Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Nimepitia huo ufafanuzi uliotolewa na bodi nikaamini kweli tunachezewa akili.

Kipi cha maana kilichowekwa humo??

Toeni ufafanuzi na siyo siasa.
 
Jina nililokuwa natumia chuo sio hili nalotumia sasa, yaani yote yamebadilika..pia sipo kwenye ajira rasmi...
Bodi ya mikopo haina data nzuri mimi na rafiki angu tulipata asilimia sawa cha kushangaza mwenzangu kaandikiwa deni kubwa kuliko langu.Nimemcheka ila sina namna nimeamua nimuonee huruma.
 
Hiyo retention fee ipo kwenye mkataba?! Kama haipo inaibukia wapi kwenye deni
 
Dawa ya deni ni kulipa na si vinginevyo
Acha kukurupuka bila kujua kinacho zungumzwa!!iukimya wakati mwingine unaficha kiwango chako cha kufikiria(elimu), mtu kimuonekano anaweza akahisi wewe ni prof!!lakini ukaongea kidogo, tu akajua kumbe ni std 3 B, inshu sio kukataa kulipa deni bali ni hicho kinachotozwa kwenye deni!!
 
Bodi ya mikopo haina data nzuri mimi na rafiki angu tulipata asilimia sawa cha kushangaza mwenzangu kaandikiwa deni kubwa kuliko langu.Nimemcheka ila sina namna nimeamua nimuonee huruma.
Hawako makini, kuna ambao wataonewa na ambao watafaidika
 
Hakuna mkopo usio na riba hiyo badala ya kuitwa riba ya mkopo kama mikopo ya biashara wanaita retention money yaani riba ya kutunza thamani ya fedha
Hyo ni too much kwa Raia mnyonge na kukomoana huko
 
Sijaona majibu yeyote ya maana kutoka loan board zaidi ya kumtisha iddy tu na kutuaminisha eti iddy ameelewa na atakuwa balozi....ameelewa nini kwenye yale malalamiko yake? Retention fees ndio kitu gani? kwani ule mkpo ni biashara? Nimrodi Mkono alituanzishia janga la kitaifa.
I wonder mkopo wa elimu unakuwa na riba kubwa kwani elimu ni biashara jamani, mbaya zaidi Lila mwaka inaongezeka Sasa mtu unakuwa unalipa nini?
 
b6f3355c-f3de-4b54-a7b3-c0d25c2da32c.jpg
 
I wonder mkopo wa elimu unakuwa na riba kubwa kwani elimu ni biashara jamani, mbaya zaidi Lila mwaka inaongezeka Sasa mtu unakuwa unalipa nini?

Deni mil 4.5 unaenda bodi kuliclear unaambiwa una deni la 12.5m yaani kila mwaka Deni linaongezeka as if haulipi kitu.
 
Hovyo sana sasa hapo wamefafanua mini?! Mwl ameeleza vzr kuliko hata hao maafisa wa Board
 
Deni mil 4.5 unaenda bodi kuliclear unaambiwa una deni la 12.5m yaani kila mwaka Deni linaongezeka as if haulipi kitu.
Huko bodi Kuna watu wanatajirikia kwa kuonea watu kimakusudi au Kuna ufisadi iweje Deni liwe Lina double badala ya kumpungua na kwanini huu ujinga uanze awamu ya magufuli tu. Watu huchukua mikopo na wakianza kulipa linapungua iweje hii ya bodi ya mikopo liwe Lina double tu
 
Kabisa kipindi hiki cha magufuli deni yaani linaongezeka kila kukicha wakati mtu unalipa kila mwezi 15%...Enzi sie tunasoma kozi price yake ilikuwa laki 4 hadi laki 8 ,boom 2500 , field elf 6 kwa siku,hadi unamaliza kozi yote unatumia milioni 2.8 hadi 3.2 kozi ya miaka mitatu!! Tulifanikiwa kulipa mapema sana na lilikuwa linapungua kadri unavyolipa na hata ukienda bodi kuchukua settlement unaona lilivyokuwa linapungua....Ila awamu ya NGOSHA ihiiiiiii ni balaa deni linaongezeka.
 
Mimi mwenyewe nafikiria kufanya hvo nipe a, b, c za kubadili majina
Ha haaa. Ni kwamba shuleni niliandikishwa jina la kinyumbani ila cheti changu cha kuzaliwa halikuwepo hilo la kinyumbani bali la ubatizo. So nilivyoolewa nikaachana na hilo la kinyumbani nikaanza kutumia lililopo kwenye cheti cha kuzaliwa nikaongeza na jina la mume wangu.
Hivyo ndivyo ilivyotokea so sikufanya makusudi kukwepa kulipa mkopo.
 
Back
Top Bottom