Na ni kwa nini uweke watu kutoka kada nyingine kwenye senior positions?
Nijuavyo mimi, senior positions ni sehemu ya promotion anayopewa mtu baada ya uadilifu na experince kwenye mid-positions za kada husika.
Je, kama hakuna waadilifu au uadilifu wao unatiliwa mashaka watu waliopo kwenye taasisi husika?
Pia tutofautishe kati ya taasisi na kada.
Jambo lingine tutofautishe uongozi au utawala na nafasi zile za chini za kiutendaji wa shughuli husika za kila siku zinazohitaji uwe umesomea fani husika, yaani uwe na taaluma ya kada husika.
Mkurugenzi Mkuu ni ngazi ya uongozi wa juu ambayo ni ya kisera na maono , ni zaidi ya kufanya daily operations za domain husika.
Kwenye ngazi za kiungozi na utendaji au mgawanyo wa majukumu kwenye taassi kubwa Mkurugenzi mkuu ni strategic level siyo managerial level au siyo operational level ambazo zinahitaji lazima ziwe na watu wa kada au fani husika. Yaani yule tunaweza kumlinganisha na raisi wa taasisi husika.
Raisi anakuwa na wasaidizi kila idara ambao ndiyo watu wa fani husika wa kazi inazofanyika na hizo idara. Yeye kidogo anafanana na General Manager ambae chini yake kuna Manager wa Fedha, ICT, Manager wa Operesheni, Mauzo, Ubora na Viwango, Usimamizi Miliki, n.k.
Hapo unaweza kubadili jina
manager na kuweka jina
mkurugenzi mfano Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi wa Fedha, n.k.
Hivyo kwa kumalizia niseme Mkurugenzi Mkuu au Kamishina Mkuu anaweza kutoka nje ya taasisi husika kutokana na sifa flani flani. Utaona mfumo wa TAKUKURU umekaa kama wa kijeshi au wa kiaskari kidogo na ndiyo maana wale watendaji wa kawaida wanaenda mafunzo kidogo ya kiaskari.
Mtu mwenye sifa toka kada za uaskari au kijeshi anaweza kuja kuongoza hiyo taasisi hasa kama malengo makubwa kuja kujenga nidhamu na uadilifu kama unaotakiwa majeshini. The same kwa jeshi la magereza.