Baada ya Tanzania kubania wageni kufanya biashara nchini, Kenya imejibu mapigo

Baada ya Tanzania kubania wageni kufanya biashara nchini, Kenya imejibu mapigo

Kusema ukweli serikali hawa jatenda haki kabisa, kwa sababu hata watz wapo wengi tu kwenye inchi za watu, wana tafuta maisha.

Mm naona kilicho pelekea kupitisha hiyo Sheria ni pressure ya uchaguzi tu ili wapate wapiga kura hakuna kingine.
Hivi CCM pressure ya uchaguzi wanaotoa wapi?. Wameifungia CHADEMA ambayo ingewapa pressure, wanaogopa nini sasa hivi wakti wamejichaguwa tayari?
 
Juzi, niliandika kuhusu agizo la Waziri Selemani Jafo linalowazuia raia wa kigeni kushiriki katika aina mbalimbali za biashara ndogondogo na za kati nchini Tanzania, amri ambayo imezua mapokezi yenye sura mbili: pongezi ndani ya nchi na tahadhari kali katika ngazi ya kimataifa.

SOMA: Waziri Jafo Awazuia Raia wa Kigeni Kufanya Baadhi ya Biashara Nchini.

Agizo hilo, linalojulikana rasmi kama The Business Licensing (Prohibition of Business Activities for Non-Citizens) Order, 2025, linaainisha aina 15 za shughuli za kibiashara ambazo kuanzia sasa hazitaruhusiwa kufanywa na raia wasio Watanzania, ikiwemo raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community – EAC).

Biashara hizo ni pamoja na huduma za uhamishaji wa pesa kwa simu (mobile money transfers), biashara ya rejareja (retail trading) isipokuwa maduka makubwa (supermarkets), karakana za kurekebisha vifaa vya kielektroniki (electronic repair shops), saluni, usafi wa mazingira (cleaning services), udalali wa mali isiyohamishika (real estate brokerage), huduma za utalii (tour guiding), pamoja na umiliki wa viwanda vidogo na vya kati (micro and small industries).

Kwa Watanzania wengi, hizi si biashara tu, bali ni njia za kiuchumi za kujikimu katika maisha yetu ya kila siku, hivyo hatua hii imepokelewa kama uamuzi wa muda mrefu uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu ili kulinda ujasiriamali wa ndani dhidi ya uingiliaji wa kibiashara wa wageni, hasa katika masoko ya mijini.

Hata hivyo, ushindi huu wa ndani umegeuka kwa haraka kuwa mgogoro wa kibiashara wa kimataifa kati ta Kenya na Tanzania.

Tarehe 30 Julai 2025, Serikali ya Kenya ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari ikionesha wasiwasi mkubwa kuhusu agizo hilo la Tanzania. Kenya imesema kwamba hatua hiyo inakiuka Common Market Protocol (CMP) ya EAC, hasa Ibara ya 13 inayotoa haki kwa raia wa EAC kuanzisha na kuendesha biashara katika nchi wanachama kwa misingi ya usawa na bila ubaguzi wa uraia (non-discrimination).

Soma Pia: Aina za biashara zilizopigwa marufuku kwa wageni wasio raia

Kenya imeeleza kwamba, pamoja na kutambua na kuheshimu mamlaka kamili ya nchi wanachama wa EAC katika kutunga sheria na sera za ndani, hatua zenye athari kimataifa zinapaswa kuchukuliwa kwa kuzingatia mashauriano (consultation), uwazi (transparency) na uratibu wa pamoja (regional coordination), misingi ambayo ndiyo kiini cha mchakato mzima wa ujumuishaji wa kimataifa (regional integration).

Kwa mtazamo wa Kenya, agizo la Tanzania ni mabadiliko ya sera ya upande mmoja (unilateral) yanayoweza kuhatarisha mafanikio yaliyopatikana katika uhuru wa kusafirisha bidhaa, huduma, na watu ndani ya ukanda wa EAC.

Kwa maoni yangu, mgogoro huu unaweza kuwa na athari mbili kuu: za kisheria (legal implications) na kiuchumi (economic implications).

Kwa upande wa sheria, Tanzania italazimika kuonesha kwamba hatua yake inefikiwa kwa maslahi ya umma (public interests) lakini pia ithibitishe wajibu wake wa kimikataba (treaty obligations) chini ya makubaliano ya EAC.

Kiuchumi, swali linabaki: Je, hatua hii ya kujilinda kiuchumi (protectionist posture) ni msaada au ni kikwazo kwa sera ya EAC ya kuwa soko lenye ushindani wa pamoja (competitive integrated market) katika dunia inayozidi kuwa ya kiushindani?

Pia tukumbuke, agizo hilo la Tanzania linaambatana na makosa ya kijinai (criminal offences). Raia wa kigeni atakayebainika kufanya biashara yoyote iliyopigwa marufuku atatozwa faini isiyopungua shilingi milioni 10 au atafungwa kwa kipindi cha hadi miezi sita. Aidha, Mtanzania yeyote atakayeshiriki au kushirikiana kwa namna yoyote na mgeni katika kuvunja amri hiyo, atakabiliwa na faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha hadi miezi mitatu.

Kwa kujibu hali hiyo, Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari imeitisha mashauriano ya dharura (emergency consultations). Kati ya mikutano iliyopangwa ni:​
  • Kikao cha kiufundi kuhusu biashara ya tumbaku (Technical Meeting on Tobacco Trade) kitakachofanyika Arusha, tarehe 4–5 Agosti 2025,​
  • Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Biashara (Joint Trade Committee) kuhusu ada, tozo na ushuru wa forodha, tarehe 11–12 Agosti 2025,​
  • Baraza la Pili la Sekta ya Fedha na Uchumi la Dharura (2nd Extraordinary Sectoral Council on Finance and Economic Affairs) litakalofanyika tarehe 30 Septemba 2025.​

Matokeo ya mikutano hiyo huenda yakaunda sura mpya ya mchakato wa ulinganifu wa kisheria na kiuchumi ndani ya EAC, lakini pia ni jaribio zuri la kutathmini mizani kati ya uhuru wa taifa (national sovereignty) na wajibu wa pamoja wa kimataifa (supranational obligations).

Kwa kumalizia, japokuwa agizo la Tanzania linaweza kutetewa kwa misingi ya maslai ya umma, uhalali wake kimataifa ni mdogo. Hali hii inaleta mjadala mkubwa wa kisera: Je, taifa linaweza kulinda uchumi wake wa ndani bila kuvunja mshikamano wa kimataifa? Na kama hilo haliwezekani, je, ni marekebisho gani yanapaswa kufanyika ndani ya mfumo wa EAC ili kuruhusu national flexibility?

Matarajio ni makubwa, si kwa Tanzania na Kenya pekee, bali kwa mustakabali wa ujumuishaji wa kiuchumi Afrika Mashariki.​

View attachment 3426132
View attachment 3426134
Kenya kuzungumza kuhusu EAC integration, ni UTAPELI na Juha tu anaweza kuumiza kichwa kuandika maneno 2000 insha kutetea huu ujinga.
 
Kusema ukweli serikali hawa jatenda haki kabisa, kwa sababu hata watz wapo wengi tu kwenye inchi za watu, wana tafuta maisha.

Mm naona kilicho pelekea kupitisha hiyo Sheria ni pressure ya uchaguzi tu ili wapate wapiga kura hakuna kingine.
Tanzania inahitaji MITAJI mikubwa, teknolojia na masoko kutoka nje na siyo MACHINGA.
 
Je haya mazuio yaliyowekwa majuzi yanazihusu biashara zetu za kidugu za kiasili za mipakani?
#Ufafanuzi tafadhali!
Screenshot_20250731-194542~2.jpg
 
Kusema ukweli serikali hawa jatenda haki kabisa, kwa sababu hata watz wapo wengi tu kwenye inchi za watu, wana tafuta maisha.

Mm naona kilicho pelekea kupitisha hiyo Sheria ni pressure ya uchaguzi tu ili wapate wapiga kura hakuna kingine.
Funga bakuli lako we nyang'au,hauoni Watanzania wanavyobanwa na wageni kwenye biashara tajwa?Mtaondoka tu mnataka hamtaki.
 
Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kutangaza kanuni mpya za leseni za biashara na kodi, Kenya imepinga hatua hizo ikizitaja kuwa za kibaguzi na tishio kwa mshikamano wa kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kenya kupitia Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu Sheria ya Fedha ya 2025 na marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, ambazo zimeweka ushuru wa bidhaa na tozo ya maendeleo ya viwanda kwa viwango vya asilimia 10 na 15.

Pia, Kenya imekosoa agizo jipya la Tanzania linalokataza raia wasio Watanzania kufanya biashara 15 zikiwemo huduma za miamala ya fedha kwa simu, matengenezo ya vifaa vya kielektroniki, saluni, utalii na umiliki wa viwanda vidogo.

Waziri wa Biashara wa Kenya, Lee Kinyanjui, amesema hatua hizo zinavunja makubaliano ya Soko la Pamoja la EAC ambayo yanataka raia wa nchi wanachama wasibaguliwe katika biashara.

“Agizo hili linafanya uwekezaji halali wa raia wa EAC kuonekana kama kosa la jinai na litadhuru uchumi wetu kwa pamoja,” amesema Kinyanjui. Ameitaka Tanzania kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kutatua suala hilo.

Kwa mujibu wa agizo hilo, mamlaka zinazotoa leseni hazitaruhusiwa kutoa au kurefusha leseni kwa raia wasio Watanzania wanaoendesha biashara hizo. Mtu atakayekaidi atatozwa faini ya angalau shilingi milioni 10 au kifungo cha miezi sita na anaweza kufutiwa viza.

Aidha, raia wa Tanzania watakaosaidia wageni kukiuka agizo hilo watatozwa shilingi milioni 5 au kufungwa miezi mitatu.

View attachment 3426106

View attachment 3426105
Kazi nzuri hii ya awamu ya 6
 
Tanzania ni nchi ya kipumbavu sana. Huwa wanafanya maamuzi bila kutumia akili. Kenya ni nchi makini sana, inaongozwa na viongozi wenye akili na wanaojitambua. Sijawahi kuona nchi makini kama Kenya na sijawahi kuona nchi ya kishetani kama Tanzania hapa Ulimwenguni.
 
MImi nilijua ni raia wa kigeni hasa wachina pale kariakoo imekuaje tena raia wote wa kigeni
 
Uamuzi sahihi, hatuwezi kuruhusu wageni waje wafanye umachinga.
 
Warundi wanapita pita majumbani kukopesha chupa za chai, wakongo wamerundikana eti waganga wa kienyeji na pia kuendesha utapeli, wakenya wanapora ardhi ili wazalishe nafaka.
Nchi lazima ilinde baadhi ya shughuli za kiuchumi za watu wake.
 
Watalipiza kisasi. Watanzania waliorundikana na Nairobi na maeneo mengine ya nchi, watafurushwa na biashara zao zitataifishwa.
Wameeundikana wanafanya nini? Hakuna wa kutaifisha chochote.

Wakenya ndio wengi kuliko Watanzania na wao ndio wanatutegemea.
 
Wameeundikana wanafanya nini? Hakuna wa kutaifisha chochote.

Wakenya ndio wengi kuliko Watanzania na wao ndio wanatutegemea.
Kwa hiyo Tanzania mmeanzisha huo utaratibu wa kikoloni kwa ajili ya kutukomoa wakenya au ni namna gani? Acheni ujinga yenu.
 
Kenya ni viherehere sana na wajuaji kupitiliza wasitake kutupanda kichwani. Hilo soko kwa watanzania tu halitoshi wageni watapata sehemu wapi? Labda wauze nje kama machinga wapange barabarani
 
Kusema ukweli serikali hawa jatenda haki kabisa, kwa sababu hata watz wapo wengi tu kwenye inchi za watu, wana tafuta maisha.

Mm naona kilicho pelekea kupitisha hiyo Sheria ni pressure ya uchaguzi tu ili wapate wapiga kura hakuna kingine.
Mkuu hizo biashara ndogo ndogo waachiwe wazawa,hajakatazwa mtu kuwekeza bongo ila wekeza kwenye ujasiriamali ama biashara za kiwango Cha kati na Cha juu.
 
Back
Top Bottom