Baada ya vifo vya Said Oswayo na mkewe, Swalha Salum mali zinatakiwa kwenda katika Familia ya Mke au Mume?

Baada ya vifo vya Said Oswayo na mkewe, Swalha Salum mali zinatakiwa kwenda katika Familia ya Mke au Mume?

Uwezekano wa kuwa kuna mali imepatikana ndani ya muda huo wa miezi 5 ya ndoa yao ni mdogo sana ingawa inawezekana.

Ndugu wa mke kuweni wapole mtoto wa marehem achukue mali za baba ake. Kama kuna chochote chenye jina la mke mtapewa
Wanataka kumdhulumu mtoto wa marehemu ambaye hiyo nyumba aliijenga akiwa na mama wa huyo mtoto
 
Marehemu enzi za uwai wake pia alikuwakicheche
IMG-20220601-WA0002.jpg
 
Maregemu Mwanamke atachukuaje mali?

Labda kama angekuwa hai na mwanaume angekuwa amefariki sababu huyo mwamamke amefariki hajazaa na Marehemu.
 
Mi tangia mwanzo nilikuwa nawaza mashemeji kujazana nyumbani ndoa haina hata miezi sita, ndomana mimba haingii, itaingiaje mmejazana ndani ya nyumba ya wanandoa wapya [emoji1787]
Ni tabia mbaya kujaza ndg nyumbani
 
Kwa dini ya kiislamu, madamu mwanamke amekufa kwanza nusu ya mali yake (binafsi) itakwenda kwa mume (hakuna watoto), robo kwa wazazi na nyingine ndiyo kwa warithi wengine.

Iliyobaki itakwenda kwa akina kaka zake.

Kwa kawaida sisi waislamu na hasa wa pwani huwa hatuchanganyi mali na mume, kila mmoja anakuwa na mali kwa jina lake, mfano nyumba, shamba, gari.
 
Ndio maana Uislamu unapenda sana kila mtu kujiandikia wosia wake pindi alalapo tena anatakiwa huo wosia alale nao chini ya mto ama chini ya godoro....Mambo kama haya ndio yanaleta changamoto sana kwa jamii,Ila yote kwa yote haki ya kila mrithi itapatikana haki yake ikiwa wakiitumia Quraan kama muongozo wao
 
Hiyo familia ya mwanamke hizo akili sjui wamezipata wapi za kung'ang'ania mali ambazo sio zao,na huyo ng'ombe wao hakufanikiwa kuzaa
 
Mi tangia mwanzo nilikuwa nawaza mashemeji kujazana nyumbani ndoa haina hata miezi sita, ndomana mimba haingii, itaingiaje mmejazana ndani ya nyumba ya wanandoa wapya [emoji1787]
Halaf mashemej wazur,ningekuwa said ningekula wote mmoja baada ya mwingine
 
NATAKA NISEME KIDOGO.
HAPA KUNA MASUALA MENGI YA KUZINGATIA.
1, YALITOKEA MAUAJI KWANZA
KATIKA QURAN SURATUL NISAA
'Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. (92) Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.'

KWA HIVYO SAID (ALIYEFARIKI),
MOJA KATIKA ALIYOTAKIWA KUFANYA NI , ALITAKIWA KULIPA FIDIA KWA FAMILIA YA MWANAMKE KAMA ALIMUUA SIO KWA KUSUDI, ILA IKIWA FAMILIA YA MWANAMKE IMESAMEHE HAMNA NENO.

2. SAID (ALIYEFARIKI) JEE WATOTO WALIOWAZAA ALIWAZAA NJE YA NDOA , AU ALIWAPATA WAKATI AMESHAOA? IKIWA ALIWAPATA BAADA AMESHAOA WANA FUNGU LAO, IKIWA ALIWAPATA KABLA YA KUOA HAWANA KITU HAPO.

3. IKIWA KUNA WATOTO WA NDOA, MKE ATAPATA CHAKE 1/8 AMBACHO KITAKWENDA KWA FAMILIA YAKE, LA IKIWA HAKUNA WATOTO WA NDOA MKE ATAPATA CHAKE 1/4.

4. MALI ZOTE AMBAZO SAID ( ALIEFARIKI) ALIMUANDIKIA MKEWE HIZO ZOTE HAZITOINGIA KWENYE MIRATHI.
MALI AMBAZO SAID AMEACHA WASIA APEWE MKEWE, HAITOWEZEKANA KUPEWA KWA SABABU KILA MWENYE KURITHIWA HAACHIWI URITHI.
KWENYE UISLAM SHERIA ZOTE ZIMEWEKWA HAZIFUATWI SHERIA ZA TWAAHUUTW.
Tanzania ya Leo ina katiba na sheria vinavyosimamia usawa wa watoto na haki zao.Ikitumika sheria ya kidini kuwanyima urithi watoto shauri likienda mahakamani watoto watapata urithi.
 
Tukio la Said Oswayo kumuua mkewe, Swalha Salum kisha na yeye kuuawa ikidaiwa amejiua bado ni gumzo Nchini Tanzania.

Wivu wa mapenzi ndio unatajwa na wengi kuhusu matukio hayo yaliyotokea ndani ya mwezi huu Mei 2022, lakini hoja yangu hapa siyo kuhusu walivyouawa, nina kitu tofauti kabisa.

Tayari kumeanza kelele kuhusu urithi wa mali, upande wa mwanamke inadaiwa wanaamini wao wana haki ya msingi, wakati huo ndugu wa mume nao wameanza kuonesha ishara kuwa wanataka kuwa sehemu ya mali hizo.

Marehemu walifunga ndoa Desemba 2021, ikiwa na maana kuwa ndoa yao ilikuwa na miezi mitano tu lakini mwanaume alikuwa vizuri kiuchumi na wadau wengi wa Mwanza wanaamini hicho ndicho kilichompeleka kwa mwanaume huyo, inasemekana lakini, hatuwezi kuusemea moyo wa mtu.

Inadaiwa mwanaume ana mtoto ambaye alimpata kabla hajamuoa huyo bibie.

Nimezungumza na wataalam wawili wa sheria na haya ndio yalikuwa maelezo yao:

MDAU WA KWANZA WA SHERIA:
Cha kwanza kabisa itaangalia kama marehemu aliacha wosia ambao unaweza kutaja mgawanyo wa mali zake na mengine yote.

Kama hakuna wosia, na wawili hao hawakuwa wamefanikiwa kupata mtoto, hapo mrithi halali ni mtoto wa huyo mwanaume hata kama alimpata nje ya ndoa.

Kinachotakiwa kufanyika ni kikao cha familia ambacho kitamchagua msimamii wa mirathi. Kama mtoto ana miaka chini ya 18 basi huyo msimamizi wa mirathi atatakiwa kusimamia mali za marehemu hadi mtoto atakapofikisha miaka 18.

Lakini kabla ya kufika huko msimamizi wa mali akishateuliwa na familia, anatakiwa kwenda Mahakamani kuapa, baada ya hapo ndani ya siku 14 atatakiwa kutafuta mali zote za marehemu ziwe kwenye orodha yake na zijulikane.

Nikirudi nyuma kama hivyo wawili hao hawakuwa na mtoto, kwenye urithi kawaida sheria inasema mtoto au watoto wanatakiwa kupata 80%, wazazi wa mume 10% na wazazi wa mke ni 10%

Mtoto akifikisha miaka 18 anatakiwa kwenda Mahakamani kuapa kuwa ametimiza umri huo na yuko tayari kuchukua mali kutoka kwa msimamizi na kuziendesha mwenyewe, au anaweza kuandika barua ya kutaka msimamizi aendelee kusimamia kwa muda atakaopendekeza yeye.

MDAU WA PILI WA SHERIA
Hapo baada ya taratibu za vikao vya familia na kumteua msimamizi wa mirathi, mali zote zitakuwa mali ya mtoto au watoto, kama hawana basi mali zitaenda kwa wazazi wa mwanaume.

Hiyo itafanyika kama marehemu hakuacha urithi wowote, mfano hao wanandoa (Swalha na Said) ndoa yao ilikuwa changa, hawakuwa na mtoto, hapo mwenye haki ya mali ni mtoto.

Mali ambazo walizipata ndani ya ndoa hizo wanaweza kugawana na upande wa mwanamke, mfano nimeona familia ya mwanamke inataka kung’ang’ania nyumba, ile siyo mali yao, labda kama wakati wanajenga walikuwa pamoja na nyaraka zipo wakati wa ujenzi kuwa mwanamke alishiriki.

Pia mali ambazo zitakuwa na jina la mwanamke pia zinaweza kuchukuliwa na upande wa familia ya mwanamke

HITIMISHO
Baada ya wadau hao, kuna yeyote ambaye anaona kisheria imekaaje kuhusu mali za marehemu Said? Kwani najua mgogoro mkubwa utaibuka muda si mrefu.... Mwenye uelewa atuelezee
👀👀
 
Kifupi walifunga ndoa ya Bakwata ambayo hamrithishi mwamamke mali. Hivo pointi ya msingi ni moja tu wosia na warangi lazima wafoji ndo maana hawataki kufungua nyumba.

Aisee...! haya yote nyie mnayotoa wapi ..?
 
Hiyo familia ya mke Njaa Tu! Inachotafuta itakipata...
 
Aisee...! haya yote nyie mnayotoa wapi ..?
Kwani mkuu umewahi kuona mwanamke wa akiisilam akiachika anachukuwa nini zaidi ya mahari aliyotolewa na ambayo huwa ni kabati, kitanda au masofa? kifupi hii familia ya mwanamke ni wanga na Malimbukeni, simjui Saidi ila alikosea njia. miezi mitano ya ndoa tayari mwanamke ameleta wadogo zake watatu kwake, wakike wawili wa kiume mmoja, tayari wote wamejifunza gari kupitia Gari za shemeji. Usiku eti wamekuja kitu kimefungwa kama Sanda na usiku huo huo mke wa Saidi kampigia babake simu na babake kaleta waganga, lakini kama haitoshi mwanamke kapiga picha hicho kitu na kapost instagram, Swali kama kuna kitu kama hicho kilionekana usiku huo kwanini hawakujipa muda wa kutafakari? kwa nini ilikuwa rahisi sana kwa baba kuwapata uganga usiku huo huo? Kwa nini baada ya hilo tukio Saidi ajisikie kuumwa na kumpigia mamake simu lakini akimzuia asiende mwanza? mwanamke mwenye nidhamu mme kampa taarifa anarudi na njaa lakini yeye kaenda kudanga tena na gari ya mme, marafiki wanampigia simu gari yako iko hotel fulani mme anapiga simu 42 mke hapokei, Kwanini siku hiyo mdogo mtu agome kwenda kulala kwa Saidi mahali ambapo alikuwa akiishi siku zote? Tafakari chukuwa hatua
 
Mali za mume zende kwa familia ya mume, Mali za Mke zende kwa familia ya mke. Mali ya pamoja igawanywe kila upande. Kesi imeisha.
 
Tanzania ya Leo ina katiba na sheria vinavyosimamia usawa wa watoto na haki zao.Ikitumika sheria ya kidini kuwanyima urithi watoto shauri likienda mahakamani watoto watapata urithi.
Sheria za nchi zipo za aina 3 zinazotambulika na Mahakama ambazo ni sheria za kimila,kiislamu na ya India ambayo tulikopi huko.Hivyo Mahakama itaamua Mwanaume alifunga ndoa ya aina ipi.Kama ni ya kimila basi watafuata mila za kwao mwanaume zinasemaje.Sheria inayoisema wewe hiyo ni ile tuliyokopi ya INDIA,nimesahau kidogo inaitwaje
 
Kwani mkuu umewahi kuona mwanamke wa akiisilam akiachika anachukuwa nini zaidi ya mahari aliyotolewa na ambayo huwa ni kabati, kitanda au masofa? kifupi hii familia ya mwanamke ni wanga na Malimbukeni, simjui Saidi ila alikosea njia. miezi mitano ya ndoa tayari mwanamke ameleta wadogo zake watatu kwake, wakike wawili wa kiume mmoja, tayari wote wamejifunza gari kupitia Gari za shemeji. Usiku eti wamekuja kitu kimefungwa kama Sanda na usiku huo huo mke wa Saidi kampigia babake simu na babake kaleta waganga, lakini kama haitoshi mwanamke kapiga picha hicho kitu na kapost instagram, Swali kama kuna kitu kama hicho kilionekana usiku huo kwanini hawakujipa muda wa kutafakari? kwa nini ilikuwa rahisi sana kwa baba kuwapata uganga usiku huo huo? Kwa nini baada ya hilo tukio Saidi ajisikie kuumwa na kumpigia mamake simu lakini akimzuia asiende mwanza? mwanamke mwenye nidhamu mme kampa taarifa anarudi na njaa lakini yeye kaenda kudanga tena na gari ya mme, marafiki wanampigia simu gari yako iko hotel fulani mme anapiga simu 42 mke hapokei, Kwanini siku hiyo mdogo mtu agome kwenda kulala kwa Saidi mahali ambapo alikuwa akiishi siku zote? Tafakari chukuwa hatua

Aisee..! Sawa Mkuu yote kwa yote inabidi tusahau kisa hiki.

Maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom