Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Du! Watu tunadanganywa kweli! Kabla ya vifurushi vipya kutangazwa Halotel ilikuwa mtu anapata kifurushi vya Internet GB 5 mpaka 7 kwa wiki kwa bei ya 5,000sh. Baada ya mabadiliko ni sh5,000 GB 2.2 na dakika 30 mitandao yote.

Kama ni kweli Serikali wamesitisha kwanini nisipate GB 5 mpaka 7 kwa wiki kwa sh5,000?
 
TCRA, Dr. Ndungulile mnatufanya malofa, bei bado ni ile ile waliyoongeza...natumia TTCL na Vodacom hawajashusha bei ya data! Shame!
 
We jamaa usisubiri mpaka utumbuliwe ;jitokeze hadharani chap achia ngazi.

Uzi tayari hivyo.

@mods naomba isomeke Ndugulile hapo kwa title
 
Huu uzi unafutwa/hamishwa sasa hivi. 😊
 
We jamaa usisubiri mpaka utumbuliwe ;jitokeze hadharani chap achia ngazi...
Huyu jamaa akipigwa chini kutakua na furaha kwa watu wengi sana. Na itaweka heshima kwa wale viongozi wote wenye kufanya maamuzi yasiyo na maslahi kwa wale waliowapa dhamana.

Na mama ataogopwa zaidi ya Jiwe na atahistahili heshima na sio yale mapambio yuliyokua tunalazimishwa tuimbe hapo awali wakati hakuna sababu ya kufanya hivyo
 
Kweli mkuu
 
Hii serikali ni ya hovyo sn, unatengeneza tatizo alafu unajidai kulitatua tena wewe mwenyewe
 
Nadhani ifuatiwe na kumsaidia kazi huyo waziri Ndugulile.Maana ameshindwa.yaani badala ya kuboresha sector yeye ameenda kuharibu.

mimi nilishitukia pale alipotoa kauli ya kutaka watu waache kutumia whatsap calls kupiga International calls.kwamba serikali inakosa mapato.

Hivyo alikuwa na mpanga wa kutafuta muarobaini wa kuzuia calls kwa njia za Whatsap,na nyinginezo kama skype. Sasa si ni kwamba huyu anatumia akili za zamani kutatua matatizo ya kisasa.Lazima atuumize tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…