Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Ndugu kweli kila kifo ni mpango wa Mungu lakini wakati mwingine aina au sababu za kifo husababishwa na wanadamu na ndio maana huko mahakamani kuna kesi za mauaji ingawa kifo ni mipango ya Mungu........

Lazima tujadili mambo kwa upana na mawazo huru ili kufikia muafaka kama taifa kwa maslahi ya taifa........

Tanzania ni nchi yetu sote haipaswi kikundi cha watu wachache kwa maslahi yao kuwa hatima za mamilioni ya WaTanzania..........

Kama hiyo Bandari ni kwa ajili ya WaTanzania na itawanufaisha WaTanzania kwanini WaTanzania wanafichwa kilichomo kwenye mkataba huo.....???

Kwanini iwe siri....??

Kifo cha Ole Nasha ni kifo kama kingine lakini inawezekana motive ya kifo chake ikawa imepangwa kwa manufaa ya wengine.......
Kuna mkataba gani uliwahi kuona?!!..
 
Mikataba ya nchi huwa ni SIRI. ..sasa unataka ujue ili iweje? kwani huiamini Serikali yako ya Chama Cha Mapinduzi kwamba inaweza kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa umma? kwa nini ?

Usiwe na mawazo hayo, ondoka wasiwasi CCM ipo makini sana kila nyanja, kila sekta, kila mkataba - Kifungu kwa kifungu, neno kwa neno.
 
Mikataba ya nchi huwa ni SIRI. ..sasa unataka ujue ili iweje? kwani huiamini Serikali yako ya Chama Cha Mapinduzi kwamba inaweza kuingia mikataba isiyo na maslahi kwa umma? kwa nini ?

Usiwe na mawazo hayo, ondoka wasiwasi CCM ipo makini sana kila nyanja, kila sekta, kila mkataba - Kifungu kwa kifungu, neno kwa neno.
una anzaje kuiamini serikali inayo ongozwa na kiumbe ambae hajakamilika kama sisi tuu..?
 
Tuache ujinga wa kuwa na dhana mbaya na kubeza kila linalofanywa na utawala uliopo na kutaka kuaminisha watu tena kwa nguvu kwamba eti ni Magufuli tu ndiye aliyekuwa na nia njema na nchi hii na kwamba wengine wote ni wapigaji tu,huko ni kumkufuru na kumkosea mwenyezi Mungu kwani mwenyezi Mungu kama aliweza kumuumba huyo Magufuli atashindwaje kuumba wengine kama yeye?
Binafsi naamini utendaji kazi wa Rais Samia ni wa makini na ni wenye lengo la kuleta manufaa kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla hivyo sikubaliani na upuuzi wowote unaeletwa na mtu yeyote kwa sababu ya chuki zake binafsi.
Najua hivi sasa kuna vita kubwa inayoendelea baina ya makundi fulani fulani kwa sababu ya utashi wao binafsi tu na wengine wamekuwa wakipinga utawala wa Rais Samia lakini huwezi kuwasikia wakizisema wazi sababu zao(halisi) bali wao wamebaki tu kujificha kwenye box la "uzalendo".
Watu hawa ndio wamekuwa vinara wa kuzua uongo kila kukicha ili tu watimize kile wanachokusudia,
Watu hawa ni sawa na chui waliojivika ngozi ya kondoo,
Watu hawa ukiwatizama usoni wanajionesha tofauti na walichokificha ndani ya mioyo yao.
Hawa watu ni wanafiki na ni wabinafsi na ni watu hatari sana.
Jibu hoja mkuu za hapo.
 
Huu mradi yamkini umetoa watu wengi roho ili utekelezwe tu.
 
Back
Top Bottom