Niwape hongera sana wachezaji wa timu ya Taifa na wananchi wote kwa ujumla kwa kuwapa moyo vijana wetu na hatimaye tumeuona ushindi
Hamasa iliyojengwa ilikuwa kubwa sana. Kuanzia vyombo vya habari, viongozi wa serikali, wa kisiasa na hata wa dini wote kwa pamoja wali wapa hamasa vijana wetu kuufikia ushindi wa leo
Kilichofanyika uwanjani kinadhihirisha kwamba kumbe watanzania si kwamba hatuwezi, ila huwa tunakosa kitu kidogo sana ambacho ni hamasa katika kile tukifanyacho
Ukiangalia kuanzia mechi ya juzi kati ya Simba na wale wakongo na hii ya leo utagundua kumbe tukitiwa moyo tunaweza kufika mbali
Katika tasnia ya ualimu, walimu wanasisitizwa kuwapa moyo na ku wahamasisha wanafunzi kujaribu na kufanya kwa kujiamini katika masomo yao bila kuwakatisha tamaa wala kuwacheka pale wanapokosea
Taifa Stars kushinda leo goli tatu kwangu mimi naona wamewapa somo kwa vitendo wale wote waliohusika kufanikisha hamasa iliyokuwepo kwamba wasisubiri mwishoni tu kuja kutia hamasa.
Na pia hili ni somo kwa viongozi wetu kwamba watu wao wakipewa motisha, wakihamasishwa kwa lugha nzuri ya upendo na ya ushindi vitu vitafanyika vizuri tu!
Binadamu hufanya kitu kizuri pale anapokuwa huru na anapopewa motivation hufanya vizuri zaidi!
Tuache lugha za vitisho kwa wafanyakazi wetu wa chini, tuache mikwara kwa tunaowaongoza badala yake tutumie lugha ya ki ungwana, lugha inayohamasisha mafanikio... hakika tutatoka hapa tulipo.
AFCON, NI ZAMU YETU
Sent using
Jamii Forums mobile app