Baada ya matendo yake sina hisia nae tena, nifanyaje?

Sio wote tuna uoga huo budaa, kwanza kujichua mbele yake ili iwe nini wakati mijulubeng ipo!!! Halafu ni suala la muda tu hiyo kulia katikati ya game ni mbaya mno na very soon kuna kijana wa ovyo atajipakulia minyama,
Atafanya yote hayo ila atabaki chini ya himaya ya mume wake
 
Sijakurupuka kumjibu hivyo,kukaa na ntu humpendi nyumba moja ni hatari,ndio chanzo cha vifo vitokanavyo na mapenzi,imagine hiyo mwanamke ndio anakupikia chakula,akiamua kukuwekea sumu au uchawi wake unekwisha,utakufa na yeye apumue vizuri.
Usalama wa huyo mwanaume huko hatarini

Huyo mwanaume angekuwa kapuku angeshaondoka,ila inaelekea jamaa ana malli sasa bibie anaona akiondoka atakuwa amejidhulumu.

Akipata mshauri mbaya jamaa atarogwa au kulishwa sumj
 
Good advice
 
Jamani pole Sana kwa magumu uliyopitia ila msamehe tu mumeo ili maisha mengine yaendelee.
Kama Kweli mumeo amekiri makosa yake na ameamua kujirudi wewe msamehe tu yaishe usiendelee kumwekea kinyongo utaumia bure
 
Ni kweli tuna mapito mengi lakini hili lako linasisimua kwa ubaya na uchungu , yaani kufikia hatua ya mtu anakunyima tendo hadi unatazama porn pembeni yake huku anaona anasikia na hafanyi chochote kukusaidia huyu si mwanamme wa kawaida ni jitu la hovyo ila lisamehe tu.
 
Kunà binadàmu wapumbavu sana.
 
 
Katika vitu navichukia ni mtu aliyekosea kujifanya victim na mbaya zaidi kuhisi msamaha wa ghafla na wa haraka ni stahiki yao pasipo kuangalia madhara waliyoyafanya.

Pamoja na yote hayo, bado unampenda sana mume wako ndio maana unaumia lakini huwezi kuondoka kwa hiyo yoyote anaekushauri kuondoka. Hajaelewa unavyohisi.

Unajua mumeo ni msaliti, unajua mume wako hana misimamo ya kiume kiasi kuendeshwa na mchepuko, mumeo hana kiasi wala heshima kwako ndio maana akacheat na mtu wako wa karibu, mumeo ni mjinga na hana ufahamu na hajali sana hisia zako. Ila katika yote hayo bado umempenda na ni furushi ulilolochagua hivyo huna ubavu wa kuondoka. Pambana nalo mkuu
 
Hapo kuna sheria ya All or nothing lazima itumike.... ama uamue kumsamehe kwa kujifunza kusamehe na umsamehe yeye na rafiki yako ama dai talaka.... zaidi ya hapo utakayeumia ni wewe....

Hints
Msamaha ni muhimu zaidi kwako kuliko kwake... Unasamehe si kwa sababu ya yeye alivyo la hasha ni kwa sababu ya wewe ulivyo na mahusiano yako na Mungu wako.... Usiposamehe utaendelea kuumia na utakufa.... Ukifa kumbuka maisha yataendelea....
 
Huu ni ushauri bora sana, kuongezea hapo ni kumtanguliza Mungu ktk hilo na kila mara kusoma na kujifunza maandiko yana tuasa nini ktk maisha yetu ya kila siku.
 
Angekua mwanaume ungempa huu ushauri??
Ningempa ushauri huo huo, bila kujali jinsia. Kila mtu anastahili nafasi ya kuponya na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maisha yake. Kuachana ni uamuzi mkubwa ambao unahitaji kufanywa kwa umakini na baada ya kutafakari kwa kina.

Kama mtu anahisi kuwa hawezi kuendelea na uhusiano kutokana na maumivu na usaliti, ni muhimu kuchukua hatua zinazofaa kwa ajili ya afya yake ya kiakili na kihisia. Hata hivyo, ni muhimu pia kujaribu njia za kuponya na kuona kama kuna nafasi ya kurekebisha mambo kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.
 
Kabisa cute...hata ukipata watoto kama ndoa inakuletea maumivu Kila siku ni Bora ukimbie....kisichochako si chako tu
Watu hawajua kwamba ,hapa duniani hakuna mtu atakayekupa furaha isipokuwa wewe mwenyewe. Unaishi kwa mateso kwa sababu sababu ya kiumbe ambaye ameamua kwa maksudi kukusaliti.
Kazi kwelikweli.
 
Unajikaza nini huku hupendi,si uondoke.
By the way tunauza mikaa na dawa za panya kwa bei ya jumla.
Hatutoi ushauri.
Namshangaa. Ngoja afe kwa stress. Watakaoumia ni watoto wake ,wazazi na ndugu zake. Hao wengine siku unazikwa baada ya wiki wanakusahau, na huyo mume anavuta kifaa kingine chap.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…