Baada ya Mume kufilisika Mke adai yuko tayari kuvunja Ndoa kuliko kurudi Kijijini

Baada ya Mume kufilisika Mke adai yuko tayari kuvunja Ndoa kuliko kurudi Kijijini

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Mdaiwa Tumaini Angumbwike (35) mkazi wa Makunguru ameiambia Mahakama ya Mwanzo mkoani Mbeya kuwa yuko tayari kutalakiana na mume wake kuliko kurudi kijijini.

Angumbwike ameiambia mahakama kuwa migogoro inayoendelea kati yake na mume wake, ilianza baada ya maisha yao kuwa magumu kutokana na biashara ya mume wake kuyumba, hivyo mume wake kumtaka warudi kijijini kuanza maisha mapya.

“Maisha niliyoyaishi kipindi hicho kijijini tena nirudi kuyaishi, hapana. Ndio maana nilitafuta mwanaume mjini kuondokana na maisha ya kijijini,” ameeleza.

Ameongeza kuwa “ Huyu mwanaume nampenda sana na migogoro iliyopo kati yetu ni mimi kugoma kurudi kijijini, hivyo nilimruhusu yeye arudi kijijini akajipange na mimi kuniacha mjini, lakini cha ajabu aliporejea alitafuta mke mwingine.”

My Take
Robert Heriel Mtibeli Wanaume endeleeni kuwapenda wake zenu Kwa moyo wa mshumaa ikibidi muwatoe out Kila wiki ila mkifirisika ndio mtajua hamjui 🤣🤣

Pia soma Baada ya kufukuzwa kazi kaka yagu alitembea na mke wangu mpaka kumzalisha
 
Kwani ukiishiwa lazima urudi kijijini?
Ndio maana kule hakuna Kodi nyumba bwerere na mashamba bwerere.

Wewe Kwa kuwa una duka la Jumla halifilisiki bakia huko huko mjini.

Cha kushangaza eti huyo.mwanamke hataki Mumewe aoe wa Kijijini.

Ndio maana Hadi nakufa sitokuja kufanya kitu kinaitwa kufunga ndoa ,never
20250102_161916.jpg
 
Wanaume tukumbuke msaada WA mke wako au mwanamke kwako ni mdogo sana, usijaribu kumuamini hao watu hubadilika kila wakati, hivo jiwekee akiba yako asiyoifahamu, jipende yeye mjali kwa kiasi , maana akipata tatizo ni lakwenu lakini ukipata tatizo ni lakwako
 
Kwani ukiishiwa lazima urudi kijijini?
wee mdada ni aje aisee!! ivi unaikiri mjini mchezo???...kila ki2 ni ela,,,,kukojoa ela,kuoga ela,kulala ela kumwona dr ela,,,,wakati kijijini kukojoa unaingia porini unafanya yako,kuoga unaingia mtoni unafanya yako,kulala unaingia shambai unafanya yako,ukiumwa unamwona mtaalam wa miti shamba mambo yanenda sawa,,,,,,,''''mjini noma!!
 
Wanaume tukumbuke msaada WA mke wako au mwanamke kwako ni mdogo sana, usijaribu kumuamini hao watu hubadilika kila wakati, hivo jiwekee akiba yako asiyoifahamu, jipende yeye mjali kwa kiasi , maana akipata tatizo ni lakwenu lakini ukipata tatizo ni lakwako
Umenena vema sana mkuu. Tatizo hawa watoto wa 2000 wanajifanya much know sana..
 
wee mdada ni aje aisee!! ivi unaikiri mjini mchezo???...kila ki2 ni ela,,,,kukojoa ela,kuoga ela,kulala ela kumwona dr ela,,,,wakati kijijini kukojoa unaingia porini unafanya yako,kuoga unaingia mtoni unafanya yako,kulala unaingia shambai unafanya yako,ukiumwa unamwona mtaalam wa miti shamba mambo yanenda sawa,,,,,,,''''mjini noma!!
Wakati huo yeye hachangii hata shilingi 50 mbovu..
 
Back
Top Bottom