Baada ya miaka mitano ijayo namwona John Heche mbali sana kwenye siasa za Tanzania

Baada yamiaka mitano atakuwa anahekima, busara zaidi, hivyo atakuwa amekomaaa
 
Mwana CCM atamuongezea gari nyingine
 
Atahamia Ccm uchaguzi huu ukipita.Jifunze kwa kilichotokea kwa Prof. Kitila, Mch. Msigwa,Kafulila na usaliti wa Prof. Haruna.
Alivyoingia Lyatonga Mrema hali ya hewa kwenye vyama vya siasa vya upinzani mdudu aliingia baada ya kukabidhi tàarifa ya kazi aliyotumwa
 
Sio Heche mkuu, huyu anapoongea huwa anamanisha, labda john myika lakini sio Heche, huyu anakariba kama ya Tundu Lisu.
 
kiongozi mahiri utamgundua, kwenye, nyakati ngumu kama hizi.

kiongozi mzuri, hawezi kuwa upande hunukao damu.

Heche, nimemfuatilia hivi karibuni nimegundua ni tunu. ni kiongozi sio tu anajiamini bali, aongeyo yanatoka moyoni mwake kizalendo.

Huyu sio kiongozi, wa pangu pakavu, tia mchuzi. yamkini tunaomba Mungu amtangulie kwenye harakati zake.

ikumbukwe upande aliochagua ni upande wa haki, upande angavu usio na chembe ya dhulma.....upande ambao hauna damu za viumbe wa Mungu.

Hakika, namuona mh Heche akifika mbali na taifa litainuliwa na hawa watu wa hii sampuli.

ukisema ajibehave kihekima, hekima amfanyie nani?......sometimes hata wahubiri huangalia muktadha....yaani nini na kipi wakizungumze. aluta continua braza, mkondo wa matumaini unawategemea.
 
Upo sahihi mkuu, ndo maana nimesema after years the guy will be next level, ndani ya kuwa makamu kuna vitu atajifunza, vingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…