Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Kwa hiyo badala ya kuomba apewe uthibitisho hela zimetumika wapi anaanza kwanza na kufukuza? Violence first before peaceful solution. Ikikutwa ni kweli hizo hela zimetumika kihalali? *********** kweli hawa jamaa. Watu magu alioweka 99% machizi kichwani yamejaa matope tu, yanawaza kukunwa asubuhi hadi usiku na magu, seriously how can people be this stupid? Nyani kabisa.

Who the f**k is magufuli? Ye ajenge hiyo nyumba kwa 40mil tuone. Sio kila kitu anachokiongea kinageuka kua ka sheria kumi za mungu. Tanzania amkeni ujinga umepitiliza. This f****r can say anything na watu mnabeba kama kilivyo as if sio binadamu tena wote tunajua ni binadamu mpenda misifa ya kijinga. For https://jamii.app/JFUserGuide sake
 
Hao unaosema walikuwa wanafanya wizi, ubadhirifu wamechukuliwa hatua gani hadi sasa?

Alituambia majizi yamehamia upinzani, mbona hakuyachukulia hatua? yamerudi na akayapokea sasa yupo nayo ccm.
Wewe unataka wachukuliwe hatua gani mkuu, wanao shitakiwa kila siku sio ndio hao mnao watetea kuwaita ni wanaharakati mnasema wanapewa/ wanabambikiwa kesi?
 
Dam55 TAKUKURU ilikuwepo tangu enzi za Mkapa na wamekuwa wakitimiza wajibu wao kama kawaida. Tofauti ni kwamba hivi sasa matangazo yamekuzwa mno!
Wakati watu wanamiliki nyumba 70 na majiaba ya pesa ndani (wakina masamaki ) hao takukuru unaosema walikuwepo walikuwa wanafanya kazi gani.?
 
Brg. Mbungo Chamwino na Mpwapwa zipo mkoani Dodoma na siyo jijini Dodoma. Makosa madogo kama haya yanaweza kushusha hadhi ya barua yako na wewe mwenyewe pia.

Hahhaaaa umepiga spana mule mule

Watu wengi walilemazwa na mfumo wa Jiji la Dsm lilivyo. Jiji La Dar lilikua linaundwa na wilaya zote 3(Saivi 5) na Mkoa wa Dar ulikua na wilaya hizo hizo

Ila ni tofauti kwa Jiji kama la Mwanza ambako kuna Halmashauri ya Jiji na Halmashauri nyingine kama Nyamagana nadhani ambazo ziko nje ya Jiji

Vivyo hivyo kwa Dodoma. Jiji la Dodoma ni ile iliyokua Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma pekeyake. Ila Halmashauri zingine Kongwa,Mpwapwa,Kondoa,Bahi nk ziko nje ya jiji

Sijui hawa viongozi wanashindwaje kuelewa vitu vidogo namna hii
 
We unafikiri zile jeuri za unanijua mimi nani zilikuwa zinatokana na nini mkuu?

Ilifika wakati wakati mtu anaajiriwa lakini ndani ya miaka 4 ana mali za milioni 150 na mshahara wake ni milioni 1 kwa mwezi
Kwani sahivi Hao watu wanao piga hawapo....
Kila system Kuna watu wanafaidika nayo....

Ova
 
Wakati watu wanamiliki nyumba 70 na majiaba ya pesa ndani (wakina masamaki ) hao takukuru unaosema walikuwepo walikuwa wanafanya kazi gani.?
Kwani umesikia Masamaki amefungwa au kuadhibiwa kwa cho chote.
 
Sasa nyumba ya milioni 60 au 40 mbona ndogo na ya kawaida sana jamani duh
Hapo nao wamezidisha chumvi
Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kuwa Magufuli na Majaliwa wanaweza wakaona wamejenga kwa gharama ndogo wakasahau vitu vingi wanavyopewa bure kama baadhi ya vifaa vya ujenzi na pia baadhi ya watumishi wa umma kufanya kazi bila malipo. Vyote hivyo vinafanywa na wafanya biashara na watumishi kwa kujipendekeza.
 
Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kuwa Magufuli na Majaliwa wanaweza wakaona wamejenga kwa gharama ndogo wakasahau vitu vingi wanavyopewa bure kama baadhi ya vifaa vya ujenzi na pia baadhi ya watumishi wa umma kufanya kazi bila malipo. Vyote hivyo vinafanywa na wafanya biashara na watumishi kwa kujipendekeza.
Haa
Ila Kweli
Iwapo Wamejenga Na Kuchimba Kwa Vipimo Vinavyotakiwa Kabisa Yaweza Kuwa Sahihi
 
Tatizo ni nini? Rais kashaona ''upigaji'' kwenye ujenzi wa nyumba TAKUKURU, kaona kwa macho lakini pia ameona kupitia taarifa za kitaalam kutoka vyombo vya kiserikali. Nyiye TAKUKURU mnaunda Tume kuchunguza. Mnachunguza nini? ningekuwa mimi labda ikilazimu ningeunda tume kwa siri ichunguze ni kiasi gani kimepigwa. Nikashabaini hilo, nachukua hatua kwa watendaji wangu kisha naenda kwa Rais namweleza kuwa ''Mheshimiwa ulikuwa sahihi siku ile kuniwakia, ukweli ni kuwa Tsh ........zimepigwa pale na tayari nimeshachukua hatua hizi..................

Tafuteni washauri wazuri wa kuwasaidia namna ya kudeal na haya mambo. Pia jitahidini sana kumwelewa Rais.
Brigadier ame amua ku grab attention tu ila sidhani kama dhamira yake ni ya dhati kabisa yakufatilia huo upigaji apo naona kama mlinda ugali tu, Hapo ilipaswa afukuze mwizi kimya kimya na kwa vile nae ana clearance kubwa ya kumuona Mkulu basi ilipaswa aandae tu report then aibuke nayo state house na file lake kumueleza mkuu madudu na hatua alizochukua BTW kuna hujuma sana baada ya hawa wanajeshi kupewa hivi vyeo kwenye hizi taasisi mana seniors wengi wanahisi wao hawaminiki ndio mana wanaletewa Wanajeshi kulead taasisi wengine tayari walikuwa kwenye mategemo ya kuwa promoted angalia hata magereza Japo CGP yupo active sana ila figisu pia zipo ili kuwachafua ukiangalia hata hii mishe ya Takukuru utaona kabisa kuwa watu wa chini yake ndio wamemuingiza chaka Brigadier Mbugo
Mi naona mjeda akiwa promoted kwenye ivi vyeo vya kiraia apewe Fursa ya kutengeneza team yake ambayo anahisi atasonga nayo poa kuliko kukuta watu ofisini ambao automatic hawapo happy na ujio wako
 
Juzi Taasisi yetu tukufu ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) WALIMWALIKA (?!) Mh.Rais kuzindua jengo lao pale Dodoma! Yaelekea majengo kama hayo yaapo pia mikoa mingine
Bahati mbaya sana kwao Mh Rais aliuponda mradi huo kuwa hauna Value for Money!
Leo nimesoma kwenye Vyombo vya Habari kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kawasimamisha watumishi wake kadhaa kutokana na kadhia hiyo!
Hii habari ni nzito kwa mustakabali wa Utawala Bora hapa nchini,na kuna maswali mengi sana ya kujiuliza:
Mosi,inakuwaje TAKUKURU wanakuwa na madudu haya,ilhali wao ndio wathibiti
Pili,kwa namna Mkurugenzi wa TAKUKURU,alivyoitkia inadhihirisha kuwa anakubaliana na Hoja ya Rais kuwa wametupiga! na kama wametupiga basi hii ni hatari!
Tatu,inakuwaje Taasisi kubwa inamwalikaa Rais kwenye magumashi .Yaani hawana Inteljinsia ya ndani ya kupunguza Vihatarishi kwa kiwango hiki!?
Je kuna sababu gani kumwalika Rais kweye vihafla vidogo dogo kama hivi! au ndio mambo ya Awamu ya TANO NI LAZIMA UONEKANE !
 
TAKUKURU NG'ATA...

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbung'o, amewasimamisha kazi watumishi 9, ambao walihusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo Saba ya Taasisi hiyo yaliyojengwa Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

=====

Hapo jana katika Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU-Chamwino) uliofanyika Jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema jengo hilo halikuwa la yeye kwenda kufungua lakini pia gharama iliyotumika katika ujenzi ni ya juu sana.

Alisema Waziri Mkuu alimwambia nyumba hiyo yeye angejenga wa Milioni 60 huku Rais Magufuli mwenyewe akisema amejenga nyumba yenye ukubwa kama huo huko kwao kwa Milioni 40

Pia soma:
Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?


Rais hajafurahishwa na jengo la TAKUKURU

Mheshimiwa Rais Nakupongeza sana jinsi unavowawajibisha watu wanaotafuna mali ya uma.
Ila kutumia 40Mil kujenga jenga la aina ile kama ulivoainisha ni kama haiwezekani . Gharama za ujenzi zinategemeana sana na aina ya material specifications kwenye BoQ ndo mana kwa sh Mil.140 inayosadikiwa kutumiwa na Takukuru kujenga hiyo ofisi ukinipa mimi ntajenga jengo la ghorofa la kuishi na itatosha WITH JUST SIMPLE MATERIALS . Lakini mwingine fedha iyoiyo anajenga ya chini na inaweza isitoshe.Kwa hiyo hoja hapa ni materials specifications, mfano kama ni tiles ni za china au Spain/italy, sanitary fittings ni za china au ulaya mabati ni ya wapi, madirisha ni Aluminmium au PVC? je kioo chake size mm ngapi? nk Tukijua haya tutaweza kujua kama hawa jamaa wamekula hela au la na ni kwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom