Baada ya Mume kufilisika Mke adai yuko tayari kuvunja Ndoa kuliko kurudi Kijijini

Baada ya Mume kufilisika Mke adai yuko tayari kuvunja Ndoa kuliko kurudi Kijijini

Mdaiwa Tumaini Angumbwike (35) mkazi wa Makunguru ameiambia Mahakama ya Mwanzo mkoani Mbeya kuwa yuko tayari kutalakiana na mume wake kuliko kurudi kijijini.

Angumbwike ameiambia mahakama kuwa migogoro inayoendelea kati yake na mume wake, ilianza baada ya maisha yao kuwa magumu kutokana na biashara ya mume wake kuyumba, hivyo mume wake kumtaka warudi kijijini kuanza maisha mapya.

“Maisha niliyoyaishi kipindi hicho kijijini tena nirudi kuyaishi, hapana. Ndio maana nilitafuta mwanaume mjini kuondokana na maisha ya kijijini,” ameeleza.

Ameongeza kuwa “ Huyu mwanaume nampenda sana na migogoro iliyopo kati yetu ni mimi kugoma kurudi kijijini, hivyo nilimruhusu yeye arudi kijijini akajipange na mimi kuniacha mjini, lakini cha ajabu aliporejea alitafuta mke mwingine.”

My Take
Robert Heriel Mtibeli Wanaume endeleeni kuwapenda wake zenu Kwa moyo wa mshumaa ikibidi muwatoe out Kila wiki ila mkifirisika ndio mtajua hamjui 🤣🤣

Unaoa Maskini unategemea nini kama sio hayo?

Maskini wengi ni wanafiki Sana.
Huyo aliolewa Kisa maisha magumu ya huko kwao kijijini.

Endeleeni kuoa Wanawake Maskini
 
Back
Top Bottom