Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Kwahiyo we Pascal huelewi kuwa Kabendera kaachiwa kwa sababu ya shinikizo la Mabeberu na hiyo faini Ni geresha tu kuda ganyia wajinga.Maana Jiwe mpaka sasa yuko kwenye kumi na nane za mabeberu.
 
Ule uzi sikuutia maanani tangu siku ya kwanza mleta mada alivyoanza kwa kudai eti Pascal alisababisha Usalama wafatilie chapisho la The Economist. Mimi nilisoma hilo chapisho kabla halijawekwa hapa tena nililisoma kiuzembe tu sikulitia maanani. Pascal ni mwandishi wa habari, ana tabia ya kuchambua taarifa na matukio fulani akaleta chapisho akalifafanua na kulipinga. Nikaja kuona kumbe sikustahili kulipuuza nikaacha wanasiasa ws JF waumane.

Sasa mtu akija na hoja eti P alimchomea Kabendera, kivipi sasa mbona akili yangu ndogo haielewi. Kwamba Pascal anaujua mwandiko wa Kabendera, au aliambiwa na mtuhumiwa kuhusu deal hiyo. Najaribu kutafuta ilikuwaje Kabendera ajulikane kwa P kuwa ndiye mwandishi sioni njia. Kwamba Usalama walihangaika kumjua wakaomba msaada kwa Pascal? Alijuaje sasa, na factors zipi zilimfanya kati ya mamia ya waandishi amtambue mhusika.

Na inakuwaje Kabendera alishindwa kuwa anonymous kwenye kazi yake ya hatari mpaka akamfanya Pascal ajue, hapa tuassume ni kweli Kabendera ndiye aliyeandika. Kazi ya hatari unamwambiaje mwenzio? Siamini katika hili.

Mimi napenda watu wachangie kile wanachojua. Akija mtu akafanya upembuzi na kuleta bandiko then likatokea la kutokea tuseme kachoma. Sio sawa.
 
Wanabodi,

Kwa vile sisi binadamu tuna uwezo tofauti, na sio watu wengi wanajitambua uwezo wao katika kitu kinachitwa "self realization", ikitokea unajitambua, na unapokasirika kwa kutotendewa haki, kwa kutwishwa misalaba ambayo sio yako, na ukiumia na kulaani watesi wako, na unajua nini kitawatokea pale Mungu anapoamua kukutua msalaba huo, then sauti ya Mungu inakuingia, na hapo hapo unakumbuka na kuwasamehe watesi wako, kabla karma haijaanza kuwafanyia kazi.

Baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera kukamatwa na polisi na kushikiliwa mahabusu kwa miezi 7, msalaba wa kukamatwa nilibebeshwa mimi. Eti ni mimi Pascal Mayalla ndiye niliyesababisha kukamatwa kwa Erick Kabendera, kwasababu ya zile makala zangu za uzalendo humu JF.
Hizi ni Baadhi ya Makala Zangu Kuhusu Uzalendo, wale wenye muda, pitieni halafu mnieleze wapi nimemponza mtu yoyote?


Japo nilijifanya mgumu na sijali, kwasababu kiukweli kabisa, makala zile wakati zinaandikwa hazikuwa na lengo la kumchomea mtu yoyote, popote, na wala sikuwahi kuwafahamu waandishi wa makala hizo. Na mpaka sasa ninapoandika leo, bado siwafahamu waandishi wowote wa makala hizo, lakini kwa upande mwingine, kwa vile kuna mwandishi wa habari, Erick Kabendera, amekamatwa katika mazingira ya kutatatisha. Baada ya askari waliotumwa kumkamata kukataa kujitambulisha, hivyo kudhaniwa ni wasiojulikana na Erick akawagomea kuwafungulia, ndipo wakamfanyia utekaji kwanza; kwa kutekwa na kufichwa kusikojulikana kwa muda siku mbili za mwanzo, huku serikali wakitupiana mpira, mara ni polisi, mara ni immigration, na kosa lake mara ni uraia ila full kujiuma uma!.

Ila baada ya kufikishwa mahakamani ndipo kukaibuka uhujumu, utakatishaji fedha na magenge ya uhalifu. No one was sure axactly what is it, hivyo any reasonable man lazima ujiulize, "what if ni kweli mwandishi ni yeye?", "what if ni kweli zile makala zangu ndizo zimeiamsha serikali na kuichochea kumtafuta anayeandika?", "what if ni kweli mwanzo alitumiwa wasiojulikana ili wampoteze kama Azory Gwanda na Ben Saanane lakini baada ya Erick kuunguza picha, ndipo ikashindikana, na kuamua kumtafutia mashitaka yoyote ya kumbambikia just to silence him? Then japo nilikuwa najikaza kisabuni, lakini automatically nilianza kujihisi, na kila siku Erick alipokuwa akifikishwa mahakamani naumia, "what if sababu ni mimi?".

Kila uzi wowote kumhusu Erick Kabendera ukipandishwa humu JF lazima humo ndani ya uzi, lazima nilikuwa natajwa as a "snitch". Kila mateso aliyokuwa anakutana nayo Erick Kabendera, na mimi yalikuwa yananiumiza psychologically. Kwanza nikawa sichangii uzi wowote kuhusu jambo lolote kwa Erick Kabendera.

Mimi ni story teller, kwa wapenda nyuzi fupi, ishieni hapa, na kwenda kule kwenye hitimisho, wapenda mastory ya JF, tuendelee hapa

Sisi Wakristu wa kweli, tunaofuata mafundisho ya Mungu wa Kweli, na kufuata mafunzo ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Kweli, tumefundishwa kusameme hata saba mara sabini, hivyo mimi kwa upande wangu, niliisha kusamehe toka siku ile ya kwanza ulipopandisha bandiko hili kwa kulipuuza, kwasababu ulikuwa hujui utendalo. Pia nimewasamehe wale wote walionituhumu ni mimi kwa kuamini kuwa kweli ni mimi.

Hitimisho:
Hivyo kwa uzi huu, baada ya ukweli wa mashitaka ya Erick Kabendera kubainika, mimi nimewasamehe "Wale Wote walionituhumu mimi kuhusika na kukamatwa kwa Erick Kabendera, na kufuatia msamaha huo, pia "Mungu nae, amewasamehe" Hakuna tena adhabu ya karma kwenye kunisingizia mimi issue ya Kabendera, ila tafadhalini sana, msirudie tena kumtuhumu mtu mwingine yoyote kwa tuhuma ambazo hamna hakina nazo! Kauli huwa zinaumba, sisi wengine tunajijua kauli zetu na madhara yake, hivyo mkituudhi tusiposamehe.


Hivyo kwa upande wangu, uwe na amani kabisa, na wote mlionituhumu humu na kungine kote, muwe na amani, nimekusamahe na kuwasamehe wengine wote kwa roho safi na roho nyeupe, lakini ili karma isikushughulikie na wewe kwa upande wako, baada ya kuujua ukweli huu, do the right thing, hata kimoyo moyo tu, inatosha Mungu anasikia kila kitu hata usipozungumza, ile kuwaza tuu, is enough!

Ubarikiwe sana.

Paskali.
Ukweli ni nini na unaujuaje huu ni ukweli na huu si ukweli?
 
Wewe mshamba sana tena sana kuwadi wa shetani.Unadhani kwa nini kuna cyber crime.Aliyoyaandika kabendera kupitia The economist ninkweli tupu.Hayo ya kumchoma kupitia maandishi ni kawaida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Pascal ametoa maoni watu wakaona yana tija wakayatumia sasa kosa lake nini?

Erick akiandika wazungu wakayatumia ni sawa

Pascal akiandika serikali yetu ikayatumia ni kosa

Ujinga mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo kwa uzi huu, baada ya ukweli wa mashitaka ya Erick Kabendera kubainika
Una uhakika 100% ule ndio ukweli kuhusu Kabendera??
Hauna shaka yoyote kwamba ameamua kukubali tuu yaishe ili awe HURU?

Swala la wewe kuwa mchongeaji wake kusema kweli SIJUI kama unahusika.
Ila kutumia yale yaliyotekea mahakamani kujitetea bado sijakuelewa mkuu
 
Erick Kabendera kwa yaliolezwa ni kweli alipata tuhuma za kutakatisha fedha. Fedha bilion moja kuingia na kutoka kwenye account za kampuni under Anti Money Laundering law alikuwa mtuhumiwa na hatimaye kakiri makosa ikiwemo la kukwepa kulipa kodi ya kipato.

Tuache ramli chonganishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tazama kichwamaji hiki kinachoamini kumuita mtu kaka au dada ni hadi uwe na uhusiano naye. Kwa taarifa yako, Pascal Mayalla namfahamu tangu nilipokuwa Sekondari na kiongozi wa TYCS akiwa anatoa mada pale Don Bosco. Ni kaka yangu kwakuwa simpati kiumri na nalifahamu hilo. Jitahidi kula samaki na dagaa kuchangamsha akili zako.
Teh teh teh teh,,,halinaga akili hilo gudulia! Eti lile samaki labda litapata akili!! Mavi-jana ya ccm hayanaga akili!
 
Kwahiyo we Pascal huelewi kuwa Kabendera kaachiwa kwa sababu ya shinikizo la Mabeberu na hiyo faini Ni geresha tu kuda ganyia wajinga.Maana Jiwe mpaka sasa yuko kwenye kumi na nane za mabeberu.
Paschal ana j ya ukweli wote sema kwakuwa ameamua.kujiunga na wasukuma mwenziwe wa awamu ya tano bado anapigania uteuzi, huenda atakumbukwa hivi karibuni
 
Kwani angekaakimya nani angemjibu. Alafu kwanini kuandika Uzi mreeeeefu, na ma reference lukuki yanini.

Vitabu vya dini vinasema majibuyenu yawe ndio, ndio, na sio,sio.
Hakuna haja ya kuandika maelezo meeeeengi,hayata saidia.
Nibora kukaa kimya alafu ukweli nauongo vitajickekecha vyenyewe kadiri muda unavyo kwenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ishara wazi kuwa aliyoyatenda yanautesa moyo wake.Ni sawa kama wanavyoumia waliomtenda Lissu.Ukimtendea mwenzako mabaya lazima na wewe mwenyewe yatakuumiza kila unapokumbuka na hasa kama malengo yako hayakutimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.

Kutokumuheshim pascal hakuwezi kumfanya asile wala apungukiwe kitu, ataendelea na shughuli zake kama kawaida, ingekuwa bora ukatwambia wakati unamheshimu alinufaika kiasi gani na heshima yako kiasi ukiiondoa atapata shida?
 
Watanzania mna vichwa vibovu Sana , Una ushahidi gan anahusika....?? Ifikie hatua kila mmoja apambane na Hali yake na sio kujibanza kwa mtu

Well said mkuu Slowly.

Pascal, pole sana kwa haya yote. Jamii yetu inapaswa ijifunze kuepuka kukumbatia speculations na notions zinazotokana na 'hearsay'. Tunachokifanya hapa ni kutengeneza "msiba juu ya msiba". Watanzania we are good at that! Let's learn to deal with facts instead of hearsays. Speculations huwa zinaua! Depressions, mental illnesses na suicidal dispositions mara nyingi husababishwa na vitu kama hivi, na ndiyo maana maradhi kama haya katika nchi zetu yako rampant.

Suala la EK linatia huruma. Sina hakika kama Eric ameonewa au la kutokana na jinsi kesi yake ilivyokuwa politicised, hivyo sitaliongelea sana suala lake hapa mpaka pale mambo yote yatakapowekwa wazi. Hata hivyo, ukweli kwamba Eric ameteseka, haukwepeki. Lakini pia jamii haikupaswa kumhukumu Pascal Mayalla bila ithibati thabiti - au kile tunachokiita "prima facie" - huku ikimmiminia shutuma kenyekenye, badala ya kuzielekeza shutuma hizo kule zinakotakiwa: kwa watesi wa Eric. Huku ni kuhamisha magoli. Why are we avoiding the real antagonist of the protagonist in this infamous theatrical play?!

Hili jambo linadhikisha sana. Kinachotokea hapa hakina tofauti na kilichotokea Shinyanga na Mwanza mwaka 1976, wazee wetu kina Mabula Mazegenuka, kina Ng'wana Ng'hoboko, na wengine wengi, wakiwemo waganga wa jadi, wafanyabiashara na wakulima, waliposhutumiwa kuua vikongwe "wachawi" na hivyo - bila hata "prima facie" - nao wakauawa, na kwa jinsi hiyo, jamii ikajikuta ikitengeneza "msiba juu ya msiba", katika tukio lililosababisha kuundwa kwa katiba mpya ya 1977, na kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ndugu Ali Hassan Mwinyi. Yote haya kwa sababu ya kitu kimoja: speculations.

Speculations, hearsays, na vitu kama hivyo, huwa si vitu vizuri muda wote, na aghalabu huwa havijengi. Tujifunze! We are better than this.
 
Ulipokuwa unaandika lengo lilikuwa ni nn? Bw pskal

Tuanzie hapo,
Lengo lako lilikuwa kuleta uelewa wa taarifa au ubatili wa taarifa?

Kwa sasa paskal umekataa kutuacha tufanye uchambuz wenyewe wa taarifa zako juu ya right and wrong

Sasa umeegemea kwenye ubatili wa kila taarifa inayomhusu rais, ikulu hata serikali na ni hapo ndipo tunakuita wewe ni snitch

Umetusaliti sote humu jf kabla hujajifunua na baada ya kujifunua ulikuwa vizur ila 2019 duh


Lkn huwa naitafari sana kauli " remember you have a family to feef not a community to empress"

Lkn mkeo na watoto wako marekani wanagreen gurd kwa nn usiwe sehemu sympathazition ya nchi !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipanya huyo
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
NI ajabu kutangaza msamaha kwa watu ambao wewe ndo wanatatikwa kukusamehe. Dunia hapa tunapita tu tutafuteni ridhiki kwa halali so kwa kujipendekeza na kuwachomea wenziyo waharibikiwe wewe upate kula. Ukweli anaujua kabendera na Mwendesha mashitaka. Mambo mbuvu mbovu ya mtu kujitokeza na kusema ukweli umejuilikana, kuna ukweli gani hapo zaidi ya kuatangaziwa mtu mmoja kakubari kulipa kwa awamu. unahakika hizo hela zitalipwa na mkubariji, acheni unafiki kama ipo ipo tu!, nyoo!, eti ukweli!. Mwalimu Nyerere hakuwa Mjinga kupigania self reliance.
 
Back
Top Bottom