Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Dah mwanangu nusu nitoe chozi ....afu nipo na manzi na nlimwambia natokea bara sasa ningetoa chozi nahisi angejua uhalisia wangu kuwa mwanaume wa Dar...

Ila mkuu tuambie sasa zile damu ni nini?[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Zile damu ni yule mama ndio inaonekana alikuwa anasababisha ,alikuwa anatumia nguvu za kichawi ku kidnap vichanga soo zile damu zilikuwa za vile vichanga

Ndio maana pale hakukuwa na mpangaji mwingine lakini alimdanganya agustino kuwa mpango wake ni kupangisha wanafunzi tu.

Kumbe raia walikuwa washa mshitukua

Lakini sina majibu ya moja kwa moja maana nguvu za giza zinamambo mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamatatizo gani hiyo nyumba mkuu? Elezea kidogo kama hautojali.
Ni kweli hata mtaani kwetu nyumba ya namna hiyo ipo, mwenyewe aliitelekeza akaweka mlinzi ili awe anaifanyia usafi lakini mlinzi hakumaliza hata mwezi akaondoka. Nyumba yenyewe ya kisasa ila imekua kama gofu vichaka vimeota hadi ndani, madirisha yalikua ya vioo ila vimeshapasuka, geti lake lipo wazi muda wote, yani limekua lijumba flani la kutisha.
Usiku taa zinawaka vizuri kwasababu umeme bado upo nadhani tanesco wanaogopa kwenda kuukata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zile damu ni yule mama ndio inaonekana alikuwa anasababisha ,alikuwa anatumia nguvu za kichawi ku kidnap vichanga soo zile damu zilikuwa za vile vichanga

Ndio maana pale hakukuwa na mpangaji mwingine lakini alimdanganya agustino kuwa mpango wake ni kupangisha wanafunzi tu.

Kumbe raia walikuwa washa mshitukua

Lakini sina majibu ya moja kwa moja maana nguvu za giza zinamambo mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah sure nimekumbuka mpska raia wakachoma moto....

Ila mwanangu Joooh mwamba agustino nimemkubali kichizi.Ningekuwa nna mamlaka jamaa ningemwachia huru alipambana kuzifikia ndoto zake ila daah naona mapoti wakampenda zaidi.

Ila ni wakati wako wa kuonesha thamani unayompa mastermind Agustino maana hakukutaja wala kumtaja yeyote yule aliamua ateketee kama mshumaa.Bless sana kwa huyu Jamaa
 
Daa pole sana wacha tuvumilie tu.

Ila hii story ikiisha itabidi tutengeneze kikundi tukisajiri tukachukue mkopo halmashauri maana kwa huu ushirikiano tutafanikiwa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ila joooh asiwe mwenyekiti wa kikundi asije akatupandia maharage bure members wote,afu hela akanunulia kuku na spoku,maharage yakikuwa atujie na kwanja badala ya kakisu si mnajua akishajilipuwa anakuwaga sio yeye[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nakuja ngoja nikavute tena[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
Hivi hakuna imoji ya kucheki inayogara gara chini
Mana nimecheka mpaka mbavu zinauma
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Hata humu kwa mtazamo wangu bado inakidhi vigezo vya kubaki kwani bado inaelezea mapito wanayopitia watu kwenye utafutaji

Kwa vile moderators wameamua kuiunganisha kule juu ni vizuri sasa ukaweka mbinu mpya za halali unazotumia kwa sasa kupambana na swala zima la utafutaji baada ya mbinu zenu kugonga mwamba

Hii itaipa nguvu kubwa story yako na itabaki kuwa funzo kwa wengine wanaodhani kwa waganga kuna kupata utajiri kirahisi au wanaouza bangi na madawa mengine ya kulevya wanapata utajiri kirahisi

Ulichokieleza kinafunzo kubwa kwa watafutaji kwani katika utafutaji watu tunapitia mahangaiko mengi sana ikiwemo kuwaza hayo ya waganga

Pamoja na yote kama utakuwa umechagua kuandika hicho kipengere chako cha mwisho kinachoelezea unayo yafanya kwa sasa kwenye post hii, jitahidi kuiweka kwa kulenga pointi za msingi unazotaka watu wajifunze

Mwisho kabisa kwani tangu uzi unaanza sikuchangia popote ila nimeufuatilia vizuri tu ili kujua hatima ya Augustino, nikushauri tu kwa vile umekiri ni story ya kweli iliyokutokea mwenyewe tafuta namna ya kwenda kumuona jamaa yako huko gerezani

Ni kweli kabisa wafungwa huwa wanahamishwa hamishwa ila ukiamua utampata tu! Nenda kampe hi atajisikia faraja

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wazo lako ni zuri sana

Ila kwa haya nilio yazungumza hapa kama kuna baharia

Atajipeleka kwa mganga kusaka pesa yaani omba ukakutana na mganga uchwara maana atakuibia pesa lakini sio nafsi

Lakini usikutane na wale wanaoiweza kazi kama unaroho ya panzi cha moto utakipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.

Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi

Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .


Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana

Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho

Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki

Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.

Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya

Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza


Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho

Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype

Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA

Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza

Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan

Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa

Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.

Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu

Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah kwa nini umekata vitunguu karibu na macho yangu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24],,ndugu pambana ww jasiri na bado mdogo sana naamini agustino amekuacha na nguvu kubwa ya mapambano komaa na usije msahau mshikaji wako kabisa

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
 
Dah kwa nini umekata vitunguu karibu na macho yangu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24],,ndugu pambana ww jasiri na bado mdogo sana naamini agustino amekuacha na nguvu kubwa ya mapambano komaa na usije msahau mshikaji wako kabisa

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Ndio hivyo hakuna namna nikukomaa tu.

Bila kuwa na hofu ya moyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah sure nimekumbuka mpska raia wakachoma moto....

Ila mwanangu Joooh mwamba agustino nimemkubali kichizi.Ningekuwa nna mamlaka jamaa ningemwachia huru alipambana kuzifikia ndoto zake ila daah naona mapoti wakampenda zaidi.

Ila ni wakati wako wa kuonesha thamani unayompa mastermind Agustino maana hakukutaja wala kumtaja yeyote yule aliamua ateketee kama mshumaa.Bless sana kwa huyu Jamaa
[emoji23][emoji23] wakati nakujibu nikihisi kunakipande utakua umeruka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa yote... Agusto kawagusa wengi sana... Mungu amsadie atoke mzima na akukute na moyo huu huu. Unapitia magumu.... Kwa ufupi tungependa angalau useme kama A level Ulifanikiwa kumaliza baada ya agusto kufungwa na unacho fanya kwa sasa ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nilipambana sana semaa kilicho niokoa kwenye yale masomo 3 nilikuwa naelewa sana sana economics na geography toka Olevo maana nilisoma masomo ya biashara

Advanced maths ilinipeleka ila nilipambana nayo vibaya sana

Degree yangu ya kwanza nimemaliza mwaka jana Udsm conas Actuarial science

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom