Iko hivi mkuu, ni mke wa jamaa yangu yy si mtu wa mitandao.nilishawahi kulileta humu. Aliondoka na kubeba vyombo vya ndani vyote na kuvunja simu ya jamaa, haikutosha akakimbilia polisi ndio kumuelekeza ustawi.
Jamaa aliitwa ustawi akasema yy pamoja na yote bado anataka walee mtoto pamoja. Mwanamke akakataa kuwa anataka aishi maisha yake. Akahitaji alipwe kiasi cha fedha kila mwisho wa mwezi maana jamaa yupo serikalini. Jamaa akadai yupo tayari kumtunza mtoto lakini si kwa kupangiwa kama ambavyo Mwanamke anadai
Ustawi kuona msimamo wa wanamke wakaamua warudishe kwanza maamzi kwa wazazi. Wazazi wamegoma kutoa uamzi wamemwambia binti yao arudi ustawi. Ndio jamaa kapokea witonwa kurudi tena ustawi