Baada ya mashambulizi: Tumerejea hewani, Tupo imara zaidi!

Baada ya mashambulizi: Tumerejea hewani, Tupo imara zaidi!

Status
Not open for further replies.
Nikajua ni nilivosikia kuwa mitandao yote itazuiwa kipindi hiki. Asanteni
 
Poleni Max.......Tulikuwa bar moja jana usiku na tulijadili suala hili!!!
 
Nikuongeza umakini tu. Maana kuna watu uwepo wa JF kwao ni headache. Lakini wataumia sana, wanapoweka ubavu wao wenzao walishapitia na wanakaza mwendo. Pamoja sana wakuu.
 
Max naomba uweke IP addresses za hao attackers kwenye hii thread tuwajibu.
 
Dah! nilikata tamaa lakini niipojaribu asubuhi hii ikakubali nikafurahi
Hongereni kwa kazi nzuri.
 
Happy to be back again, dahhhh jana nimeteseka balaa yaani siomchezo.
 
Poleni sana, Jana ilikuwa kama vile tuko msibani
 
Ndugu Founder Maxence Melo Jana umetoa maelezo kiasi juu ya site yetu pendwa kupotea hewani hata wakati huu pia bado inasumbua Nashindwa kuelewa kwanini hamkujiweka imara haswa kipindi hiki cha uchaguzi Je hamkujua kua forum hii ni Pendwa na ndio inayotoa latest news kuliko popote?! Nadhani picha mnayojaribu kututengenezea members wenu ni kuwa Tuamini mnatumika kisiasa kutopatikana Hewani ..Siasa sio safi kabisa na ni vyema kuficha hali ya ushabiki wazi wazi
 
Last edited by a moderator:
Hongereni kwa kuirudisha na kuipaza JamiiForums angani. Washindwe na walegee...
 
Hi JF Team,
Poleni sana kwa shambulio hili. Kuna wengine tuna idea na mambo ya mitandao, nilipoona tu jana kuwa JF haiko hewani nikajua kuwa huo ulikuwa ni uharamia na njama za maksudi ili kuzuia kile kilichokuwa kinajiri kwenye matukio ya kupiga kura ili kuwanyima haki Watanzania wasipate taarifa muhimu za Uchaguzi.

Tunalaani kwa nguvu zote kitendo hiki cha kiharamia.
 
du, pole sana mkuu. nilipoona tu jf haipatikani nikajua sisiemu wameishafanya ugaidi wao.
 
Pole na hongera, jana nililazimika kulala mapema, leo walau nitakuwa na sababu ya kutabasamu ukizingatia kwenye kata yangu matokeo yanaonesha ukawa ipo juu kama nyota.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom