Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Aseeh. Hii story nimeifuatilia kimya kimya mwanzo mwisho. Inafundisha sana.

Jooohs, wee na Agustino mna historia. Mtu akiangalia kwa haraka anaeza conclude kwamba jamaa alikutumbukiza kubaya. Ila kwa mimi naeza kusema jamaa alikufungua akili kwa kiasi kikubwa, na ukajua maisha ni nini mapema sana.

Kiukweli watu wakishibana kwenye urafiki huwa inakua ni zaidi ya ndugu. Ndio maana Agustino alitaka ufanikiwe maishani kama yeye alivyokua na ndoto hizo. Alitaka uote anachoota yeye na ndio maana kauli yake kwako alitaka uendelee kukomaa.

Kinachofurahisha ni kwamba unajua kustruggle kufanikisha isue yyte. Struggle zile zile zipeleke kwenye maisha ( na ndicho unachokifanya) hakikisha hurudi nyuma wakati unataka ufikia lengo (mf. Uliporudi kutafta mbegu kwa mara ya kwanza ulizikosa hukukata tamaa ukatimua mbio fasta akachukua tochi geto ukaziona)

Ukilenga kufanya jambo la kukufanikisha usiogope viunzi (Kama vile vya mama mwenye nyumba kukukodolea macho ukashindwa kutoa mwili ila baadae ukaamua kuruka hicho kiunzi)

Mwisho wa yote, timiza ndoto zako afu usimsahau Agustino man. Ni mpambanaji man. Mkifanya kombination mtatoboa kikubwa man.

Big up kwa kutupa funzo kubwa man. Mungu afanikishe kila ulichoplan bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kijana mpambanaji piga mwendo kazi bado hujaimaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"MWANANGU ENDELEA KUKOMAA"
😢😢😢😢 hii ni painful mpaka nimenywea.
Augustino ni "mtu wa chuma", wengi jela huwa wanaanza kutoa story za kujililia kama vile"nateseka,ndugu yangu usifanye vile utakuwa kama mimi n.k"
Lakini Augustino anakwambia endelea kukomaa mwanangu.
Huyu Augustino inawezekana utotoni mwake alinyanyasika na dhiki, na ni kitu hataki nasaba nacho kabisa, nacho akaamua kufata ule msemo wa "The End Will Justify The Means"
 
Shukrani sana mkuu kwa mawazo mazuri ya kutia moyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu siwezi kabisa na sidhani kama itatoea

Maana kiukweli mama yangu ananipenda sana

Hata nilikuwa nikifanya kosa kubwa lazima atalifunika tu ili ionekane sijafanya chochote ngoja Nikuwejee mkasa wa historia yangu na mama yangu ulipo anzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini hamkukata rufaa ya hio kesi
Kutokana na ile kesi nilivyokuwa jamaa alikuwa amezidiwa kwa kweli kutokana na ushahidi upande wa serikali waliokuwa nao

Hata wangeenda mbele bado wasingeweza kutoboa pia ukikata rufaa ukashindwa wangeongeza miaka ingefika hata 60

Achilia mbali wazazi wake wote walikuwa hawajasoma hata maswala ya rufaa sidhani kama wangewezana nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaah mlipambana sana wewe na agu


Nasema hivi hii story ni tiba ya corona
Anaebisha alete fact hapa
 
Butimba ni gereza la wafungwa mwenye matukio makubwa makubwa,kuna father yangu mdogo kafungwa hapo ,yeye kapiga matukio makubwa,kuua,kupora na kuvunja maduka, kula bangi daaa matukio hatar,ila nashangaa huwa anatoka na kurudi tena,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stori Kali ila inakatisha tamaa kwa sisi wazee wa kujilipua...kuna mambo nimeyaishi katika hii stori na bado nakomaa mpaka nitoboe ...

Bug up ziende kwa AG kwa uthubutu usiopimika hata kwa kipima joto ..jooohs na wewe uko vizuri tunaweza kushirikiana kupambana kama bado unaendelea kutumia njia mbadala...
 
Oky wakuu hii ndio itakuwa episode ya mwisho nawashukuru wote waliokuwa baga kwa bega toka uzi unaanza mpaka sasa tumemaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maisha uliyopitia ni darasa tosha la maisha, pia Augustino ni wa muhimu sana katika maisha yako usimsahau kabisa ni rafiki wa kweli huyu uwe unamtembelea mara moja moja
 
Augustino ni mtu mmoja ana moyo wake.
I like the dude.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…