Baada ya mahojiano ya Chief Odemba na Tundu Lissu leo nimeelewa kwa nini dereva yuko Ubeligiji

Baada ya mahojiano ya Chief Odemba na Tundu Lissu leo nimeelewa kwa nini dereva yuko Ubeligiji

Waliomkosakosa? Risasi 16 zilipenya mwilini. Tosha kumuangusha hata tembo! Hakuna cha ujinga labda upumbavu kwa waliopanga tukio.

Anyway, Lissu leo hii ni jinamizi linalosotesha watawala. Hata JPM hakuwa na ujasiri wa kukutana na Lissu mpya face to face au kupeana mikono. Hata kutaja jina lake tu.

Nakuhakikishia akikanyaga hapa Tanzania lazima atapotezwa na wasiojulikana na hivyo kupoteza ushahidi!
Tafakari dereva anaushahidi gani?, labda ushahidi wa mambo ya bosi wake? (Lichukue tukio jipe wewe binafsi utapata jawabu)
 
Waliomkosakosa nao wajinga sana

Over!
Unajitambua wewe? Siku hao unaowalaumu kwa kukosa shabaha wakulenge wewe au mwanao urudi hapa kushangilia ujinga wa wanasiasa wendawazimu!
Mna polisi, mahakama na majaji mnaowateua wenyewe na magereza pia. Mlishindwa nini kufuata utaratibu wa kumshitaki na kumfungia?
Mungu amekuleta ubaoni Leo huenda anataka kukutumia wewe ukammalize Kama ulivyomfanyia yule nduguyo! Nonsense!
 
Yaani serikali itake kukua tundu lissu imkose?!!!!!!! Mnaumwa nyie, chunguzaneni vizuri chamani kwenu huko mnakobinywa na mwenye kigoda chake Huku nje mkijifanya kuchelewa ilhali ndani ya nafsi hampendi.
Jaribu kuishirikisha akili yako vyema kabla uandike huu upuuzi wako hapa! Kama kwenye chama Chao Kuna muuaji kwanini basi polisi isichunguze na kuwabaini? Au nao wapo juu ya Sheria? Unaichafua polisi kimtindo siyo? Yaani muuaji awe cdm halafu hao policcm wamwache tu badala ya kuchukua ujiko ili wapande vyeo! Na zile cctv camera kwenye nyumba aliyokuwa akiishi kalemani zilinyofolewa na cdm?
 
Tafakari dereva anaushahidi gani?, labda ushahidi wa mambo ya bosi wake? (Lichukue tukio jipe wewe binafsi utapata jawabu)
Ongeza fikra, kama unaweza na kama uko honest.

Katika mazingira ya sasa, julize: dereva akiwasili Tanzania, akaripoti kituo cha polisi kisha kupotea kabisa kama kina Soka, taarifa na HITIMISHO la polisi litakuwaje?
 
Aliyewahi eneo la tukio alikuwa ni nani?
Aliyewahi kutoa taarifa ITV ni nani?
Nani aliyetoa kamera za usalama [mahali ambapo polisi wapo muda wote]?

Nani alichunguzwa baada ya Lissu kutoa taarifa kuna gari imekuwa ikimfuatilia majuma mawili mfululizo[alitoa rangi , aina na namba ya gari husika] polisi gani alichukulia uzito kuchunguza?

Kwanini Makonda anahusishwa sana na tukio hili?

Je serikali iliwahi kutoa maelezo yoyote juu ya ile barua ya Makonda na mkewe kuzuiwa kuingia marekani kwa kunyima watu haki ya kuishi?
 
Ongeza fikra, kama unaweza na kama uko honest.

Katika mazingira ya sasa, julize: dereva akiwasili Tanzania, akaripoti kituo cha polisi kisha kupotea kabisa kama kina Soka, taarifa na HITIMISHO la polisi litakuwaje?
Binafsi sio tatizo kwa dereva kabisa, naye ni muhanga kama lissu, walitaka kuuwawa, aidha labda dereva awe alikuwa informer kueleza bandits wapo wapi kwa muda fulani.
 
Binafsi sio tatizo kwa dereva kabisa, naye ni muhanga kama lissu, walitaka kuuwawa, aidha labda dereva awe alikuwa informer kueleza bandits wapo wabi kwa muda fulani.
Kwa fikra zako, polisi wako zero kabisa katika kufahamu tukio hili hadi hapo dereva wa Tundu Lissu atakapokuja Tanzania na kuwaeleza kilichotokea na "hao aliokuwa akiwasiliana nao"?

Halafu polisi hawajaweza kabisa kutumia utaratibu wa Interpol kuwasiliana na dereva kumhoji tangu alipokuwa Kenya na sasa Belgium, kama alivyouelezea Lissu? Yaani, kwa mawazo yako, LAZIMA dereva arudi Tanzania ili wamhoji kwenye vituo vyao vya polisi, sio?
 
Itakumbukwa kuwa IGP Simon Siro alisema polisi wameshindwa kuendelea na uchunguzi wa kisa cha Tundu Lissu kupigwa risasi kwa sababu hakuwepo Tanzania. Lakini hata baada ya Lissu kurejea nchini bado polisi walisema hawawezi kuendelea na uchunguzi hadi dereva wake naye arejee kwa sababu ndiye aliyeshuhudia risasi zikipigwa. Lakini pia hadi leo polisi hawajafungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo la kijinai na kigaidi.

Katika mahojiano hayo Lissu amesema anaishtaki kampuni ya Tigo kwa kuhusika kwake kutoa taarifa zilizofanikisha Makonda na genge lake kumpiga risasi.

Kwa sasa Tundu Lissu amekamilisha maadalizi ya kufungua kesi hiyo na miongoni mwa watu watakaoitwa kutoa ushahidi ni polisi, Makonda na dereva. Kwa sababu hiyo ni wazi dereva ni mtu muhimu sana katika kesi hiyo na kuja kwake nchini kunaweza kusababisha ushahidi wake kupotea au kupotezwa. Nadhani imeeleweka " kupotea au kupotezwa"!

Bila kusahau yule kibopa alitekwa akawaona watekaji lakini hadi leo kimyaaa!
 
Back
Top Bottom