Baada ya watoto wa shule kufariki wakivuka ndio Serikali ya CCM inafikiria kujenga daraja

Baada ya watoto wa shule kufariki wakivuka ndio Serikali ya CCM inafikiria kujenga daraja

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mabilioni ya pesa za umma mnatafuna.

Mnajenga madarasa hewa kwa tril 1.3

Watoto wanafariki wakivuka mto kwa mtumbwi kwenda shule. Mnakula pesa.

Hamjali maisha ya wananchi mpaka wafe.

========

Serikali kujenga daraja mto uliouwa wanafunzi Kigoma​

Kigoma. Wakati miili ya wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama ndani ya maji ya mto Luiche juzi imepatikana, Serikali imetangaza uamuzi wa kujenga daraja eneo hilo kuwaondolea wananchi adha ya kutegemea mitumbwi isiyo salama.

Uamuzi huo umetangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Tobias Andengenye leo Jumamosi Februari 25, 2023 wakati wa hafla fupi ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya wanafunzi hao iliyofanyika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma, Maweni.

“Pamoja na kujenga daraja eneo la mto Luiche, Serikali pia itatekeleza miradi ya ujenzi wa meli na vivuko kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika,” amesema Andengenye

Hii siyo mara ya kwanza Serikali kuahidi kuenga daraja eneo la mto Luiche kwani ahadi kama hiyo imewahi kyutolewa Februari, 2021 na aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Mkoa wa Kigoma wakati huo, Issa Liyanga.

Kwa sasa, wakazi wa Kata ya Kagera iliyoko takriban umbali ya Kilometa 12 kutoka katikati ya mji wa Kigoma wanaokadiriwwa kuwa zaidi ya 9, 000 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 wanavuka mto Luiche kwa kutumia mitumbwi isiyo salama kwa gharam kati ya Sh400 hadi Sh1, 000 kwa ajili ya nauli ya mitumbwi.

Mto Luiche inayomwaga maji yake ndani ya Ziwa Tanganyika hujaa na maji yake kwenda kwa kasi nyakati za masika unapojaa huku pia ndani yake kukidaiwa kuishi wanyama wakali wakiwemo mamba na viboko

Miili kupatikana
Miili ya wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama majini baada ya mtumbwi waliopanda kupinduka imepatikana ndani ya maji ya mto Luiche, hatua chache kabla ya kuingia Ziwa Tanganyika ambako mto huo humwaga maji yake.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Jacob Chacha ametaja wanafunzi ambao miili yao imepatikana kuwa ni Zabibu Jumanne (8) aliyekuwa anasoma darasa la pili na Ramadhani Matatizo (12) aliyekuwa darasa la tano.

“Jitihada zinaendelea kuwatafuta Tatu Omari na Ashura Ramadhani ambao hawajaonekana tangu mtumbwi ulipopinduka,” amesema Kamanda Chacha.

Wanafunzi waliofikwa mauti, wenzao wawili ambao hawajapatikana pamoja wengine wawili waliookolewa walizama majini Saa 1:30 asubuhi jana Ijumaa Februari 24, 2023 baada ya mtumbwi wao kupinduka wakati wakivuka mto Luiche wakitokea mtaa wa Mgumile kwenda Shule ya Msingi Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji kupinduka.
Wanafunzi wawili, Issa Omari na Michael Gogolo pamoja na nahodha wa mtumbwi, Demee Ntuguye waliokolewa katika ajali hiyo.

Gharama ya msiba
Katika hatua nyingine, Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Tobia Andengenye imetangaza kugharamia shughuli zote za mazishi ya wanafunzi hao waliofikwa na mauti wakiwa njiani kwenda shuleni.

“Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za ajali hii iliyopoteza maisha ya watoto wetu; Serikali inaungana na wafiwa katika msiba huu mzito na itabeba gharama zote za msiba huu kuhakikisha watoto wetu wanapumzishwa kwa heshima zote,” alisema Andengenye

Chanzo: Mwananchi
 
Mabilioni ya pesa za umma mnatafuna.

Mnajenga madarasa hewa kwa tril 1.3

Watoto wanafariki wakivuka mto kwa mtumbwi kwenda shule

Mnakula pesa .

Hamjali maisha ya wananchi mpaka wafe.

Bangi iruhusiwe kuvutwa hadharani!
 
Bangi na red light shop(maduka ya Malay…a)wananchi tupate kutoa stress za kifisadi.
RLD.jpg
 
Hua najiuliza Kama Kigoma Ni Tanzania.
Jana nimeona clip ya watoto wanaandikia ardhini, ardhi imepakwa rangi nyeupe, watoto Ni wengi hawaenei kwenye madarasa.
Jana hii mbichi maskini watoto wamepotea mtoni kwa kukosa daraja. Huku Dar kijiferi kinakarabatiwa kwa bilioni Saba na ushee.
Kigoma ndio walikotokea wale wabunge firebrand kina tumbili lkn kumbe Ni wachumia tumbo tu. Dada Joy nae Ni wa kulekule alikaa elimu miaka 5 lkn hata kiingereza hakujifunza achilia mbali kutatua matatizo ya watu wa Kigoma.
Au labda watu wa Kigoma mchango wao wa Kodi Ni mdogo mno.
Najiuliza Yale ma trilioni ya madarasa yalijenga madarasa mikoa gani? Hapa Mbezi sijaona darasa katika shule yoyote, Kibaha sijaona, Kigoma hakuna madarasa achilia mbali madawati.
Waziri wa fedha yupo
Waziri wa elimu yupo Tena huyu alisindikizwa bungeni na mabusu kemkem ili alete bajeti nzuri lkn wapi.
Waziri wa Tamisemi yupo
Na nanihii yupo na Mimi nipo....
 
Kigoma ni wabinafsi sana tofauti na Kilimanjaro
 
Halafu Zz anongelea waliokufa na siasa za kijinga
Nilisema badala waongelee maisha yanayoendelea kwa sasa

Hebu angalia Watoto wanaenda shule na majivu badala ya Tablets

Watoto wamejazana darasani kama zizi la mbuzi

Halafu Bungeni wanawaza waganga wa kienyeji tu
Naona wana chale mpaka kwenye kucha
 
Tulia ww, Tupo busy kuwapa Simba na Yanga M5 za magoli

Halafu Zz anongelea waliokufa na siasa za kijinga
Nilisema badala waongelee maisha yanayoendelea kwa sasa

Hebu angalia Watoto wanaenda shule na majivu badala ya Tablets

Watoto wamejazana darasani kama zizi la mbuzi

Halafu Bungeni wanawaza waganga wa kienyeji tu
Naona wana chale mpaka kwenye kucha
Mkuu umeongea maneno mazito
 
Hua najiuliza Kama Kigoma Ni Tanzania.
Jana nimeona clip ya watoto wanaandikia ardhini, ardhi imepakwa rangi nyeupe, watoto Ni wengi hawaenei kwenye madarasa.
Jana hii mbichi maskini watoto wamepotea mtoni kwa kukosa daraja. Huku Dar kijiferi kinakarabatiwa kwa bilioni Saba na ushee.
Kigoma ndio walikotokea wale wabunge firebrand kina tumbili lkn kumbe Ni wachumia tumbo tu. Dada Joy nae Ni wa kulekule alikaa elimu miaka 5 lkn hata kiingereza hakujifunza achilia mbali kutatua matatizo ya watu wa Kigoma.
Au labda watu wa Kigoma mchango wao wa Kodi Ni mdogo mno.
Najiuliza Yale ma trilioni ya madarasa yalijenga madarasa mikoa gani? Hapa Mbezi sijaona darasa katika shule yoyote, Kibaha sijaona, Kigoma hakuna madarasa achilia mbali madawati.
Waziri wa fedha yupo
Waziri wa elimu yupo Tena huyu alisindikizwa bungeni na mabusu kemkem ili alete bajeti nzuri lkn wapi.
Waziri wa Tamisemi yupo
Na nanihii yupo na Mimi nipo....
Umemsahau na mwami
 
Mabilioni ya pesa za umma mnatafuna.

Mnajenga madarasa hewa kwa tril 1.3

Watoto wanafariki wakivuka mto kwa mtumbwi kwenda shule

Mnakula pesa .

Hamjali maisha ya wananchi mpaka wafe.

Hivi, wewe muuza kangala, na muuza mbege nani zaidi? Harafu nimekumbuka vituko vya muuza mbege jamani😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom