Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Baada ya Rais kung'aka, Mkurugenzi TAKUKURU awang'ata watumishi 9 waliohusika ujenzi/usimamizi wa majengo 7 ya TAKUKURU

Sasa kama Rais ni mkali kiasi hiki lakini watu bado wanapiga mpaka ndani ya takukuru sa hizo zama za wana demokrasia je hali ilikuwaje sasa wakuu.
 
Lengo hasa la tume huru hiyo ni nini? Je wanaweza kuja na maoni tofauti na ya mheshimiwa?
 
Ahahahah ila Mh. Magufuli huyu baba tutakuja kumkumbuka mno. "hebu kaa bwana husije kunifanya nione ata hizo nyota nilikupa bure" Rais lazima uwe mtu wa kufanya maamuzi magumu, wanyooshe tu baba hakuna namna.
 
Naona ameamka kutoka usingizini.....na ukute kwenye mgao alikuwepo sema mzee amesanuka ndio anajidai kuchukua hatua.
Hapana, Jmkuu wake alisikika akisema "hizi gharama nimezisikia hata kabla wewe hujaingia TAKUKURU .."
 
Aliyetoa wazo la kujenga ofisi chato kama ni yeye mwenyewe nayeye ajiuzulu
 
Mh. Magufuli na wateuliwa wake toka JWTZ aliowateua kusimamia taasisi mbalimbali nje ya jeshi kuweni macho wakati wote.
Kwa hulka ya binadamu watu waliokuwa kwenye hizo taasisi zingine wanaweza kutopenda namna wasivyo aminiwa na kuletewa mtu toka nje ya taasisi yao.
Wanaweza kuanza kuwatengenezea mizengwe wachafuke ili wanajeshi wasiaminiwe tena kama sasa.
Wateuliwa pigeni kazi mkiwa macho, muwe ACTIVE, PROACTIVE lakini kamwe msiwe REACTIVE inaweza kuwagharimu.
 
Back
Top Bottom