Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Mechi ilipangwa, waganda walikuwa hawana cha kupoteza, Museven mwenyewe mechi ya kwanza alifurahi kwa droo na kusema timu zote ni za nyumbani. Ingekuwa kwenya ungejua ujirani ukoje.
Mm naioenda stars ila natokeo yetu ni ya ujirani mwema.
Sikwenda uwanjani kwa sababu mazingira yote yalionesha tunashinda mechi, hata kama possibility ya kufuzu ilitegemea mechi ya Cape Verde na Lesotho. Nilijua hakutakuwa na ushindani wowote.

- 98% ya watu hawajui nini kinachoendelea, wao huamini kila kinachosemwa mdomoni, hawana maswali ni kufuata upepo

- 1.8% wanajua nini kinaendelea, kila jambo linapotokea huwa wanashirikisha bongo zao na kujua nini maana yake

- 0.2% Wanapanga kinachotokea, wanaanzisha matukio kwa sababu zao maalum.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakereka sana kila naposikia kila kiongozi anazungumza kuhusu hii mechi ya Taifa stars na Uganda akinza kwa kumpongeza rais wetu mpendwa Magufuli.
Nachojiuliza Magufuli anapewa pongezi ya kazi gani? Kati ya Magufuli na mashabiki na wachezaji ni nani wa kwanza kupewa pongezi?
Huu ni ujinga wapeni pongezi wachezaji na mashabiki kwa kufika na kucheza vizuri Magufuli hana hata chembe ya pongezi kwenye mchezo huu... Bora hata Makonda alikua kwenye kamati na kiki zake za msimu...


Sent using Jamii Forums mobile app
Alitoa milioni 5 mbona hatukuona matunda badala yake ikapigwa, jana yenyewe amekiri aliogopa kwenda uwanjani maana hakutarajia. Pongezi ziwaendee vijana kwa juhudi zao pamoja na kocha wao. Wameona mpira unalipa ukijionyesha kwenye mashindano makubwa kama hayo. Huu ndio wakati wa kujiuza kwa timu kubwa za nje
 
Mhhhh!!! Si kweli kama ni kuhonga basi tumewahonga na Lesotho, haikubaliki hata kidogo eti Uganda watubebe wakati huo huo matokeo yetu yalikuwa yanategemewa sana na Lesotho imekaaje ,na huko kwao walitufunga ngapi kiasi kwamba leo ionekane wametubeba? Basi kama ni wabebaji kweli wangetubeba toka mwanzo,mpira ni dakika 90 tukubali tu kwamba Leo timu yetu ilikuwa vizuri,na kwenye soka ndivyo ilivyo kwamba lolote laweza kutokea,mbona haya mambo yapo tu hata nje mara ngapi zile timu tunazozijua zina uwezo mzuri inatokea wanacheza hovyo mpka unashangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Issue ilikuwa ni kushinda mechi ya Dar, kufuzu ilitegemea mechi ya CV vs Lesotho. Kushinda Dar nilijua tutashinda hilo halikuwa tatizo kwangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi hasa chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?

Asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo

Asante kasi ya Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii kauli yako ina maanisha nn? [emoji116][emoji116]
"Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera zote kwa 100% ziwaendee Wachezaji hasa walofunga magoli bila kumsahau Kocha wao......!
Hizi hongera kwa Makonda ni UNAFIKI,UBAZAZI na kutaka Wanasiasa KUJITAFUTIA UMAARUFU usio na tija kwa Taifa na sanasana ni kuwagawa Watz.
CCM acheni hizi cheap politics.....mmezidi sana.Akifa mtu au ikishinda timu mnatumia kujitangaza..!Pambaf zenyu.
Kwakua wameshinda sio?,wangepoteza mechi zigo la misumali angebebeshwa Makonda sio!,"pathetic"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda aliwasiliana na Mkuu mwenzake ndio Vijana wakatufanyia wepesi.
 
Ushindi wa goli 3 kwa 0 ilioupata timu ya taifa stars leo dhidi ya Uganda na hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Nchi za African@ AFCON zitakazochezwa Misri mwezi June mwaka huu ni uthibitisho mwingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda ni hadhina kwa taifa kwenye upangaji na usimamizi wa masuala ya kitaifa.

kwa faida ya wengi ni kwamba Mh Makonda alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuiwezesha taifa stars kufuzu AFCON 2019 ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa na jukumu la kushirikiana na Uongozi wa timu kubuni mbinu na mikakati ya kiufundi ndani na nje ya uwanja, bila shaka kwa matokeo yaliyopatikana inahitaji kiburi na husuda na wivu kupinga kwamba hajafanikiwa.

Jukumu lingine kubwa lilikuwa ni kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji ya kupambana na kushinda. Katika hili la kuhamisha watu kujitokeza tumpe Kongole Makonda kwa niaba ya kamati aliweza kuwaunganisha watu maarufu kutoka tasnia za muziki, filamu, wanamitindo, wanasiasa na kuwaomba kutumia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhamisha wananchi na matokeo yake yameonekana uwanja ulijaa yaani zaidi ya watu 60,000 walikuwepo taifa.

Kwa kurejea baadhi ya mambo mengine mengi ambayo mhe Makonda amewahi kufanya;-

## kufanikisha kama kusaidia Walimu katika Mkoa wa Dar es salaam kupanda daladala bure,

## kufanikisha upatikanaji wa bima za afya @ toto kadi kwa mamia ya watoto ambao wametelekezwa na wazaz.

## kuwapatia viatu bandia walemavu, kuchangia matibabu ya wagonjwa mbalimbali nje ya Nchi.

## kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusu ardhi na kuwasaidia wakina mama hasa wajane waliodhurumiwa Nyumba na mashamba.

## kupanua huduma za kijamii kama vile ujenzi wa hospital Temeke, shule za sekondari na Msingi hivyo kuwawezesha wananchi na wanafunzi wengi kupata huduma.

Makonda ni binadamu pamoja na mafanikio hayo Lukuki aliyofanya katika kipindi kifupi ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa yaweza kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale amefanya lakini hayaondoi ukweli kwamba amejitanabaisha kuwa ni asset kwa taifa letu.
HII NI KWA HISANI YA BASHITE.
umekuja hivi baada ya punguzo la bei nadhani utakuwa ulimwagiwa sana ngoja stim zipungue akili ikurudie
 
Hongera hizo si kwa Makonda au mpenda sifa mwingine yeyote bali ni kwa wachezaji na kocha wao tu kwa jitihada zao zilizoiletea Tanzania sifa kubwa. We are all proud of them. Waganda walicheza kukamilisha ratiba walikuwa wameshafuzu. Kaeni chonjo mtakutana nao Misri bila wapenda sifa.
Sawa Mganda ,nimekusoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye benchi la ufundi aongezwe kocha kutoka nchi za kiarabu...
 
Back
Top Bottom