Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

joooh, nimesoma comments karibu zote, wadau wamemaliza. Sitaki nirudie Ila kwangu kunafunzo tofauti kidogo na wenzangu.

Jamii inamtazama Augusto Kama mtoto au kijana aliyepotoka sana, na pengine Kuna watu walisema akome, ameacha Shule anashughulika na bangi.

Binafsi, kwa kusoma hii habari, nimepata funzo kwamba Augusto hakukengeuka alikuwa kijana mwenye maono, akaanza kuyatekeleza, akateleza,

Eagerness and greed ya mafanikio, imemuweka pale, na Hana moyo wa kukata tamaa,

Kama kila mwanajamii angemtazama Augusto kwa maono yake asingeweza kusema amekengeuka.

Mungu akupe afya na nguvu huko gerezani, Ono lako liko hi na utakuwa tajiri, ukitoka.

Rafiki mpambanie nduguyo, ijali familia yake, mtembelee Mara kwa Mara as much as practicable. HILI NI JEMBE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
It's true "...urafiki bora haupimwi kwa MUDA, bali upimwa kwa MATENDO..."

Ni story iliyojaa visa vya kusisimua na mafundisho.

Asante sana chief Joh kwa hili na pia pole kwa yaliokukuta, maana mimi nisiyeweza hata kupata taswira ya bwana Agu nina jisikia hivi, infact I can't imagine kwa upande wako ikoje.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Augustino bado anaishi,,akitoka atatusua tu.


It is not over until you are dead!!!!


Kikubwa uhai tu
 
Oooky Inaendelea..................



Wakati naendelea kujiuliza huyu agustino atakuwa kaenda wapi wazo likaniijia nimpigie tena yule ndugu yake labda atakuwa kapata baadhi ya information nikampigia tena akaniambia bro siumetoka kunipigia sasa muda si mrefu nimekwambia sina taarifa yake akinitafuta tu nitakupigia basi nikatoka pale getto nikaanza safari kuelekea centre pengine nikae pale naweza kumuona labda anapita na madumu nikampokee

Muda ulikuwa unayoyoma jua linaelekea kuzama nikaanza mwendo ukumbuke hapo alipokuwa anakaa ilikuwa kunaka umbali hadi kufika centre ikabidi nitembee haraka haraka hadi kufika pale nikakuta maboda boda kibao wamekaa wanapiga story, wengine wanakunywa uji kulikuwa kunamama anapika pale centre.

Mimi muda huo nimechanganyikiwa kila muda napiga simu ya agustino lakini haipatikani nikajipa moyo labda simu yake itakuwa imezima maana alikuwa anakatecno kadogo sana lakini touch screen. Basi nikaendelea kuzuga pale huku nikiendelea kusikiliza sauti za wale boda boda wa kibishana kuhusu simba na yanga, wengine wakiongea lugha za kienyeji

Wakati na zidi kutafakari huku nikikodolea macho kila piki piki inayopita pale nikawa na matumaini labda itakuwa ni agustino lakini nilikuwa naambulia patupu daa nikiangalia muda unazidi kwenda nikipiga simu haipokelewi mara muda kidogo naona message kutoka voda kifurushi chako kimeisha.

Ikabidi nisimame nitazame kibanda ambacho kiko karibu nikaona kimoja kiko upande mwingine nikavuka upande wa pili wa bara bara nikaenda kibandani nikatoa noti ya elfu moja nikapewa vocha ya mia tano nukarudishiwa mia tano
huku nikiendelea kukodolea macho kila usafiri unaopita pale

Ikabidi nivuke tena bara bara niende kukaa ile sehemu niliokuwa nimekaa kufika nataka kukwangua vocha mkononi siioni kusachi mfukoni na ile jero peke yake nikaanza kurudi kukagua pale chini labda nitakuwa nimedondosha wapi nikafatilia barabara yote hadi pale kibandani sikuona kitu.

Nikatoa tena ile 500 nikanunua vocha nyingine kuweka nampigia jamaa bado simu haipatikani daa nikaendelea kukaa pale hadi giza kabisa likaingia nikawaza huyu jamaa atakuwa yuko wapi nilikaa pale hadi wauza mboga kina mama kila mmoja akaanza kubeba sinia anaondoka zake

Daa nikapiga mawazo au kati ya zile taxi zilizokuwa zinapita hapa moja kati yake atakuwa alikuwa ni agustino ngoja nirudi getto kwake kufika pale nikakuta baadhi ya wapangaji pale kuwauliza wanasema bado jamaa hajarudi labda atakuwa yuko shuleni.

Asee niliondoka huku nimechoka hata nguvu za kutembea nilikuwa sina nilitembea hadi nikafika pale hostel nikamwambia muddy kuwa nimeenda kwa agustino lakini sijamkuta lakini jamaa alichukulia kawaida ikabidi kwenda jikoni kwa mpishi nikapiga nae msosi maana wanafunzi walikuwa wameshamaliza kula wengine wameenda prepo ikabidi niingie hostel nianze kuuchapa usingizi

Sijui wenzangu walikuwa wananionaje, nadhani walikuwa wananiona kama mtu aliyekata tamaa na masomo halafu siko serious maana prepo nilikuwa sionekani, soma yangu ya kusua sua kila siku nasingizia naumwa kichwa kumbe hali yangu naijua mwenyewe kunasiku nilikuwa natoka darasani naenda hostel nikapita nyuma ya darasa la wanaosoma arts nikasikia wanacheka vibaya sana huku head boy anasema wale majamaa hawako serious

Kama yule anae doji prepo anasingizia kuumwa kichwa halafu jioni unamuona anaenda kuvuta bangi asee nikapita tu walivyoniona dirishani wakazuga kunyamaza kumbe baharia nimesikia kila kitu.

Wakati nimejilaza pale kitandani huku nikiendelea kupiga ile namba ya agustino bila mafanikio nikawaza sana nitafanya vipi nimpate huyu jamaa maana nilikuwa na hofu sana, niliendelea kupiga ile simu bila mafanikio kesho yake asubuhi ilikuwa ni siku ya shule nikawahi kuamka mapema sana nikajiandaa vizuri nikavaa sare za shule nikamwabia muddy ngoja niwahi kwa agustino maana ndio nilikuwa namuona kama rafiki nilie kuwa nimebaki nae wengine wote wananiona kilaza

Basi nikaanza kutembea fasta hadi nikaiacha kwa mbali mipaka ya shule nikaanza mdogo mdogo kumezwa na vichaka vilivyokuwa vimetapakaa kila sehemu ya ule mtaa basi nilitembea haraka Hadi nikafika kwenye ile nyumba kuangalia mlango umefungwa ikabidi nigonge mlango wa yule mpangaji pale nikamuuliza agustino hajarudi asee

Majibu aliyonipa yalikuwa ni yakusikitisha sana na kuniogopesha maana yule mpangaji akasema alirudi hapa usiku sana na maaskri wakafungua mlango wakapekuwa ila hawakujua walichukua nini kisha wakaondoka nae yaani nilitaka kupooza palepale ilibidi nikae chini ya udongo nikajua mambo ndio yamesha haribika kabisa.

Basi ilibidi niondoke pale nikiwa na maswali mengi , nijajiuliza nirudi shuleni au nikachukue mizigo yangu niwaambie nimezidiwa naenda kulazwa hospital, nkajiuliza tena hivi shule na maisha yangu kipi bora wakati naendelea kujiuluza nikakumbuka yule ndugu yake alietuma mzigo ikabidi nimvutie kamba alipokea nikamwambia jamaa agustino kakamatwa na maaskari jamaa kashituka sana kaniuliza mara mbili mbili nikamwambia ndio walikujanae hadi kupekuwa alipopanga jamaa akakata simu.

Kisha nikatembea fasta kurudi shuleni nikaenda kuingia hadi hosteli nikakuta jamaa ndio wanajiandaa wanavaa nguo waende kwenye ratiba za shule mimi nilipofika nikaanza kuvua yale mavazi yangu kisha nikabadili nguo nyingine za kawaida nikasepa

Nilisema ngoja kwanza niende hadi kule kwa babu labda atakuwa kupigwa kaambiwa ataje wafuasi wake nikanza mchaka mchaka haraka zangu nimefika pale mtoni navuka haraka haraka nikateleza kiatu chote kikazama ndani ya matope ikabidi nivue nikaanza kutoa yale matope kisha nikavaa hivyo hivyo kibichi nikaendelea na safari........

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee story tamu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku nikaanza kuwaza eti mtoto wangu, kaenda kwa mganga, kapanda maharage, kaenda kuyachuma kakuta Ni mimi, akajisemea nimuue mama au niachane na utajiri? Basi nikashtuka nikaanza kuomba na kukemea hiyo roho ya kishirikina kwa wanangu
Mungu niepushe mimi maisha matamu hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo kesi anatoka ata Kama kafungwa.....anakata rufaaa..alimradi uwe na mzego kiaina...ila Ni kesi rahisi Sana kwa mda aliokaa....na kwakua Ni kesi alishtakiwa na jamhuri Ni rahisi zaidi kutoka. Hapa wahudhuriaji wa mahakamani hope mtanielewa...tafta mtu ambae anacheza karibu na magereza na Mahakama akupe staili....maana siez weka inafanyikaje iyo makitu
 
Mkuu tukio kama hili limewahi kumtokea ndugu yangu kabisa wa baba yangu mkubwa akiwa na rafiki yake, walianzia kwa mganga ili kupata utajiri wakafuata masharti yote kabisa na sharti la mwisho wakapewa kamba za katani na kuambiwa waende nje kidogo ya kijiji (ni jirani na mbuga ya serengeti) watawakuta ngo'mbe wawafunge na zile kamba na kuwaleta kwa mganga baada ya hapo pesa itakuw ni ya kumwaga. Walipofika pale walichokiona kwanza ni vumbi linatimka na muda si mrefu Nyati wawili walioshiba wako vichwa chini spidi 240 km/h. Ndugu yangu anasema mbio alizotimka siku hiyo si za dunia hii. Hii si hadithi na mimi si muumini wa mambo hayo lakini tulikuwa tunajua katumwa kwenda kuleta ng'ombe na mganga na miaka ile mgodi wa Nyamongo (sasa North Mara) ulikuwa chini ya wenyeji na mambo ya ushirikina yalikuwa mengi sana.
Dah mkuu nimecheka hatar nataman Kama ungeelezea kwa kirefu zaid
 
Jaman NAOMBENI msaada Kuna Uzi nautafuta Ila nimejisahau jina lake

Kuna jamaa alikua na rafiki yake ambaye alikua mwizi mwizi na pia walikua wanafunga sungura

Wakienda kukata majani kila nyumba wanayoipita yule rafiki yake anasema pale no kwandug yangu halafu anaenda kuiba bila jamaa kujua

Kifo Cha huyo jamaa kilitokana na kuumwa na mbwa alipoenda kuiba kwenye nyumba ya mzungu


Pliz anaekumbuka huo Uzi naomba anitag
 
Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.

Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi

Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .


Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana

Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho

Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki

Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.

Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya

Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza


Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho

Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype

Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA

Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza

Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan

Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa

Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.

Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu

Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee!
 
Back
Top Bottom