Baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama ni timamu, je, tumshauri to do "The needful?" au akomae nao, till they do him away?

Mkumbusheni afanye hesabu ndogo tu 2025-1992 =......
Hilo jibu la hapo hicho kizazi ambacho nyumba moja kuna shabiki wa yanga,lipuli,simba na dodoma mji tafsiri ya haraka ni kuwa "hakuna kuogopana"

Mkumbusheni pia tunaenda kipindi ambacho watu watamchagua mtu wao .....
 
Wakati Ndungay unawakanndya na kuwashambuliwa na kuwadhihaki wabunge wako kina Lema, Lissu na Mbowe ukijiona mtukufu Sana kisa unaalikwa Sana Ikulu, hukujua wakati hukuta.

Muosha naye huoshwa. Hapa duniani hatuna wakati udumuo. Tenda haki kwa wote maana hata wewe kesho yako huijui.
 
Kesi inafunguliwa soon huko Arusha mkuu.
 
Mimi nawaza tu kale ka elfu 27 nilikolipa tangia october kwa ajiri ya kuletewa umeme kwa umbali unaohitaji nguzo tatu kama bado katafanya kazi ama laaa, nchi yetu ni kama vile inazunguka Roundabout , tunaenda na kurudi pale pale
 
Nadhani ni muda wa bunge kuisimamia serikali iondoke kwenye kuwa rubber stamp ya serikali. Nadhani tabia ya wabunge kutetea serikali bungeni imepelekea kujishushia heshima yake kiasi Cha speaker akitoa maoni yake anaonekana msaliti.

Bunge lisikubali serikali ikope mpaka imepata maelezo ya kutosheleza. Kama Bunge lingesimama kwenye nafasi yake huu mkanganyiko usingetokea. Bunge lihame kwenye mrengo wa kutetea serikali na ihamie kwenye mrengo wa kuisimamia serikali na ikibidi kuweka zuio la kukopa madeni mengi.
 
Kama ni spika wa bunge nakubaliana nawe ila kama ni ndugai ntakupinga milele.

Hana legitimacy ya kuhoji hilo.
 

Pascal acha unafiki wako, huyo unayesema mtu wenu amesingiziwa kipi ambacho hakusema kwenye ile clip? Ukisikiliza kwa makini bila ushabiki utasikia pale anapohitimisha na kusema TUONE hapo 2025 kama hao watu wa tozo watakubalika au la!!! Sasa huo sio usemi wa kuonesha stress za uchaguzi hapo ifikapo 2025?
 
Mkuu kuna mambo kama wewe huyajui, au wengi wetu hatujui haimaanishi kwamba kila mtu hayajui.

Ndugai AMEKOSA SANA. ameomba radhi Watanzania wote ukiwemo wewe kwa kuwa anajua AMEKOSA SANA. Sasa nyinyi wengi wenu hamjui AMEKOSA nini lakini yeye anajua
 
Blai hatakiwi kuresign, anatakiwa kupambana, hii ni mihimili miwili tofauti, blai anatakiwa atafute uugwaji mkono ndani ya mjengo ili vita iwe kali zaidi
 
Ni kweli lakini sio bunge litakaloongozwa na ndugai.

Bunge la Ndugai ni dhaifu na halifai. CAG Assad alikuwa akikagua na kuwapelekea ripoti ili achkue hatua lakini ni nini kilitokea???
 
Nazani kuna shida kwanza ya washauri wa kisiasa wa Presidaa wanampa manano ya kumpanikisha hiyo kauli ya homa ya 25 kapewa aseme na aliyefanya hivyo anatriger mgogoro tu, narudi kwenye hoja hapo Kusema jamaa afanye kinachotakiwa itategemea na utashi wake na namna uzoefu ulivyo, Tanzania ukisema hafu ukasusa ni kosa kubwa watakushughulikia ni vema ubanane nao humohumo hadi wao wakutoe ambapo najua kupata 2/3 ya kura ni ngumu sana
 
Point point, haya yote yanatokana na kua na katiba mbovu
 
It is Never too late to do the right thing. Jamaa yetu asisubiri upepo uvume ili aione ilipo njeti ya Kuku, wakati ni huuhuu kabla vikao vya bunge kuanza hivi soon Na kukosa mahali pa kuficha USO wake, maana sio zamu za wakatoliki Na waislamu tu Bali sasa ni zamu ya wanaume Na wanawake kupokezana, hivyo mama tulia akson aanze kupiga jalamba in case worse becomes worse.

tulisemaga sisi kuwa madaraka ya rais ni makubwa mno wakadhani ni kilele za wapinzani tu kumbe sivyo bwana, ni kwa faida jata ya wavaa kijani. No safe zone.
 
Ki-Katiba Spika Kama anatokana na wabunge atapoteza nafasi ya uspika Kama hana sifa za kuwa mbunge. Sifa ya kuwa mbunge ni kuwa mwanachama wa Chama cha siasa! Rais ndiyo Mwenyekiti wa CCM kwa hiyo Chama kikimvua uanachama tu amekosa uspika na ubunge na hata Mafao halipwi.

Ila Ndugai ni mburula na wenzie akina Bashiru wamemtanguliza yeye naye kaingia kingi.
 
Hiyo haiwezi kutokea Rais Na Mwenyekiti wa chama Na amirijeshi mkuu na mkuu wa hazina ya nchi akose LA kufanya kuwasambaratisha maadui zake. Hiyo ni ndoto ya mchana kweupe, ccm asilia IPO intact, hao wanaobweka ni wale neo-ccm wageni Na wachanga kwenye chama kama akina wale watoto waliofishwa bungeni kupunguza shombo za kitoto. Mzee Yusufu Makamba mmoja ni sawa Na akina polepole 3000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…