Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Wewe kama hufanyi kazi shauri zako utaishia kuramba viatu vya chakubanga
In God we trust
 
Reactions: BAK
Wanajamvi,
Kwa takwimu zilizotolewa hivi majuzi na kuonesha Tanzania inashika nafasi ya 153 kati ya nchi 156 kwa kiwango cha furaha Duniani. Leo hii historia imebadilika angalau kwa masaa kadhaa. Endapo takwimu za "furaha" zingechukuliwa Leo, basi Tanzania Leo tungeshika namba Moja. Kwa ushindi huu wa Taifa Stars, nimeona furaha kuanzia kwa Mh. Rais mpaka kwa wananchi, Chama tawala mpaka kwa wapinzani, Walimu mpaka kwa wanafunzi. Ama kweli Leo Tanzania imeshika namba moja kwa kiwango cha furaha Duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama hakika baada ya miaka 39 ya kucheza soka la mchangani, kwa Mara nyingine Tanzania tumeingia kwenye record ya timu zinazoenda Misri kwenye mashindano ya Afcon kwa ushujaa mkubwa.
Rais wa JMT amesikika akiwapongeza wachezaji kwamba wamefanya Jambo zuri.
Faida ya Tanzania kushiriki mashindano haya ni kwamba tutaongeza wachezaji wanaocheza nje soka la kulipwa, tutarajie kuona sports academy nyingi kufunguliwa hapa Tz maana wawekezaji wengi (wa ndani na wa nje) wameona namna mpira unavyolipa hapa Tanzania. Social utility nazo zinaongezeka (watu wanakunywa bia nusu Bei now) na mengine mengi.
Hivyo kwa ukubwa wa heshima hii tulioletewa na taifa 🌟 namuomba Rais apitishe siku mbili za mapumziko kwa watu ili kusherekea historian hii ukizingatia bia imeshushwa Bei tuepushe ofisi zisiwe "hangover zone"
 
Shangwe la leo limezidiwa na la Simba dhidi ya AS Vita ni vita muraaa

Sent from my TECNO CA6 using Tapatalk
 
Duh. Nilitegemea swali hili lingetoka kwa dogo wa kindergaten.
Hujui mchango wa serikali ktk michezo na kuweka mazingira rafiki?

Kuna mijitu itapasuka kwa chuki na wivu dhidi ya stars kufika afcon.
 
Yeye ndio Mkuu wa Nchi

Kila Jambo likivurugika Kwenye Nchi Lawama anapewa Rais Kwanini likikaa sawa tusimsifu?

Hongera Dkt Magufuli kwa ushindi mfululizo kuanzia wa Simba, Hasana Mwakinyo Na Leo Taifa Stars

Wanafiki wakiongozwa Na Da Mange wameumbuka
 
Mange kasemaje kwani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada hujui kutumia akili ulizo pewa, popoma ww.

MGC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…