Avatar
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 11,128
- 11,921
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Diamond 3- 0 zari
Haya majamaa ya Chadema yana roho mbaya kama wachawi yaani yalitamani Taifa stars ishindwe eti kwa sababu Magufuli ni rais.
Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) leo majira ya saa 12:00 jioni katika Uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar inacheza na timu ya Taifa ya Uganda(The Cranes) katika mchezo wa kufuzu kucheza Michuano ya Mataifa ya Afrika(AFCON) nchini Misri
Lesotho yenye alama sawa na Tanzania itakuwa ugenini inamenyana na Cape Verde.
Msimamo wa Kundi ulivyo kabla ya Mechi za mwisho leo
Taifa Stars ili kufuzu AFCON pia inategemea na matokeo ya Lesotho ambapo iwapo Lesotho. Taifa Stars itafuzu iwapo itashinda dhidi ya Uganda na Lesotho atoke droo au afungwe na Cape Verde
Lakini iwapo Taifa Stars na Lesotho zote zitashinda badi Stars inabidi ishinde magoli mengi na kukaa juu ya Lesotho kwenye msimamo wa kundi kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga
UPDATES:
Mashabiki wamevunja geti upande uwanja wa Uhuru na NBSP kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Taifa Stars na Uganda.
Nguvu ya mashabiki imewashinda polisi na walinzi wengine na kulivunja geti hilo saa 10.33 jioni hali iliyowalazimu polisi kujipanga upya kuzuia hali hilo.
Katika kipindi cha takribani dakika tano kabla ya polisi kuzuia mashabiki wengi tayari walikuwa wameingia na kwenda moja kwa moja jukwaani
***
View attachment 1053045
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali awanaendelea kuingia uwanja
***
Polisi imewatawanya kwa mabomu ya machozi mashabiki waliotaka kuingia uwanjani kwa kupitia uwanja wa Uhuru katika mechi ya Taifa Stars na Uganda, kutokana na msongamano uliopo kwenye mageti ya Uwanja wa Taifa
***
Vikosi vinavyoanza mchezo wa leo
***
Taifa Stars inapata goli la kuongoza dhidi ya Uganda goli lililofungwa dakika ya 21 na Saimon Msuva. Msuva alipokea pasi safi kutoka kwa John Bocco 'Adebayor'
Aidha, katika mchezo mwingine matokeo katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde bado ni 0-0
***
MAPUMZIKO: Taifa Stairs inaenda mapumziko ikiwa inaogoza kwa goli 1-0 dhidi ya Uganda. Katika mchezo wa Lesotho na Cape Verde milango bado ni migumu
Stats zilivyo hadi Mapumziko
***
Taifa Stars inapata bao la pili kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Erasto Nyoni baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari dakika ya 51.
***
Goli la tatu kwa Tanzania kutoka kwa beki Aggrey Morris akimalizia kwa kichwa pasi ya John Bocco dakika ya 57
***
FULL - TIMEStats baada ya mchezo kumalizika leo Machi 24, 2019
View attachment 1053145
View attachment 1053149
Baada ya matokeo ya leo, Tanzania na Uganda zinafuzu ambapo Uganda inaongoza kundi ikiwa na alama 13 na Tanzania ikiwa na alama 8
Kwa taarifa yako na Burundi ya Nkurunziza imo!
ametoa ule mpira upande wa mashariki akapiga locomotive bent bila kusimama ya kwanza alipiga inaitwa reo bent anayumba akiwa amesimama beki akakubali kutoka kwenye njia akaamua kuondoka akajabeki wa pili akapiga locomotive bent huku anaenda kama anataka kupiga back pass akageuka, quick turn "tunaita" quick reflect akapiga mpira mmoja lion pass "stand volley" mpira unaofanana kama chini unapofungia tai hapa basi kilichotokea kwa Aggrey Morris kwenda deep kwenye box akapiga side freak head kwenye paji la uso sio kisogoni sio usoni ngoma ikaenda nyavuni kushoto kwake ambapo ni kulia kwa goalkeeper Dennis Onyango hakuwa chap mpira ulienda taratibu sana lakini vipimo viwango na utulivu wa wa Agrrey Morris overlapping central back.
kwako Jesse John
Mie niliposikia jamaa yetu ndio anaongoza uhamasishaji wa ushindi nikajua ushindi ni lazimatujiangalie, kuna uwezekano wa uganda na tz mmoja au wote kufungiwa.........
hii game ilitakiwa tushinde moja bila au 2-1,,, hizi 4-0 sijui ngapi tayar zimeleta alarm
Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah wanywa pepsi serikali imetudharau sijui au inatuhesabia kama ni raia wa uganda?
Hahahahaaaaaa leo kupitia ofa hii lazima kuna watu watajifunza kunywa pombe
Naona munashangilia mitandaoni, uraian kila mtu yuko na mambo yake hata habari kuwa sitazi inacheza hawana.Nyie hater's wa Stars kisa itikadi za kisiasa. Watanzania wenzenu wamewasamehe ila inabidii mjitathmini na mbadilike.