Baada ya walimu walio kuwa wamejificha kwenye Ofisi za Elimu Msingi, Sekondari na TSD ndani ya Halmashauri kutimuliwa sasa Idadi ya walimu Waongezeka

Ni ujinga wao wangefanyiwa recategorization wala haya yasingekuwepo maana wangelipwa mshahara binafsi, tamaa ya fisi imewaponza.
Wangefanyiwa recategorization ipi wakati wamesomea ualimu na wamekimbia darasani kufundisha wakaenda kujichimbia Ofisi Za Elimu msingi au sekondari?
 
Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya na miji zipo187+ unapata wapi PhD holders wa kiasi hicho na wawe wa elimu. Mambo mengine watu hawawazi kabisa
Kuongoza walimu kama afisaelimu Sio lazima uwe na PhD ya ualimu.
Wenye phd UDOM na UDSM wako kibali ni suala la kuwapangia vituo vya kazi , kuwapa magari ya kufanya kazi, Ofisi na hiyo mishahara minono wanalipwa was io na PhD
 
Wangefanyiwa recategorization ipi wakati wamesomea ualimu na wamekimbia darasani kufundisha wakaenda kujichimbia Ofisi Za Elimu msingi au sekondari?
Kuna wengine unakuta ana diploma ya education lakini ana degeree ya accountancy hivyo anakuwepo uhasibu huku cheo chake ni mwalimu, kwenye ualimu alishafika mbali mshahara hivyo lazima aanze kama Accountant II ambayo ni 710,000 lakini kumbe mshahara wake kwenye ualimu ni 1M+
 
Kuongoza walimu kama afisaelimu Sio lazima uwe na PhD ya ualimu.
Wenye phd UDOM na UDSM wako kibali ni suala la kuwapangia vituo vya kazi , kuwapa magari ya kufanya kazi, Ofisi na hiyo mishahara minono wanalipwa was io na PhD
Kumbe rahisi hivyo eeeh [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] basi sawa
 
La kwanza na la muhimu ni kufikiria na kushughulikia swali hili "kwanini wanahama huko vijijini?"
 
Mwandishi ni mwalimu wa kawaida
Na hapo ameonesha wivu na chuki na huenda amekosa nafasi ambayo aliitarajia kwa muda mrefu

Na kwa kuwa anaajira tayar hayuko tayar kuona wanaajiliwa wengine wengi na ndio maana anaona waajiliwe wachache

Huu ni upuuzi tu
 
Duu, nimeamini adui wa walimu ni mwalimu mwenyewe.
Ndio hivyo moja ya kada ambayo wafanyakazi wengi hawapendani ni walimu ,chuki ,ubinafsi, kutopenda wengine wafanikiwe ,muda wote wnapenda waone wote WAKO duni

sent from HUAWEI
 
PhD hapo umekosea kabisa! Mbona kuliko na hizo PhD kumefeli pia?
 
Asante mkuuu
 
La kwanza na la muhimu ni kufikiria na kushughulikia swali hili "kwanini wanahama huko vijijini?"
Km nilivyoeleza, mazingira ya kufundisha na kujifunzia kuboreshwa. Serikali inafikiria tu madarasa lkn wamemsahau mwalimu na maslahi yake.
 
shule iko kijijini ina wanafunzi 600 au 700 ina walimu 12, ya mjini yenye idadi hiyo hiyo ya wanafunzi Ina walimu 25 hadi 30 na zaidi. Kuna shule mjini mwalimu anaingia drasani Mara mbili kwa wiki tu.

Uwiano haupo. Na hili serikali haizungumzii kabisa km vile hawaoni.

Kama serikali haiko tayari kuwahamishia vijijini inapaswa kuajiri.
 
PhD za akina Mwigulu, Jafo, Doto, Lipumba n.k zimejaa lakini hakuna cha maana wamefanya hapa nchini
Kimsingi hizi PhD za hawa viongozi ni za magumashi. Jaribu kutafuta machapisho yao km utayaona.

Ni magumashi kwasababu hivi mwalimu was udsm au udom anawezaje kumsupervise waziri ipasavyo na ahakikishe anapata PhD ya haki. Anawezaje kumsimamia kwa haki na kwa misingi imara ya kitaaluma km siyo kipeana hizi PhD.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…