Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,926
- 6,422
Hakuna shortcut ukienda kwa mganga ukuongezea matatizo na kukufanya mteja ili kuku zisikatike kwakeNimechoka kutype imebidi nipige bla bla tumalize maana kunawatu walikuwa wanatamani wanipige ngumi kisa muendelezo
Sent using Jamii Forums mobile app
Augustino siyo muoga ku riskKuna vijana wachache Sana huwa wanaogopa kurisk maisha yao ili kupata wanachokitaka Agostino ni mmoja Kati ya wachache hao.... Lakini ni rafiki mzuri Sana , usimsau jamaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee story tamu sanaOooky Inaendelea..................
Wakati naendelea kujiuliza huyu agustino atakuwa kaenda wapi wazo likaniijia nimpigie tena yule ndugu yake labda atakuwa kapata baadhi ya information nikampigia tena akaniambia bro siumetoka kunipigia sasa muda si mrefu nimekwambia sina taarifa yake akinitafuta tu nitakupigia basi nikatoka pale getto nikaanza safari kuelekea centre pengine nikae pale naweza kumuona labda anapita na madumu nikampokee
Muda ulikuwa unayoyoma jua linaelekea kuzama nikaanza mwendo ukumbuke hapo alipokuwa anakaa ilikuwa kunaka umbali hadi kufika centre ikabidi nitembee haraka haraka hadi kufika pale nikakuta maboda boda kibao wamekaa wanapiga story, wengine wanakunywa uji kulikuwa kunamama anapika pale centre.
Mimi muda huo nimechanganyikiwa kila muda napiga simu ya agustino lakini haipatikani nikajipa moyo labda simu yake itakuwa imezima maana alikuwa anakatecno kadogo sana lakini touch screen. Basi nikaendelea kuzuga pale huku nikiendelea kusikiliza sauti za wale boda boda wa kibishana kuhusu simba na yanga, wengine wakiongea lugha za kienyeji
Wakati na zidi kutafakari huku nikikodolea macho kila piki piki inayopita pale nikawa na matumaini labda itakuwa ni agustino lakini nilikuwa naambulia patupu daa nikiangalia muda unazidi kwenda nikipiga simu haipokelewi mara muda kidogo naona message kutoka voda kifurushi chako kimeisha.
Ikabidi nisimame nitazame kibanda ambacho kiko karibu nikaona kimoja kiko upande mwingine nikavuka upande wa pili wa bara bara nikaenda kibandani nikatoa noti ya elfu moja nikapewa vocha ya mia tano nukarudishiwa mia tano
huku nikiendelea kukodolea macho kila usafiri unaopita pale
Ikabidi nivuke tena bara bara niende kukaa ile sehemu niliokuwa nimekaa kufika nataka kukwangua vocha mkononi siioni kusachi mfukoni na ile jero peke yake nikaanza kurudi kukagua pale chini labda nitakuwa nimedondosha wapi nikafatilia barabara yote hadi pale kibandani sikuona kitu.
Nikatoa tena ile 500 nikanunua vocha nyingine kuweka nampigia jamaa bado simu haipatikani daa nikaendelea kukaa pale hadi giza kabisa likaingia nikawaza huyu jamaa atakuwa yuko wapi nilikaa pale hadi wauza mboga kina mama kila mmoja akaanza kubeba sinia anaondoka zake
Daa nikapiga mawazo au kati ya zile taxi zilizokuwa zinapita hapa moja kati yake atakuwa alikuwa ni agustino ngoja nirudi getto kwake kufika pale nikakuta baadhi ya wapangaji pale kuwauliza wanasema bado jamaa hajarudi labda atakuwa yuko shuleni.
Asee niliondoka huku nimechoka hata nguvu za kutembea nilikuwa sina nilitembea hadi nikafika pale hostel nikamwambia muddy kuwa nimeenda kwa agustino lakini sijamkuta lakini jamaa alichukulia kawaida ikabidi kwenda jikoni kwa mpishi nikapiga nae msosi maana wanafunzi walikuwa wameshamaliza kula wengine wameenda prepo ikabidi niingie hostel nianze kuuchapa usingizi
Sijui wenzangu walikuwa wananionaje, nadhani walikuwa wananiona kama mtu aliyekata tamaa na masomo halafu siko serious maana prepo nilikuwa sionekani, soma yangu ya kusua sua kila siku nasingizia naumwa kichwa kumbe hali yangu naijua mwenyewe kunasiku nilikuwa natoka darasani naenda hostel nikapita nyuma ya darasa la wanaosoma arts nikasikia wanacheka vibaya sana huku head boy anasema wale majamaa hawako serious
Kama yule anae doji prepo anasingizia kuumwa kichwa halafu jioni unamuona anaenda kuvuta bangi asee nikapita tu walivyoniona dirishani wakazuga kunyamaza kumbe baharia nimesikia kila kitu.
Wakati nimejilaza pale kitandani huku nikiendelea kupiga ile namba ya agustino bila mafanikio nikawaza sana nitafanya vipi nimpate huyu jamaa maana nilikuwa na hofu sana, niliendelea kupiga ile simu bila mafanikio kesho yake asubuhi ilikuwa ni siku ya shule nikawahi kuamka mapema sana nikajiandaa vizuri nikavaa sare za shule nikamwabia muddy ngoja niwahi kwa agustino maana ndio nilikuwa namuona kama rafiki nilie kuwa nimebaki nae wengine wote wananiona kilaza
Basi nikaanza kutembea fasta hadi nikaiacha kwa mbali mipaka ya shule nikaanza mdogo mdogo kumezwa na vichaka vilivyokuwa vimetapakaa kila sehemu ya ule mtaa basi nilitembea haraka Hadi nikafika kwenye ile nyumba kuangalia mlango umefungwa ikabidi nigonge mlango wa yule mpangaji pale nikamuuliza agustino hajarudi asee
Majibu aliyonipa yalikuwa ni yakusikitisha sana na kuniogopesha maana yule mpangaji akasema alirudi hapa usiku sana na maaskri wakafungua mlango wakapekuwa ila hawakujua walichukua nini kisha wakaondoka nae yaani nilitaka kupooza palepale ilibidi nikae chini ya udongo nikajua mambo ndio yamesha haribika kabisa.
Basi ilibidi niondoke pale nikiwa na maswali mengi , nijajiuliza nirudi shuleni au nikachukue mizigo yangu niwaambie nimezidiwa naenda kulazwa hospital, nkajiuliza tena hivi shule na maisha yangu kipi bora wakati naendelea kujiuluza nikakumbuka yule ndugu yake alietuma mzigo ikabidi nimvutie kamba alipokea nikamwambia jamaa agustino kakamatwa na maaskari jamaa kashituka sana kaniuliza mara mbili mbili nikamwambia ndio walikujanae hadi kupekuwa alipopanga jamaa akakata simu.
Kisha nikatembea fasta kurudi shuleni nikaenda kuingia hadi hosteli nikakuta jamaa ndio wanajiandaa wanavaa nguo waende kwenye ratiba za shule mimi nilipofika nikaanza kuvua yale mavazi yangu kisha nikabadili nguo nyingine za kawaida nikasepa
Nilisema ngoja kwanza niende hadi kule kwa babu labda atakuwa kupigwa kaambiwa ataje wafuasi wake nikanza mchaka mchaka haraka zangu nimefika pale mtoni navuka haraka haraka nikateleza kiatu chote kikazama ndani ya matope ikabidi nivue nikaanza kutoa yale matope kisha nikavaa hivyo hivyo kibichi nikaendelea na safari........
Sent using Jamii Forums mobile app
Jaman ndoimeisha[emoji58]Nimechoka kutype imebidi nipige bla bla tumalize maana kunawatu walikuwa wanatamani wanipige ngumi kisa muendelezo
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]Usiku nikaanza kuwaza eti mtoto wangu, kaenda kwa mganga, kapanda maharage, kaenda kuyachuma kakuta Ni mimi, akajisemea nimuue mama au niachane na utajiri? Basi nikashtuka nikaanza kuomba na kukemea hiyo roho ya kishirikina kwa wanangu
Mungu niepushe mimi maisha matamu hivi
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah mkuu nimecheka hatar nataman Kama ungeelezea kwa kirefu zaidMkuu tukio kama hili limewahi kumtokea ndugu yangu kabisa wa baba yangu mkubwa akiwa na rafiki yake, walianzia kwa mganga ili kupata utajiri wakafuata masharti yote kabisa na sharti la mwisho wakapewa kamba za katani na kuambiwa waende nje kidogo ya kijiji (ni jirani na mbuga ya serengeti) watawakuta ngo'mbe wawafunge na zile kamba na kuwaleta kwa mganga baada ya hapo pesa itakuw ni ya kumwaga. Walipofika pale walichokiona kwanza ni vumbi linatimka na muda si mrefu Nyati wawili walioshiba wako vichwa chini spidi 240 km/h. Ndugu yangu anasema mbio alizotimka siku hiyo si za dunia hii. Hii si hadithi na mimi si muumini wa mambo hayo lakini tulikuwa tunajua katumwa kwenda kuleta ng'ombe na mganga na miaka ile mgodi wa Nyamongo (sasa North Mara) ulikuwa chini ya wenyeji na mambo ya ushirikina yalikuwa mengi sana.
nani kakudanganya..usidanganywe na waganga uchwara kama aliyekutana naye huyu jamaaUtajili wa aina hiyo huwa haudumu
Aisee!Baada ya kufuta lile tope mdogo mdogo nikaanza kupandisha kimpando cha kuelekea kwa babu nikafika pale nikazuga kama nimeenda kuomba ganja akaanza kusema asubuhi yote umekuja kufanya nini nikamwambia nimekuja kufata dawa.
Akaniambia yamebaki makapi , kisha akaniuliza yule mwenzako agustino mzigo amesha leta nikasema hapana.
Ikabidi aingie ndani aniletee yaleyale makapi
Nilitoka pale kwa babu nikijua agustino hakuuza mtu yoyote kwa polisi basi nikaanza kutembea kurudi shuleni kwa yale mavazi nilishindwa nitarudi vipi ikabidi nitafute sehemu nikae nitulie nione jinsi gani nitatunga hoja .
Nilikaa mahali nikawaza agustino hana ndugu mahali pale nikasema nitafanyaje niende hata kumuona kituoni nikakosa jibu maana na mimi nilikuwa na hofia usalama wangu nilimpigia tena ndugu yake yule nikamwambia awaambie wazazi wake hata na yeye pia aje kumuona maana haikuwa mbali sana
Nilimwambia pia aje niwaoneshe getto ikiwezekana wachukue vitu vyake vya muhimu wa mtunzie jamaa aliniambia yeye anatangulia kashamwambia baba yake atakuja kesho
Basi alivyofika nilienda kumpokea pale centre tukaenda hadi getto jamaa akajitambulisha kuwa nikakaake tukavunja kufuli tumeingia ndani tafuta vitu muhimu kama simu, kadi ya banki,walet vyote hakuna na baadhi ya vitu vingine sivikumbuki
Basi yule kaka yake japo wakuvuta na kamba kesho yake akasema nije nimpeleke kituoni tumpelekee msosi mimi nilikubali ila nikamwambia nitabaki mbali kabisa usikie maafande watakwambiaje.
Kweli kesho yake nilivunja vipindi nikamsindikiza Yule jamaa alivyorudi akaniambia walimuoji ikabidi awaambie yeye ni kaka yake alitokea wilaya nyingine kuja kumletea msosi, Jamaa aliulizia kama anaweza muwekea dhamana ya pale kituoni maafande walikataa wakasema tena jarada lake linapelekwa mahakama ya wilaya
Daa jamaa alichoka tulirudi nae hadi getto kesho yake tena tukaenda kumuona na yule jamaa ndio nikajua kweli bongo nyoso yani hawakupi nafasi ya kuongea na mtu ukishapeleka msosi unaonja askari wanachukua unatembea mbele huwezi ongea hata siri na mtuumiwa , Halafu kituoni kumbe hawapiki sasa nikawa najiuliza hivi waliokamatwa na hawana ndugu karibu huwa wanakula nini kabla hawajapelekwa magereza
Kiufupi agustino kesi yake ilipelekwa mahakama ya wilaya, tena alishitakiwa na jamuhuri kwa kosa la kukamatwa na zaidi ya kili 100 za bangi tena alikamatwa na ushahidi kabisa boda boda wake kwa kujitetea ikabidi amchomee kabisa alisimama kama shahidi wa mwisho
Kulingana na mapambano ya bangi kipindi kile bila huruma hakimu alimtundika miaka 30 jela. Nimechoka kutype
Oky ngoja niendelee nakumbuka siku ya mwisho nimeenda kumuona pale magereza nikiwa nimeshika mkate na vipande vya sabuni + wembe nikajua labda kidogo kule magereza kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuongea na mfungwa asee kufika tuliruhusiwa raia kama 20 hivi kwa mkupuo eti tuongee na wafungwa wetu kwa zile kelele sikuweza kumsikia vizuri neno nililolisikia kutoka kwake ni MWANANGU ENDELEA KUKOMAA
Na hapo nilikuwa nimetoka shuleni wilaya nyingine wakati natoka kwenye lile gereza nilijisikua huzuni sana kiasi kwamba nilijikuta na bubujikwa na machozi baada kama ya mwaka na nusu kupita nikiwa chuoni niliongea na yule kaka yake akaniambia agustino alihamishwa butimba mwanza
Kunakipindi niliona magufuli ameenda pale niliangaika sana kumtafuta agustino kwenye zile camera lakini sikufanikiwa kumuona rafiki yangu kipenzi now kamanda agustino amemaliza miaka 5 gerezani. kwa kifungo cha miaka 30 kwa jinsi wanavyo hesabu amebakiza miaka 15 gerezan
Mimi bado nikijana sana mwaka huu mwezi fulani na fikisha 24 yrs damu bado inachemka naendelea kupambana rafiki yangu mpambanaji agustino, kufa na kupona, kwa hali na mali nijipanue kiuchumii ili siku ukitoka gerezani husije kunicheka eti nilikuwa napoteza muda kitaa
Nataka uje unikute nimesha tengeneza bara bara nzuri ya kiuchumi uje tuishi maisha ya kidoni kama zilivyokuwa ndoto zako.
Nilichojifunza urafiki bora haupimwi kwa muda unapimwa kwa matendo maana niliishi na agustino katika kipindi kifupi sana lakini ameacha historia kubwa sana ndani ya maisha yangu
Nineandika kwa haraka vibaya vibaya kama kutakuwa na makosa tusameeane
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wwe ushaenda kwa mganga?na je unamafanikio uliopata kupitia hao waganga?nani kakudanganya..usidanganywe na waganga uchwara kama aliyekutana naye huyu jamaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wwe ushaenda kwa mganga?na je unamafanikio uliopata kupitia hao waganga?