Baada ya Mwl. Mussa Iddy kulalamika, HESLB yatoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa urejeshaji mikopo

Retention fee ni pale serikali inapodai ila serikali inapodaiwa Kama malimbikizo ya haya maalimu areas hakuna retention fee.

MIALIMU bana.
Retention fee inaumiza.

na hasa kwa mfanyakazi ambaye hasumbui kulipa, Loan Board wana masharti magumu kuliko commercial banks
 
Wanamuhujumu rais ili aonekane mbaya kwa wananchi
 
Mwaka 2013 nilipoenda kuangalia deni langu bodi lilikuwa Tsh 12,908,741 (hii inajumuisha hela halali niliyotumia mwenyewe pamoja na ada ilikuwa Tsh 11,394,700, Administration fee Tsh 113,947, retention fee Tsh 1,192,422)..
Mkuu vp kwenye salary slip ukimaliza ule mkopo wa kawaida retention haionekani au manake hata mimi nna mpango deni likiisha kwenye salary slip nikae zangu kimya labda rais ajaye atakuja kutuokoa na huu wizi.
 
Kiukweli ni kukiuka mkataba, mtu unasaini mkataba makato 8% mwisho wa siku unalipa 15%, Kwa wale wa TGS D wanalamba 105,000 nzima nzima. Sio haki kwakweli.
Hiii sheria ya 15% ilibd iwahusu hawa ambao wamesaini mkataba wa hivi ila wale wa 8% wangeendelea na mktaba wao ilaa kuvunja makubaliano ni kuto kutiii mkataba wa kukopeshana HESLB liangalieni hili pia .
 
wale wa kusifu na kuabudu (UVCCM na mataga) huwezi waona kwenye huu uzi
 
Serikali inafanya biashara gani mpaka itukopeshe hela sisi wenye hela wenyewe?.
Kwani wenye hela tumekataa kwa vitendo kukopeshwa? Mnakubaliana na serikali ndo maana mnakopa na kulipa.
 
Katika mambo ambayo yamem-discredit Magufuli na ameonekana ni roho mbaya ni hili la bodi ya mikopo na masuala yote ya watumishi ya hali na stahiki zao.
 
Retention fee ni pale serikali inapodai ila serikali inapodaiwa Kama malimbikizo ya haya maalimu areas hakuna retention fee.

MIALIMU bana.
Ukitukana walimu,unakua mjinga zaidi.Acheni kutetea uozo huu kisa nyinyi mnanufaika nao.
 
Kwa inavyofanya serikali ya CCM,utashangaa 2025 inapita kwa asilimia 95.

Mi naona hiyo retention fee ni ndogo, wangeongeza mbinyo.
 
Mtasema mengi na nyaraka nyingi mno na vifungu VIngI Ila kweli Bodi hii ni tatizo, watumishi wengi wanalia.
 
Alafu kwenye zile form za mkataba hizo habari za rentation zilikuwepo?
Hazikuwepo chief, yaani mimi huo mkataba nilikuwa nao sema nowdays sijui hata ukowapi na masharti yake yako tofauti kabisa na vile hawa bodi wanavyo nyonga rai wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…