Mwaka 2013 nilipoenda kuangalia deni langu bodi lilikuwa Tsh 12,908,741 (hii inajumuisha hela halali niliyotumia mwenyewe pamoja na ada ilikuwa Tsh 11,394,700, Administration fee Tsh 113,947, retention fee Tsh 1,400,094).
Baada ya miaka 6 kupita huku nikiendelea kulipa deni lilifikia Tsh 14,101,163.82 hii inaonesha kulikuwa na ongezeko la Tsh 1,192,422.82 ambayo kwao walisema ni retention fee.
Mwajiri alipeleka deni la awali la Tsh 12,908,741 na hii ndio walikuwa wanapunguza huko kila nikilipwa salary na naishukuru serikali ilipoongeza 15% ilinisaidia kuwahi kumaliza kulipa deni hili la awali maana nilitakiwa kumaliza 2024 au 2025 kama wangeendelea kukata 8% lakini kwa maamuzi magumu ya serikali ikanifanya nimalize deni hilo 2019.
Hii Tsh 1,192,422.82 ambayo iliongezeka na haikuwekwa kwenye deni la awali bado natafakari namna ya kuilipa maana sijaridhika na hili ongezeko la retention fee kipindi nilichokuwa nalipa.
Na kama ni halali mbona serikali huwa tunaidai hela kwa mda mrefu hata zaidi ya miaka hiyo 6 lakini wao wakija kutulipa hawatulipi na retention fee?
Nawaza nilipe hili deni lililobaki au nisubiri hadi serikali itakaponilipa hela ninayoidai kwanza ndio nimalizie kuwalipa bodi ya mikopo.
Ni mwaka na sehemu umepita bado sijapata jibu kama niwalipe au nisubiri AREAS kwanza.
Note:
Niliwauliza watu wa bodi ya mikopo kama hii retention fee nisipolipa nayo ina retention fee?
Walisema kama ukimaliza kulipa principal loan basi retention fee huwa haiongezeki tena, inabaki hiyo hiyo hata ukidelay kulipa.
Sasa kwa majibu hayo waliyonipa yalinipa kiburi cha kusubiri serikali inilipe kwanza AREAS za kuanzia 2019 ndipo nimalizie kuwalipa. Hadi wa leo sijarudi kuangalia kama retention bado iko hiyo hiyo au nayo wameifanyia retention.
Ila niwatie moyo tu kuwa deni la bodi linalipika na linaisha as long as unalipa hata kama ni kidogo kidogo.
HABA NA HABA HUJAZA KIBABA