, Makonda na dereva. Kwa sababu hiyo ni wazi dereva ni mtu muhimu sana katika kesi hiyo na kuja kwake nchini kunaweza kusababisha ushahidi wake kupotea au kupotezwa. Nadhani imeeleweka " kupotea au kupotezwa"!
Makonda ninamuonea huruma.
 
Dereva naye ni muhanga wa tukio hili, lakini kwa nini hakuguswa na risasi walau moja, pia dereva atakuwa na lipi la ajabu kwa sababu yeye atasema," alishtukia risasi zikipigwa kutokea upande wa kushoto, na watu ambao kwa vyovyote hawezi kuwatambua, nasema hivi hivi dereva naye alikuwa ni muhanga.
Ni kweli lakini katika uchunguzi kuna zaidi ya hayo yatahitajika kwa maana kabla ya tukio na baada ya tukio.
 
Hawajashindwa chochote na hawatokuja kushindwa na vikitu kama chadema, wao wametulia tu wanawachora wawaone mnapoishia. Hawakushindwa kuzuia maandamano watashindwa kumuhoji mbowe kweli???
Kwa hiyo wanahusika na kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu! Mbele ya mahakama ya kimataifa wataumbuka kuwa ndiyo watu wasiojulikana!
 
Ni kweli lakini katika uchunguzi kuna zaidi ya hayo yatahitajika kwa maana kabla ya tukio na baada ya tukio.
Upo sahihi, kwa kuwa dereva ni muhanga, kwanini anafichwa kwa nguvu kubwa, aje, hapa, kuna jambo nyuma ya pazia trust me!
Lissu ni muhanga
Dereva ni muhanga
Wanahaki ya kudai kutaka kuuwawa, lkn ajabu muhanga mmoja anamdhibiti muhanga mwingine, hivi hatujiulizi hili?
 
Waliomkosakosa nao wajinga sana

Over!
Waliomkosakosa? Risasi 16 zilipenya mwilini. Tosha kumuangusha hata tembo! Hakuna cha ujinga labda upumbavu kwa waliopanga tukio.

Anyway, Lissu leo hii ni jinamizi linalosotesha watawala. Hata JPM hakuwa na ujasiri wa kukutana na Lissu mpya face to face au kupeana mikono. Hata kutaja jina lake tu.
 
"Injustice somewhere is the threat to justice everywhere."

Reverend Dr. Martin Luther King Jr.


Je, wewe binafsi ungejisikiaje endapo kama zile risasi za moto alizopigwa Tundu Lissu kule Dodoma angepigwa nazo mama yako mzazi?? Je, ungefurahi au ungehuzunika kutokana na tukio hilo???
kwani tundu lisu ni baba yako?
 
Upo sahihi, kwa kuwa dereva ni muhanga, kwanini anafichwa kwa nguvu kubwa, aje, hapa, kuna jambo nyuma ya pazia trust me!
Lissu ni muhanga
Dereva ni muhanga
Wanahaki ya kudai kutaka kuuwawa, lkn ajabu muhanga mmoja anamdhibiti muhanga mwingine, hivi hatujiulizi hili?
Nakuhakikishia akikanyaga hapa Tanzania lazima atapotezwa na wasiojulikana na hivyo kupoteza ushahidi!
 
Back
Top Bottom