Tetesi: Baada ya upepo wa Mahakama kuwakalia vibaya: Lipumba, Sakaya na Kambaya kuhamia CCM muda wowote

Hii ni taarifa niliyodokezwa na mdau mmoja ambaye ni mhusika kwenye 'kitengo cha manunuzi' CCM.

Lipumba na timu yake wamelazimishwa kuhakikisha wanahamia rasmi CCM kabla ya January.

Maulid Mtulia ametangulizwa makusudi ili kupima upepo, hasa baada ya ushahidi kuonyesha wazi kwamba wataangukia pua mahakamani, wameona ni heri lawama kuliko fedheha.

Tuendelee kusubiri, kila msaliti atajianika mwenyewe

Mungu hajawahi kumficha mnafiki .
Kumbe mtulia alikuwa kambi lipumba!!!!!
 
Acha wanasiasa wafaidi keki ya taifa. wengine tujifunze uvumilivu
 
hivi vita sefu anashinda wanataka kumuwahi kabla hajahama yeye kwenda chadema na kumuacha lipumba mtupu
 
Sisi wapuuzi sana, kama ni kweli yanayosemwa humu ndani Kuwa wanasiasa wananunuliwa basi tusianzidhe wala kulaumu yanayoendelea huko Libya.

Tuende Kilwa, Bagamoyo, Tanga tukafungue upya Masoko yetu na sisi tuanze kufanya.
 
Kuna nyepesi zinazunguka kumhusu Magdalena Sakaya, kwamba anaitosa CUF na kuhamia CCM muda wowote kuanzia sasa. Mwaka huu tutasikia na kuona mengi.
Magdalena Sakaya tulishamwambia Machoni ni cuf ila Rohoni ni chama changu kilichoondoka na lile zao la kahawa lililomsomesha pale Kombo mpaka Kibosho Girls.
Lakini najua Mama yangu Mambonge na Mzee Costa Hamis Sakaya sio chama changu tena hata mbuge mwenzake Komu na Diwani Deo Massawe ana lijua hilo .
Hizi Siasa za komokomoa najua Magdalena hajaziona leo kwa hiyo kushiriki kumhukumu kwa maslahi ya muda ni laana ambayo inaishi kwa vizazi vingi mpaka atakayekumbuka kuvunja ndo inapatikana pona yake. Seif aliipigania cuf mpaka ikafika hapo ilipo kwa hiyo historia hujirudia kwa uzuri au kwa ubaya
 
Sisi wapuuzi sana, kama ni kweli yanayosemwa humu ndani Kuwa wanasiasa wananunuliwa basi tusianzidhe wala kulaumu yanayoendelea huko Libya.

Tuende Kilwa, Bagamoyo, Tanga tukafungue upya Masoko yetu na sisi tuanze kufanya.
Hakuna tofauti yoyote kati ya yanayotendwa na ccm na biashara ya utumwa , hiyo yote ni biashara ya binadamu
 
Hivi biashara hii si imelaaniwa alafu watu wanaifanya. Basi huku yao inakuja kutoka kwa Wananchi walioipata Elimu ya Uraia
 
Hii ni taarifa niliyodokezwa na mdau mmoja ambaye ni mhusika kwenye 'kitengo cha manunuzi' CCM.

Lipumba na timu yake wamelazimishwa kuhakikisha wanahamia rasmi CCM kabla ya January.

Maulid Mtulia ametangulizwa makusudi ili kupima upepo, hasa baada ya ushahidi kuonyesha wazi kwamba wataangukia pua mahakamani, wameona ni heri lawama kuliko fedheha.

Tuendelee kusubiri, kila msaliti atajianika mwenyewe

Mungu hajawahi kumficha mnafiki .
Maalim seif atapumua
 
Hakuna mwanaccm mcha Mungu .
Mbona mm nina hofu ya Mungu tena kubwa tuu ndo maana sipepesi macho ktk kusimamia kweli ili kweli iniweke huru. Bila kuwa huru huwezi kuja na hoja ikawa na mashiko ndo maana watu hukimbia hoja zao
 
Labda si mwanaccm .
 
Hao washanunuliwaga kisha wakaachwa hapo kwa mkopo
 
Back
Top Bottom