Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sometimes naona wanasema 'redirected'
huku JF sipati...
Kijana huna kazi yakufanya?Wakuu salama?
Kumekuwepo na wimbi la watu kupotea kisha kupatikana hai au wakiwa wamekufa. Pia kuna wengine wamepotea na hawajaonekana mpaka sasa. Matukio yote yamekuwa yakiitwa "Kutekwa na watu wasiojulikana".
Kinachoshangaza ni kuona wanaorudi baada ya kupotea wakikaa kimya kama hakuna kilichowatokea. Mfano mzuri ni tukio la kutekwa JamiiForums siku ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwa kuwa vijana wengi tulikuwa bado sekondari, naomba kujua kama JamiiForums waliita press conference kuelezea watekaji wao walikuwa wanataka nini.
Ufafanuzi huo utatupa mwanga sisi vijana kwa sababu wengi wetu tunaamini watekwaji wa mwanzo walikuwa ni JamiiForums Where We "dare" to talk Openly.
Wote waliofanya haya.JamiiForums Message
Tumerejea: Tupo imara zaidi!
Wakuu,
Tunafarijika kuwafahamisha kuwa tumerejea hewani baada ya kupata mashambulizi ya makusudi yenye kulenga kuzuia upatikanaji wa huduma kwa watumiaji wa JamiiForums (DDOS Attack) kwa takribani masaa 7, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 2 usiku.
Mashambulizi haya yaliyolenga kuidhoofisha miundombinu yetu, yamefanywa kwa kupangwa na kwa kiwango tulichobaini kuwa yalifanywa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mashambulizi ya kimtandao.
Tunalaani kwa nguvu zetu zote kitendo hiki na vingine vya mwelekeo kama huu vyenye kulenga kunyamazisha sauti za wananchi.
Timu yetu ya wataalamu itaendelea kufanya kazi kwa umakini zaidi katika kipindi hiki cha Uchaguzi na tunaomba ushirikiano wa wanachama na wadau wa JamiiForums pale mtakapoona huduma zetu zinasuasua kwa namna yoyote ile katika upatikanaji. Wasiliana nasi kupitia support@jamiiforums.com
Tunawashukuru sana kwa uvumilivu wenu katika kipindi hiki na tunawatakia kila la heri katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu.
Uongozi,
JamiiForums
Ila topic imesema 7 years.
Maybe was network problems huko kwenu.
Huku mjini haikuwepo hiyo
Nakumbuka kile kipindi nadhani lile ndio mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kuikumba JFJamiiForums Message