Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Baada ya serikali kutoa tangazo la kusitisha bei mpya ya vifurushi hasa vya data bado makampuni yamekaza shingo yameongeza bei na hayajarudisha kama ilivyokuwa awali huku suala hili likitafutiwa suluhisho . Je, jeuri hii inatoka wapi?
 
Nadhani madame Samia Jumanne anaweza kufanya jambo kwenye hii Wizara inayoongozwa na daktari wa binadamu. Alizungumza Jana kwenye hotuba yake kuwa anawapanga Mawaziri kulingana na angalau taaluma zao ziendane na matakwa ya wizara husika atakayokwenda kuiongoza!

Ni wakati sahihi kumpeleka huyu Ndugulile kunakomfaa yaani wizara ya afya kwani huku kwenye mawasiliano anakwama mno! Madame tutanyie wepesi Jumanne mbali!
Sasa Dr wa binadamu wapi na wapi? Na izi elimu zetu za kumeza tu bila kujiongeza haya ndo madhara yake, anadanganywa nae anaingia mkengee huku kwenye ICT hakumfai aende alikosomea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walikuwa wanapima upepo tu na hili tulilisema humu.

Mitandao ina nguvu sana!

Dr.Slaa sasa atapongeza uamuzi huu
Hivi unafikiri ingekuwa ndo yule Hayati ambae hivi sasa nyama nyama zake ndo zinaishia, unadhani wangesitisha?! Sana sana hapa ingekuwa tunasubiri vichambo tu hapo kesho wakati wa Sala ya Pasaka!
 
Na mafuta jamani, yamepotea especially ya alizeti na ukiyakuta hiyo bei balaa lita 5 elf 30 badala ya elf 22.
Hii nguvu ya kulalamika pia mngeielekeza kwenye mambo ya sukari, petroli, unga, nauli pindi a
 
Hizi menu mbona bado hazijarudi normal?au ni mimi tu ntakua sio Mtanzania?
 
Hizi ni taarifa za kubumbaa, wametuchezea kang'ombaa tutulie ila hakuna mabadiliko yyte kweny hizo menu espl Halotel.
 
We nawe huna hata akili. Sasa unadhani yeye alikua hajui?
Rais hujua kila kitu kanachifanywa kwa hyo tumpe muda hata wiki 2 bado hajamaliza watu wameanza kumuona huyu mama muungwana sana kiliko watangulizi wake [emoji354] itaongea watanzania kupongeza na kukaataaa haichukui hata muda.
 
Habari zilizo teka mitandao na nje ya mitandao ni taarifa ya vifurushi vilivyo badilishwa.
Hii ilinilazimu kuandaa uzi maalumu usemao Tanzania tupaze sauti kupinga mfumo wa vifurushi vipya
Kwa namna moja au nyingine nilionekana kama naropoka tu.
Lakini siku ya leo mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA wameliona hilo na kuja na taarifa hizi👇
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya bei mpya ya vifurushi yamesitishwa kwa muda.



Hata hivyo, amesema uamuzi huo utahusu vifurushi vya data pekee huku vile vya ujumbe mfupi wa maneno na kupiga zitaendelea kama ilivyotangazwa mapema leo Ijumaa.



“Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida,” amesema Mwakyanjala alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu dakika chache zilizopita.



Kanuni ndogo za gharama na tozo za vifurushi, utangazaji wa huduma na ofa maalum zilizotungwa na TCRA, zimeanza kutumika leo ambapo, matumaini ya wengi ilikuwa ni bei za vifurushi kupungua lakini ikawa tofauti.


Sauti yetu imesikika.
Aliye sikia kilio chetu ni mama yetu mpendwa, Rais Samia Suluhu Hassan na Wala sio TCRA
 
Back
Top Bottom