Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using
Jamii Forums mobile app