Oooky Inaendelea..................
Wakati naendelea kujiuliza huyu agustino atakuwa kaenda wapi wazo likaniijia nimpigie tena yule ndugu yake labda atakuwa kapata baadhi ya information nikampigia tena akaniambia bro siumetoka kunipigia sasa muda si mrefu nimekwambia sina taarifa yake akinitafuta tu nitakupigia basi nikatoka pale getto nikaanza safari kuelekea centre pengine nikae pale naweza kumuona labda anapita na madumu nikampokee
Muda ulikuwa unayoyoma jua linaelekea kuzama nikaanza mwendo ukumbuke hapo alipokuwa anakaa ilikuwa kunaka umbali hadi kufika centre ikabidi nitembee haraka haraka hadi kufika pale nikakuta maboda boda kibao wamekaa wanapiga story, wengine wanakunywa uji kulikuwa kunamama anapika pale centre.
Mimi muda huo nimechanganyikiwa kila muda napiga simu ya agustino lakini haipatikani nikajipa moyo labda simu yake itakuwa imezima maana alikuwa anakatecno kadogo sana lakini touch screen. Basi nikaendelea kuzuga pale huku nikiendelea kusikiliza sauti za wale boda boda wa kibishana kuhusu simba na yanga, wengine wakiongea lugha za kienyeji
Wakati na zidi kutafakari huku nikikodolea macho kila piki piki inayopita pale nikawa na matumaini labda itakuwa ni agustino lakini nilikuwa naambulia patupu daa nikiangalia muda unazidi kwenda nikipiga simu haipokelewi mara muda kidogo naona message kutoka voda kifurushi chako kimeisha.
Ikabidi nisimame nitazame kibanda ambacho kiko karibu nikaona kimoja kiko upande mwingine nikavuka upande wa pili wa bara bara nikaenda kibandani nikatoa noti ya elfu moja nikapewa vocha ya mia tano nukarudishiwa mia tano
huku nikiendelea kukodolea macho kila usafiri unaopita pale
Ikabidi nivuke tena bara bara niende kukaa ile sehemu niliokuwa nimekaa kufika nataka kukwangua vocha mkononi siioni kusachi mfukoni na ile jero peke yake nikaanza kurudi kukagua pale chini labda nitakuwa nimedondosha wapi nikafatilia barabara yote hadi pale kibandani sikuona kitu.
Nikatoa tena ile 500 nikanunua vocha nyingine kuweka nampigia jamaa bado simu haipatikani daa nikaendelea kukaa pale hadi giza kabisa likaingia nikawaza huyu jamaa atakuwa yuko wapi nilikaa pale hadi wauza mboga kina mama kila mmoja akaanza kubeba sinia anaondoka zake
Daa nikapiga mawazo au kati ya zile taxi zilizokuwa zinapita hapa moja kati yake atakuwa alikuwa ni agustino ngoja nirudi getto kwake kufika pale nikakuta baadhi ya wapangaji pale kuwauliza wanasema bado jamaa hajarudi labda atakuwa yuko shuleni.
Asee niliondoka huku nimechoka hata nguvu za kutembea nilikuwa sina nilitembea hadi nikafika pale hostel nikamwambia muddy kuwa nimeenda kwa agustino lakini sijamkuta lakini jamaa alichukulia kawaida ikabidi kwenda jikoni kwa mpishi nikapiga nae msosi maana wanafunzi walikuwa wameshamaliza kula wengine wameenda prepo ikabidi niingie hostel nianze kuuchapa usingizi
Sijui wenzangu walikuwa wananionaje, nadhani walikuwa wananiona kama mtu aliyekata tamaa na masomo halafu siko serious maana prepo nilikuwa sionekani, soma yangu ya kusua sua kila siku nasingizia naumwa kichwa kumbe hali yangu naijua mwenyewe kunasiku nilikuwa natoka darasani naenda hostel nikapita nyuma ya darasa la wanaosoma arts nikasikia wanacheka vibaya sana huku head boy anasema wale majamaa hawako serious
Kama yule anae doji prepo anasingizia kuumwa kichwa halafu jioni unamuona anaenda kuvuta bangi asee nikapita tu walivyoniona dirishani wakazuga kunyamaza kumbe baharia nimesikia kila kitu.
Wakati nimejilaza pale kitandani huku nikiendelea kupiga ile namba ya agustino bila mafanikio nikawaza sana nitafanya vipi nimpate huyu jamaa maana nilikuwa na hofu sana, niliendelea kupiga ile simu bila mafanikio kesho yake asubuhi ilikuwa ni siku ya shule nikawahi kuamka mapema sana nikajiandaa vizuri nikavaa sare za shule nikamwabia muddy ngoja niwahi kwa agustino maana ndio nilikuwa namuona kama rafiki nilie kuwa nimebaki nae wengine wote wananiona kilaza
Basi nikaanza kutembea fasta hadi nikaiacha kwa mbali mipaka ya shule nikaanza mdogo mdogo kumezwa na vichaka vilivyokuwa vimetapakaa kila sehemu ya ule mtaa basi nilitembea haraka Hadi nikafika kwenye ile nyumba kuangalia mlango umefungwa ikabidi nigonge mlango wa yule mpangaji pale nikamuuliza agustino hajarudi asee
Majibu aliyonipa yalikuwa ni yakusikitisha sana na kuniogopesha maana yule mpangaji akasema alirudi hapa usiku sana na maaskri wakafungua mlango wakapekuwa ila hawakujua walichukua nini kisha wakaondoka nae yaani nilitaka kupooza palepale ilibidi nikae chini ya udongo nikajua mambo ndio yamesha haribika kabisa.
Basi ilibidi niondoke pale nikiwa na maswali mengi , nijajiuliza nirudi shuleni au nikachukue mizigo yangu niwaambie nimezidiwa naenda kulazwa hospital, nkajiuliza tena hivi shule na maisha yangu kipi bora wakati naendelea kujiuluza nikakumbuka yule ndugu yake alietuma mzigo ikabidi nimvutie kamba alipokea nikamwambia jamaa agustino kakamatwa na maaskari jamaa kashituka sana kaniuliza mara mbili mbili nikamwambia ndio walikujanae hadi kupekuwa alipopanga jamaa akakata simu.
Kisha nikatembea fasta kurudi shuleni nikaenda kuingia hadi hosteli nikakuta jamaa ndio wanajiandaa wanavaa nguo waende kwenye ratiba za shule mimi nilipofika nikaanza kuvua yale mavazi yangu kisha nikabadili nguo nyingine za kawaida nikasepa
Nilisema ngoja kwanza niende hadi kule kwa babu labda atakuwa kupigwa kaambiwa ataje wafuasi wake nikanza mchaka mchaka haraka zangu nimefika pale mtoni navuka haraka haraka nikateleza kiatu chote kikazama ndani ya matope ikabidi nivue nikaanza kutoa yale matope kisha nikavaa hivyo hivyo kibichi nikaendelea na safari........
Sent using
Jamii Forums mobile app