Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Tatizo ni nini? Rais kashaona ''upigaji'' kwenye ujenzi wa nyumba TAKUKURU, kaona kwa macho lakini pia ameona kupitia taarifa za kitaalam kutoka vyombo vya kiserikali. Nyiye TAKUKURU mnaunda Tume kuchunguza. Mnachunguza nini? ningekuwa mimi labda ikilazimu ningeunda tume kwa siri ichunguze ni kiasi gani kimepigwa. Nikashabaini hilo, nachukua hatua kwa watendaji wangu kisha naenda kwa Rais namweleza kuwa ''Mheshimiwa ulikuwa sahihi siku ile kuniwakia, ukweli ni kuwa Tsh ........zimepigwa pale na tayari nimeshachukua hatua hizi..................

Tafuteni washauri wazuri wa kuwasaidia namna ya kudeal na haya mambo. Pia jitahidini sana kumwelewa Rais.
 
Yeye mwenyewe alitakiwa ajiuzulu kwa kujipendekeza mpaka akashtukiwa
Kweli mkuu, huyo Jenerali kaaibishwa vibaya sana.
Ameonekana hajui wala hakustuka mapema kwamba hivyo vibanda ni bomu alilotakiwa kulitegua kabla Magufuli hajamwambia hivyo.
Magu alitamani amungoe hizo nyota,kilichobakia aombe kurudi kambini.
 
TAKUKURU NG'ATA...

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbung'o, amewasimamisha kazi watumishi 9, ambao walihusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo Saba ya Taasisi hiyo yaliyojengwa Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

=====

Hapo jana katika Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU-Chamwino) uliofanyika Jijini Dodoma, Rais Magufuli alisema jengo hilo halikuwa la yeye kwenda kufungua lakini pia gharama iliyotumika katika ujenzi ni ya juu sana.

Alisema Waziri Mkuu alimwambia nyumba hiyo yeye angejenga wa Milioni 60 huku Rais Magufuli mwenyewe akisema amejenga nyumba yenye ukubwa kama huo huko kwao kwa Milioni 40

Pia soma:
Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Rais hajafurahishwa na jengo la TAKUKURU

Hapa kuna dalili za kutafuta (favor) upendeleo yaani staili ya kutoa hongo kama Rais alivyosema kutaka kujenga nyumba ya TAKUKURU Chato wakati nyumba tayari ipo! Walijenga Ruangwa kwa Waziri Mkuu - je hii siyo dalili za kutoa hongo? Enlighten us please.
 
Kweli mkuu, huyo Jenerali kaaibishwa vibaya sana.
Ameonekana hajui wala hakustuka mapema kwamba hivyo vibanda ni bomu alilotakiwa kulitegua kabla Magufuli hajamwambia hivyo.
Magu alitamani amungoe hizo nyota,kilichobakia aombe kurudi kambini.
Bora kambini,maana majukwaa ya wanasiasa ni kuvuana nguo tu
 
Sasa kama Rais ni mkali kiasi hiki lakini watu bado wanapiga mpaka ndani ya takukuru sa hizo zama za wana demokrasia je hali ilikuwaje sasa wakuu.
We unafikiri zile jeuri za unanijua mimi nani zilikuwa zinatokana na nini mkuu?

Ilifika wakati wakati mtu anaajiriwa lakini ndani ya miaka 4 ana mali za milioni 150 na mshahara wake ni milioni 1 kwa mwezi
 
Sasa kama Rais ni mkali kiasi hiki lakini watu bado wanapiga mpaka ndani ya takukuru sa hizo zama za wana demokrasia je hali ilikuwaje sasa wakuu.
Hali ilikuwa Mbaya Sana , ujio wa Magufuli ulikua Maalum, na ndio maana wengine hatuachi kumsupport mpaka amalize awamu zake zote mbili.
 
Hali ilikuwa Mbaya Sana , ujio wa Magufuli ulikua Maalum, na ndio maana wengine hatuachi kumsupport mpaka amalize awamu zake zote mbili.
Pia Wafanyakzi,Wanafunzi wa vyuo,Wastaafu wanam support sana kwa anayowafanyia.

Mwambie asante sana
 
Viongozi wengi nchi kama sindano za kushonea hadi itiwe uzi ndo inafanya kazi
 
Rais wangu huyu jamaa hataki mchezo,yule jamaa mkuu wa takukuru kaambiwa "simama wewe na tumbo lako kubwa,ndo mana mnene mnene hivi"[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji87][emoji87] maneno hayo kayaongea bwana Jiwe. Aseee
 
Back
Top Bottom