Jana mtu wa CCM anayejiita mchungaji wa Mungu, Masanja Mkandamizaji aliweka picha za mradi wa umeme wa maji huko Lesotho na kuuita wa Stiglers Gorge.
View attachment 1530629
Hiyo ndiyo picha ya Masanja ya jana.
Sasa leo msemaji mkuu wa serikali ameisifia serikali ya awamu ya tano kwa upanuzi wa kiwanda cha ASAS Dairies huku akiita kama juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuongeza ajira na unywaji wa maziwa nchini. Hiki ni kiwanda cha mtu binafsi na serikali haihusiki nacho kwa namna yoyote ile zaidi ya muwekezaji huyo kulipa kodi pale anapouza na kuagiza bidhaa. Kazi kweli kweli!
View attachment 1530634
Kwa siku za hivi karibuni msemaji mkuu wa serikali amekuwa akitoa takwimu za upotoshaji mkubwa hasa baada pia ya jana kuhutubia vyombo vya habari na kusema kuwa kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2020 pato la Tanzania limefikia shilingi za kitanzania TRILIONI 122.5! Sijui kwanini anajiita "Dokta" Hassan Abbas. Haelewi hata maana ya "TRILIONI"