pandagichiza
JF-Expert Member
- Jul 9, 2013
- 5,248
- 3,663
Habari haina ukweli wowote ipuuzwe.Habari zilizo teka mitandao na nje ya mitandao ni taarifa ya vifurushi vilivyo badilishwa.
Hii ilinilazimu kuandaa uzi maalumu usemao Tanzania tupaze sauti kupinga mfumo wa vifurushi vipya
Kwa namna moja au nyingine nilionekana kama naropoka tu.![]()
Lakini siku ya leo mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wameliona hilo na kuja na taarifa hizi👇
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.
Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.
“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.
Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.
Sauti yetu imesikika.
Hadi muda huu tigo sh 1500 unapata mb 300