Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

Kwa mfululizo huu, tusipoteze rasilimali zetu kwa uchaguzi. Hebu tupiganie viti vingi vya ubunge na udiwani, huko kwenye urais labda tumwachie Lipumba azurure bure.

Karibuni ACT, Karibuni CHADEMA
 
y January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.

Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

Igiza na wewe tuone,mji wenyewe umekushinda hadi utegemee dada yako akupe pesa.
 
kwa hiyo hata wewe Hassan Wenger nawe ulifaidika kimaslahi ndio maana unapiga debe kwa sana?
 
hamna wachungaji hao matapeli tu, jana sheikh wa bagamoyo amewakana ma sheikh ubwabwa walienda kutega nyama choma kwa lowassa
 
y January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.

Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

kama mlishindwa kuwavua gamba hawa hawa wanaotumia nguvu za maigizo na ambao wamekosa uadilifu, mtawezaje kuwazuia leo hii kwa maneno yale yale mliyotumia wakati imetangazwa chama kinajivua gamba mheshimiwa?
 
Hii nchi wenye akili za misukule ni wengi kuliko wenye utashi wa kibinadamu.
 
Nakubaliana na wanaosema huyu lowassa hafai kuwa Rais. Ni mroho na mlafi wakila kitu. Iweje anunue nchi hii. Maana kama ameweza kutapeli wasomi, mashekhe, wachungaji na wanafunzi wa elimu ya juu munazani wakulima na wafugaji watawezaje kumpinga? Mbaya zaidi hata machinga waokota makopo na bodaboda nao wameshikiwa akili na huyu fisadi.

watu wanachukua pesa zake si hazina shughuli,lakini hao wote hakuna wa kumpigia kura,kama ccm watamchagua
 
sijui huko atakuwa ametoa sadaka kiasi gani kusababisha kila mchungaji kuacha kanisa lake na kuandamana kwa ajili ya kushinikiza Lowasa agombee urais?
 
Hawa wachungaji toka kona zote za nchi ni lini walikutana wakaafikiana kuwa mgombea anayefaa ni huyo! Hii ni zaidi ya usanii, ni hatari sana. Vyombo vya usalama viamke.

Wewe umeamka umechukua hatua gani?

Utatulia tuu
 
Washehereshaji wa harusi (MC) huwa wanafanyaga mambo kama haya:;

1. Sasa ni zamu ya wakwe kwenda kumpa bwana na bibi harusi mkono wa heri.

2. Baada ya wakwe sasa watafuata mashangazi wa bwana harusi

3. Baada ya mashangazi sasa wanafuata wajomba wa bwana harusi

4. Sasa ni zamu ya wafanyakazi wenzake bwana harusi.

5 Bado list ni ndefu .....................................

Lowassa tunaomba uweke ratiba kamili ya makundi yote uliyopanga nayo kuja kupiga picha hapo dodoma Haya mambo ya kutuambia katika hali isiyo ya kawaida hatuyataki sisi siyo watoto wadogo.
 
Kuna wakulima 1000 nao wanataka waje,mwambie el awawezeshe nao waje dodoma.
 
Back
Top Bottom