Killa Cam
JF-Expert Member
- Jun 12, 2022
- 2,264
- 6,679
Mkuu Amsterdam patamu sana ila kule Dominican Republic na Aruba hatari sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Amsterdam patamu sana ila kule Dominican Republic na Aruba hatari sana.
Imagine! Utadhani hiyo shida ya daraja imeanza Jana au juzi. Kumbe likuwepo hata enzi ya mwendazake Rais wa wanyonge. Au nasema uwongo ndugu yangu Muuza Kangala ?!Bangi iruhusiwe kuvutwa hadharani!
Mpaka tuje kupata viongozi waadilifu na wanaoona miaka 100 mbele basi taifa letu litakuwa na umasikini wa kujitakia tuMkuu umeongea maneno mazito
PumbavuImagine! Utadhani hiyo shida ya daraja imeanza Jana au juzi. Kumbe likuwepo hata enzi ya mwendazake Rais wa wanyonge. Au nasema uwongo ndugu yangu Muuza Kangala ?!
Hii nchi ina maigizo mengi sana.Mabilioni ya pesa za umma mnatafuna.
Mnajenga madarasa hewa kwa tril 1.3
Watoto wanafariki wakivuka mto kwa mtumbwi kwenda shule
Mnakula pesa .
Hamjali maisha ya wananchi mpaka wafe.
![]()
Serikali kujenga daraja mto uliouwa wanafunzi Kigoma
Kwa mara nyingine, Serikali imeahidi kujenga daraja eneo la mto Luiche ulioko Manispaa ya Kigoma Ujiji ili kuwaondolea wananchi adha ya kutumia mitumbwi isiyo salama kuvuka mto huo. Ahadi hiyo...www.mwananchi.co.tz
Imagine! Utadhani hiyo shida ya daraja imeanza Jana au juzi. Kumbe likuwepo hata enzi ya mwendazake Rais wa wanyonge. Au nasema uwongo ndugu yangu Muuza Kangala ?!
ujiji wamejaa waswahili ambao hawataki kufanya kazi.kuna kijiwe kiko karibu sana na soko la kagera ukipita pale saa 12 asubuhi utakutana na wazee kwa vijana wanakunywa kahawa muda wote.Kumbe Ujiji kuna umaskini sana!
Jamaa pesa ni kulipana posho na kununua mashangingiMabilioni ya pesa za umma mnatafuna.
Mnajenga madarasa hewa kwa tril 1.3
Watoto wanafariki wakivuka mto kwa mtumbwi kwenda shule. Mnakula pesa.
Hamjali maisha ya wananchi mpaka wafe.
========
Serikali kujenga daraja mto uliouwa wanafunzi Kigoma
Kigoma. Wakati miili ya wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama ndani ya maji ya mto Luiche juzi imepatikana, Serikali imetangaza uamuzi wa kujenga daraja eneo hilo kuwaondolea wananchi adha ya kutegemea mitumbwi isiyo salama.
Uamuzi huo umetangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Tobias Andengenye leo Jumamosi Februari 25, 2023 wakati wa hafla fupi ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya wanafunzi hao iliyofanyika viwanja vya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma, Maweni.
“Pamoja na kujenga daraja eneo la mto Luiche, Serikali pia itatekeleza miradi ya ujenzi wa meli na vivuko kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika,” amesema Andengenye
Hii siyo mara ya kwanza Serikali kuahidi kuenga daraja eneo la mto Luiche kwani ahadi kama hiyo imewahi kyutolewa Februari, 2021 na aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Mkoa wa Kigoma wakati huo, Issa Liyanga.
Kwa sasa, wakazi wa Kata ya Kagera iliyoko takriban umbali ya Kilometa 12 kutoka katikati ya mji wa Kigoma wanaokadiriwwa kuwa zaidi ya 9, 000 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 wanavuka mto Luiche kwa kutumia mitumbwi isiyo salama kwa gharam kati ya Sh400 hadi Sh1, 000 kwa ajili ya nauli ya mitumbwi.
Mto Luiche inayomwaga maji yake ndani ya Ziwa Tanganyika hujaa na maji yake kwenda kwa kasi nyakati za masika unapojaa huku pia ndani yake kukidaiwa kuishi wanyama wakali wakiwemo mamba na viboko
Miili kupatikana
Miili ya wanafunzi wawili kati ya wanne waliozama majini baada ya mtumbwi waliopanda kupinduka imepatikana ndani ya maji ya mto Luiche, hatua chache kabla ya kuingia Ziwa Tanganyika ambako mto huo humwaga maji yake.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, Jacob Chacha ametaja wanafunzi ambao miili yao imepatikana kuwa ni Zabibu Jumanne (8) aliyekuwa anasoma darasa la pili na Ramadhani Matatizo (12) aliyekuwa darasa la tano.
“Jitihada zinaendelea kuwatafuta Tatu Omari na Ashura Ramadhani ambao hawajaonekana tangu mtumbwi ulipopinduka,” amesema Kamanda Chacha.
Wanafunzi waliofikwa mauti, wenzao wawili ambao hawajapatikana pamoja wengine wawili waliookolewa walizama majini Saa 1:30 asubuhi jana Ijumaa Februari 24, 2023 baada ya mtumbwi wao kupinduka wakati wakivuka mto Luiche wakitokea mtaa wa Mgumile kwenda Shule ya Msingi Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji kupinduka.
Wanafunzi wawili, Issa Omari na Michael Gogolo pamoja na nahodha wa mtumbwi, Demee Ntuguye waliokolewa katika ajali hiyo.
Gharama ya msiba
Katika hatua nyingine, Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Tobia Andengenye imetangaza kugharamia shughuli zote za mazishi ya wanafunzi hao waliofikwa na mauti wakiwa njiani kwenda shuleni.
“Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za ajali hii iliyopoteza maisha ya watoto wetu; Serikali inaungana na wafiwa katika msiba huu mzito na itabeba gharama zote za msiba huu kuhakikisha watoto wetu wanapumzishwa kwa heshima zote,” alisema Andengenye
Chanzo: Mwananchi