Teknolojia ipi ambayo Marekani anayo peke yake kiasi kwamba kunaweza kuifanya Huawei ipotee kutokana na vikwazo?!Mkuu tatizo sio kutengeneza. Hapa kiini cha tatizo sio kutengeneza. Kiini ni teknolojia ya kutengeneza hicho kitu.
Kama ni kutengeneza mbona karibu vitu vingi vinatengenezwa China.
Teknolojia ya kutengeneza simu kwa mfano Marekani imewachukua miaka zaidi ya 50 kufikia hapo walipo. Je China itabidi aingie kwenye utafiti aje na teknolojia yake mpya ya simu kwa miaka mingi?
Marekani anachombinya China ni kutumia teknolojia yake tu. Yeye atafte ya kwake. Hiyo ya kwake China ataipata lini?
Isitoshe Huawei anacho-rely sana kutoka US ni component parts.
Na wala sio kwamba kila component anayoagiza US haipatikani sehemu nyingine yoyote duniani... hello no! Na wala sio kwamba kampuni za China hazina uwezo KABISA wa kutengeneza hizo components; hell no!!
Ni kutokana na ukweli huo ndio maana nikasema, in the long run, China ndie atafaidika! Ndie atafaidika kwa sababu zile kampuni za Kichina ambazo zilikuwa haziwezi kushindana na kampuni za US, hatimae zitapata platform!
Ukanda ule ule wa China, kuna SMIC na Unison ambazo zipo mainland China, na kuna MediaTek iliyopo Taiwani. Huawei wenyewe wanayo HiSilicon.
Na Huawei ni kama flagship ya China, nchi ambayo ipo very supportive kwa tech companies za Kichina. Kwa maana nyingine, serikali ya China inaweza kufanya lolote wawezalo kuhakikisha Chinese Tech Firms zinakuwa fully independent in the long run!
Halafu unahoji China hiyo technology yao wenyewe wataipata lini?! Hivi watu China mnaichukuliaje?! Hivi unadhani ile technlogy espionage aliyokuwa anafanya walikuwa wanatangaza dini?
Hivi una habari China wame-invest sana kwenye R&D?! Four years ago, The New York Time waliandika:-
Na hiyo 4 years ago ilikuwa bado kabisa kukubwa na sakata lililopo hivi sasa! Umeshawahi kujiuliza ni nguvu kiasi gani inatumika hivi sasa kuhakikisha wanakuwa independent kupitia kile ambacho Xi Ping amekuwa akikiita "Self-Innovation Independence"!But China’s tech industry — particularly its mobile businesses — has in some ways pulled ahead of the United States. Some Western tech companies, even the behemoths, are turning to Chinese firms for ideas.
China na wenyewe wana ile the so called Silicon Valley of China! Miaka ya nyuma hapo Silicon Valley, ilikuwa full copy and paste! Hivi sasa unaambiwa ukionekana ume-copy technology mahali, unapigwa chini!
Na amini usiamini, ikitokea Trump akarudi madarakani kisha akaendelea kukaza tena kwenye miaka yake 4 ijayo, rais ajae hata akiamua kuondoa vikwazo ili hatimae US Firms waanze kufanya biashara na Huawei, itakuwa almost TOO LATE kwa sababu ama watakuwa wameshapata supplier mwingine, au wameshajitoleza from home-produced component parts.
Ni kutokana na ukweli huo ndio maana, Bloomberg, kutoka huko huko USA waliandika:-
Na anachofanya Trump ni kutengeneza lenye makali huku na huku... upande mmoja anadhani anaikomoa China lakini upande wa pili linaiumiza Marekani yenyewe!The Trump sanctions in some ways validated Huawei’s ability to develop cutting-edge technology, from fifth-generation networking gear to AI chips.
Kwa mfano, kampuni zilizokuwa zina-supply semiconductors chipsets zitakuwa zimepoteza kiasi gani kukosa soko kubwa kama Huawei?
Na ujinga zaidi, anaipiga ban Huawei, kwa upande mwingine Xiaomi ambao nao ni Wachina wanakuja kushika nafasi ya Huawei kwenye global smartphone market!!