Baada ya Tanzania kubania wageni kufanya biashara nchini, Kenya imejibu mapigo

Baada ya Tanzania kubania wageni kufanya biashara nchini, Kenya imejibu mapigo

Tanzania ni nchi ya kipumbavu sana. Huwa wanafanya maamuzi bila kutumia akili. Kenya ni nchi makini sana, inaongozwa na viongozi wenye akili na wanaojitambua. Sijawahi kuona nchi makini kama Kenya na sijawahi kuona nchi ya kishetani kama Tanzania hapa Ulimwenguni.
Wewe mbugila katazo ni la mataifa yote kwanini walalamike Kenya peke yake?
Mbona mataifa mengine hayajalalamika!?
 
kuna wale wanajifanya wapigania haki wa mombasa, niliwasikiliza jana wanasema, Tanzania haiwezi kusurvive bila kenya kwa sababu biashara ya MPESA halopesa na zingine za miamala, wafanyabiashara ni wakenya. ati mawakala wenu wa miamala hapa bongo ni wakenya? wakenay wako very ignorant about Tanzania na wanaamini hakuna kitu mtanzania anafanya chenye faida bila wao. kama kuna mtu anaamini miamala ya fedha Tanzania wanaofanya ni wakenya wakati mimi sijawahi kutoa mpesa, helopesa au yas, au nmb, crdb wakala etc kwenye kibanda cha mkenya, hao wakenya wapo wapi sasa?
 
Huu umoja wa kipumbavu uliowekwa na UK ni uvunjwe haraka sana hauna faida kwa TZ , bali ni viongozi wa jumuiya hiyo ndio wanalipana posho na mishahara kufuru , ili kuwanyamazisha wasipige kelele kinacho endelea huko EAC.

Tanzania hamkeni kataeni hii jumia ya EAC, kazi ya EAC ni kuipunguzia majukumu ya serikali kwenye maswala ya kiuchumi, kiulinzi , etc
 
Juzi, niliandika kuhusu agizo la Waziri Selemani Jafo linalowazuia raia wa kigeni kushiriki katika aina mbalimbali za biashara ndogondogo na za kati nchini Tanzania, amri ambayo imezua mapokezi yenye sura mbili: pongezi ndani ya nchi na tahadhari kali katika ngazi ya kimataifa.

SOMA: Waziri Jafo Awazuia Raia wa Kigeni Kufanya Baadhi ya Biashara Nchini.

Agizo hilo, linalojulikana rasmi kama The Business Licensing (Prohibition of Business Activities for Non-Citizens) Order, 2025, linaainisha aina 15 za shughuli za kibiashara ambazo kuanzia sasa hazitaruhusiwa kufanywa na raia wasio Watanzania, ikiwemo raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community – EAC).

Biashara hizo ni pamoja na huduma za uhamishaji wa pesa kwa simu (mobile money transfers), biashara ya rejareja (retail trading) isipokuwa maduka makubwa (supermarkets), karakana za kurekebisha vifaa vya kielektroniki (electronic repair shops), saluni, usafi wa mazingira (cleaning services), udalali wa mali isiyohamishika (real estate brokerage), huduma za utalii (tour guiding), pamoja na umiliki wa viwanda vidogo na vya kati (micro and small industries).

Kwa Watanzania wengi, hizi si biashara tu, bali ni njia za kiuchumi za kujikimu katika maisha yetu ya kila siku, hivyo hatua hii imepokelewa kama uamuzi wa muda mrefu uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu ili kulinda ujasiriamali wa ndani dhidi ya uingiliaji wa kibiashara wa wageni, hasa katika masoko ya mijini.

Hata hivyo, ushindi huu wa ndani umegeuka kwa haraka kuwa mgogoro wa kibiashara wa kimataifa kati ta Kenya na Tanzania.

Tarehe 30 Julai 2025, Serikali ya Kenya ilitoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari ikionesha wasiwasi mkubwa kuhusu agizo hilo la Tanzania. Kenya imesema kwamba hatua hiyo inakiuka Common Market Protocol (CMP) ya EAC, hasa Ibara ya 13 inayotoa haki kwa raia wa EAC kuanzisha na kuendesha biashara katika nchi wanachama kwa misingi ya usawa na bila ubaguzi wa uraia (non-discrimination).

Soma Pia: Aina za biashara zilizopigwa marufuku kwa wageni wasio raia

Kenya imeeleza kwamba, pamoja na kutambua na kuheshimu mamlaka kamili ya nchi wanachama wa EAC katika kutunga sheria na sera za ndani, hatua zenye athari kimataifa zinapaswa kuchukuliwa kwa kuzingatia mashauriano (consultation), uwazi (transparency) na uratibu wa pamoja (regional coordination), misingi ambayo ndiyo kiini cha mchakato mzima wa ujumuishaji wa kimataifa (regional integration).

Kwa mtazamo wa Kenya, agizo la Tanzania ni mabadiliko ya sera ya upande mmoja (unilateral) yanayoweza kuhatarisha mafanikio yaliyopatikana katika uhuru wa kusafirisha bidhaa, huduma, na watu ndani ya ukanda wa EAC.

Kwa maoni yangu, mgogoro huu unaweza kuwa na athari mbili kuu: za kisheria (legal implications) na kiuchumi (economic implications).

Kwa upande wa sheria, Tanzania italazimika kuonesha kwamba hatua yake inefikiwa kwa maslahi ya umma (public interests) lakini pia ithibitishe wajibu wake wa kimikataba (treaty obligations) chini ya makubaliano ya EAC.

Kiuchumi, swali linabaki: Je, hatua hii ya kujilinda kiuchumi (protectionist posture) ni msaada au ni kikwazo kwa sera ya EAC ya kuwa soko lenye ushindani wa pamoja (competitive integrated market) katika dunia inayozidi kuwa ya kiushindani?

Pia tukumbuke, agizo hilo la Tanzania linaambatana na makosa ya kijinai (criminal offences). Raia wa kigeni atakayebainika kufanya biashara yoyote iliyopigwa marufuku atatozwa faini isiyopungua shilingi milioni 10 au atafungwa kwa kipindi cha hadi miezi sita. Aidha, Mtanzania yeyote atakayeshiriki au kushirikiana kwa namna yoyote na mgeni katika kuvunja amri hiyo, atakabiliwa na faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha hadi miezi mitatu.

Kwa kujibu hali hiyo, Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari imeitisha mashauriano ya dharura (emergency consultations). Kati ya mikutano iliyopangwa ni:​
  • Kikao cha kiufundi kuhusu biashara ya tumbaku (Technical Meeting on Tobacco Trade) kitakachofanyika Arusha, tarehe 4–5 Agosti 2025,​
  • Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Biashara (Joint Trade Committee) kuhusu ada, tozo na ushuru wa forodha, tarehe 11–12 Agosti 2025,​
  • Baraza la Pili la Sekta ya Fedha na Uchumi la Dharura (2nd Extraordinary Sectoral Council on Finance and Economic Affairs) litakalofanyika tarehe 30 Septemba 2025.​

Matokeo ya mikutano hiyo huenda yakaunda sura mpya ya mchakato wa ulinganifu wa kisheria na kiuchumi ndani ya EAC, lakini pia ni jaribio zuri la kutathmini mizani kati ya uhuru wa taifa (national sovereignty) na wajibu wa pamoja wa kimataifa (supranational obligations).

Kwa kumalizia, japokuwa agizo la Tanzania linaweza kutetewa kwa misingi ya maslai ya umma, uhalali wake kimataifa ni mdogo. Hali hii inaleta mjadala mkubwa wa kisera: Je, taifa linaweza kulinda uchumi wake wa ndani bila kuvunja mshikamano wa kimataifa? Na kama hilo haliwezekani, je, ni marekebisho gani yanapaswa kufanyika ndani ya mfumo wa EAC ili kuruhusu national flexibility?

Matarajio ni makubwa, si kwa Tanzania na Kenya pekee, bali kwa mustakabali wa ujumuishaji wa kiuchumi Afrika Mashariki.​

View attachment 3426132
View attachment 3426134
Kwa nini hatua ya consultation isingeanza kwanza?
 
Yametolewa maamuzi bila kufanya utafiti na uchunguzi wa kina,
VITA KUBWA VYA KARIAKOO NI DHIDI YA WACHINA NA SI JAMII ZA EAST AFRIKA,SHIDA UAMUZI UMETOLEWA WA KIJUMLA JUMLA BILA KUONA KUNA WASWAHILI WENZETU WALALA HOI TU.
 
Yametolewa maamuzi bila kufanya utafiti na uchunguzi wa kina,
VITA KUBWA VYA KARIAKOO NI DHIDI YA WACHINA NA SI JAMII ZA EAST AFRIKA,SHIDA UAMUZI UMETOLEWA WA KIJUMLA JUMLA BILA KUONA KUNA WASWAHILI WENZETU WALALA HOI TU.
Sheria inasema Non Citizens, haijataja Wakenya.

Mwisho wa siku biashara ndogo hazilipi kodi, hatutaki machinga
 
Kusema ukweli serikali hawa jatenda haki kabisa, kwa sababu hata watz wapo wengi tu kwenye inchi za watu, wana tafuta maisha.

Mm naona kilicho pelekea kupitisha hiyo Sheria ni pressure ya uchaguzi tu ili wapate wapiga kura hakuna kingine.
Ccm hawana pressure yoyote sema mawaziri wa kenya wanatafuta cheap popularity
 
Kumbe wewe ni mkenya? Rudi kwenu hakuna kufanyabiashara za kimachinga hapa TZ. Ndio maana unatoa mapovu sana.
Biashara ni huduma. Naitoa kwa manufaa ya waTZ. Taabu ni nini?
 
Wewe mbugila katazo ni la mataifa yote kwanini walalamike Kenya peke yake?
Mbona mataifa mengine hayajalalamika!?
Mataifa mengine hayajitambui. Wewe kinakuuma nini?
 
Upuuzi mkubwa huu SI tunalia na wachina we UNAENDA piga marufuku WA Kenya. Madhara ni makubwa SHIDA ya KUWEKA WATU wasio na sifa NDO hii. HIVI hatuja jifunza yaliyo tokea afrika kusini KUHUSU vita na wageni KWENYE BIASHARA HIVI gen z Wakilii anzisha watanzania wenzetu wataponea wapi?



Kwishaaaaa
 
Back
Top Bottom