DOKEZO Baada ya Serikali kushindwa ni muda sasa wa kurejesha Daladala za kusafirisha abiria Kariakoo-Kimara-Mbezi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hatua gani hapo imepigwa ikiwa tatizo badala ya kutatuliwa, ndio limeongezeka?
mabasi ya mwendokasi yalikuepo ya kutosha na hapakua na malalamiko. hivi sasa kumetokea changamoto kidogo tu ndio turudi nyuma kweli πŸ’

tayari mbia atakaefanya kazi za usafiri wa mwendokasi ameshapatikana ni suala la muda tu ataanza kutoa huduma πŸ’

suala la kukata tamaa panapotokea changamoto Fulani, libaki kua ni suala binafsi tu. But as country we can not tolerate that at all.πŸ’

necessary efforts and measure are in place, the challenge is going to be addressed as soon as possible, relax kua na subra kidogo tu πŸ’
 
Kwahiyo raia waendelee kupata tabu mpaka huo mchakato ukamilike?

Unajua hiyo vurugu ya kugombea bus inaweza sababisha vifo au ulemavu kwa wengine?
 
Kwahiyo raia waendelee kupata tabu mpaka huo mchakato ukamilike?

Unajua hiyo vurugu ya kugombea bus inaweza sababisha vifo au ulemavu kwa wengine?
suala hapa, sio raia waendelee kupata tabu, wala kusitisha huduma iliyopo, kwamba inaweza kuleta madhara kwa abiria wanaoigombania, au kurudisha ile ya zamani anayo pendekeza mtoa hoja πŸ’

suala hapa ni kwamba, hao abiria ni Lazima wapate huduma bora ya usafiri, na hicho ndicho kinacho fanyiwa kazi na wahusika wa kisekta kama ambavyo nimeeleza awali πŸ’

inafahamika abiria wanapata tabu sana, lakini pia kama serikali, shinikizo ni kubwa zaidi na tupo katika vikao vya bajeti.....

hata hivyo bado ustahimilivu na subra vinahitajika kwa watumia usafiri huo, wakati jitihada na hatua za makusudi kutatua changamoto hiyo zikifanyiwa kazi πŸ’h
 
Ni kupewa kampuni binafsi ili iendeshe yaani watapiga pesa balaa serikalini ipewe %%%

Tujifunze kwenye nchi zilizo Endelea mfano German,Finland, Switzerland, uingereza, marekani
Kweli kabisa .
Tatizo serikali inataka nayo ifanye biashara ndo tatizo usimamizi unakuwa mdogo na watu wanaibua changamoto ili wapige hela
 
Sure
 
ni ukosefu wa akili tu. kitu kidogo kama hicho kuendesha ni rahisi sana. kama raia wapo wengi nanmna hiyo, ina maanisha mradi una wateja wengi wa kutosha, wanashindwa nini kuongeza mabasi? badala ya raia kusubiri bus iwe vise versa?kwenye biashar akama hiyo unachohitaji kingine ni nini kama wateja/wasafiri wapo na wanapanga hadi foleni kwako? Mungu amekupa wateja kwenye biashara yako, halafu unashindwa kuwasafirisha, unahitaji Mungu akupe nini kingine?

kama mabasi ya kichina ni mabovu, mbona ulaya yapo hadi ya mtumba? ni kweli mradi wowote wa serikali watu huwa wanaiba kwasababu wanaona kama hakuna mwenye nacho, basi, wekeni tenda, hata wazungu waje wawekeze, walete mabasi ya kutosha kama walivyo wao huko. Ulaya unaweza kununua ticket yako ya mwezi mzima au ya wiki, au ya siku moja, unapita mlangoni unascan tu unaendelea, mabasi yao ni mazuri na reasonable kuliko hiyo mingalangala ya kichina.

Na hiyo garama ya usafiri toka kimara hadi posta haitofautiani saana na garama ya usafiri ulaya, hata ikizidi ni kidogo sana, na kwa wingi wa abiria, hata mzungu akija kuwekeza hapa kwa kuleta mabasi mengi, hatakula hasara sana. mkurugenzi wa iyo mradi kama ameshindwa fukuza, wapo watanzania wengi tu wanaweza kufanya hiyo kazi.
 
Wenye mabasi wakiona abiria ni wengi wanaona fursa ya kuongeza mabasi(Akili Ya Biashara). Serikali haijawahi kuwa na akili ya biashara.
 
Kwahiyo raia waendelee kupata tabu mpaka huo mchakato ukamilike?

Unajua hiyo vurugu ya kugombea bus inaweza sababisha vifo au ulemavu kwa wengine?
Imesababisha video na ulemavu kiasi gani Hadi Sasa!?..unafiki tu,uweke daladala moro road kutapitika!...ulikuwepo 2007/8 ukashuhudia foleni hiyo Barbara!?..Leo magari yameongezeka unataka urudishe,yatapaki wapi pale kkoo?
 
Upumbavu sana, yaani TUMESHINDWA kupiga hesabu peak time tunahitaji magari kiasi gani? kupunguza huo umati wa watu vituoni.

Tumeshindwa kumaintain maintenance ya magari kiasi chakuwa na availability ya magari yakutosha muda wote?
 
Umeongea jamba jema sana, yani huu mradi ungeendelea pamojana madaladala ya Mbezi kariakoo via Morogororoad na Mbezi posta via morogororoad. Watu wanaumia, wanapoteza vitu vyao kisahuu mradi jamani? Hivi viongozi hawalioni hii kelele?
 
Imesababisha video na ulemavu kiasi gani Hadi Sasa!?..unafiki tu,uweke daladala moro road kutapitika!...ulikuwepo 2007/8 ukashuhudia foleni hiyo Barbara!?..Leo magari yameongezeka unataka urudishe,yatapaki wapi pale kkoo?
Acha iongo wewe ushaona foleni inayosababishwa na vibajaji vilivyo jimilikishia njia hiyo? Usiongee kama1sio mtumiaji hizi bus, usumbufu wake ni mkubwa sana
 

Mabasi ya Mwarabu yako njiani .... Mkwe alisema by September shida ya usafuri itakuwa ni history.
 
Kwa maoni yangu bora wangeyatoa yote road daladala za kawaida zifanye kazi kwenye hiyo road ya mwendo kasi kwisha sinajingine
 
Watu wa Route za Kimara mjini kati mnateseka sana poleni sana.
 
Mambo ya public goods hakuna mtu mwenye uchungu na mali za umma. Inasikitisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…