Kama ilivyoshindwa mambo mengi, kufikia hadi kuuza Bandari basi ni vema sasa kurejesha tena usafiri wa Daladala kama ilivyokuwa awali Kutoka Kariako hadi Mbezi kupitia Kimara.
Hii ni kwa sababu wakazi wa maeneo hayo wanayo haki ya kusafiri kutoka makwao na kwenda mjini.
Naona dalili ya Jambo baya kutokea muda wowote kwenye Stendi ya Mwendokasi Gerezani
Angalia hali hii, hawa wote wanazo tiketi mkononi, kitendo cha kuwauzia tiketi huku mabasi yakiwa hamna japo ni Wizi lakini pia kunasababisha manung'uniko yatakayokuja kuzaa maafa kwa ngumi kuvurumishwa kwenye stendi hiyo
Lakini kwanini tufike huko?
View attachment 2997552