Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Oky wakuu hii ndio itakuwa episode ya mwisho nawashukuru wote waliokuwa baga kwa bega toka uzi unaanza mpaka sasa tumemaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulivyoimalizia story naimani umetusikitisha wengi sana, pia tunashukuru kwa madini uliyotuletea maana tumejifunza mengi sana

Mungu akubariki utimize ndoto zako rafiki wa kweli 🙏
 

Attachments

Oky wakuu hii ndio itakuwa episode ya mwisho nawashukuru wote waliokuwa baga kwa bega toka uzi unaanza mpaka sasa tumemaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Why am I tearing up reading that. Jooohs, you have a lot of emotional maturity. As they say, maturity comes with experience not age.

Wewe ni rafiki wa kweli unajua maana ya urafiki wa kweli. Najua hata rafiki yako huko alipo anajua wewe ni rafiki wa kweli.

I sincerely hope you'd be able to keep that fire and enthusiasm.

Thank you for sharing that. Xoxo.
 
Stori Kali ila inakatisha tamaa kwa sisi wazee wa kujilipua...kuna mambo nimeyaishi katika hii stori na bado nakomaa mpaka nitoboe ...

Bug up ziende kwa AG kwa uthubutu usiopimika hata kwa kipima joto ..jooohs na wewe uko vizuri tunaweza kushirikiana kupambana kama bado unaendelea kutumia njia mbadala...
komaaa tu mkuuu kuuza bangi utatoboa wala usiwaze kudakwa
 
Dah! Hii story n tamu
Inafurahisha na inasikitisha, Agu ni rafiki yako wa kweli fanya uwezavyo angalau uwakumbuke wazazi wake

Pili kama alivyokusihi kwamba ENDELEA KUPAMBANA, hii kauli ifanyie kazi ili hata akitoka jela uweze kumpiga tafu.

Big up sana Jooohs, wewe ni mpambamaji haswa
 
Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.

Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi

Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .


Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana

Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho

Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki

Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.

Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya

Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza


Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho

Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype

Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA

Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza

Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan

Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa

Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.

Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu

Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu jooohs jitahidi upambane kiasi kwamba agustino akija kutoka gerezani umpe mtaji japo wa 3m ajiendeleze atimize malengo yake.

Pili jitahidi uwe unaenda kumuona japo kila mwaka na umwambie kabisa kuwa unaendelea KUKOMAA Kama alivyokuasa kuwa MWANANGU ENDELEA KUKOMAA na kwamba siku akitoka una zawadi yake ( mtaji ) , hii itampa nguvu Sana jamaa huko gerezani

WANA JAMII FORUMS, TUSIFANYE MAKOSA TENA OCT 2020
 
Usiku nikaanza kuwaza eti mtoto wangu, kaenda kwa mganga, kapanda maharage, kaenda kuyachuma kakuta Ni mimi, akajisemea nimuue mama au niachane na utajiri? Basi nikashtuka nikaanza kuomba na kukemea hiyo roho ya kishirikina kwa wanangu
Mungu niepushe mimi maisha matamu hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Butimba ni gereza la wafungwa mwenye matukio makubwa makubwa,kuna father yangu mdogo kafungwa hapo ,yeye kapiga matukio makubwa,kuua,kupora na kuvunja maduka, kula bangi daaa matukio hatar,ila nashangaa huwa anatoka na kurudi tena,

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio hivyo mkuu nasikia wanalima 24 hours

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stori Kali ila inakatisha tamaa kwa sisi wazee wa kujilipua...kuna mambo nimeyaishi katika hii stori na bado nakomaa mpaka nitoboe ...

Bug up ziende kwa AG kwa uthubutu usiopimika hata kwa kipima joto ..jooohs na wewe uko vizuri tunaweza kushirikiana kupambana kama bado unaendelea kutumia njia mbadala...
Mkuu kama una malengo ya kufika mbali thamini sana muda nilicho jifunza magereza ni sehemu inayopoteza sana ndoto za watu.

Mimi kiukweli ni risk taker mkubwa lakini kwenye mambo ya msingi

Sitaki nguvu zangu zikaishie magereza nimekuwa mpole siwezi piga hata kifaranga cha kuku wa mtu

Nikiona polisi wanapita kulia mimi nageuza kushoto



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom