Baada ya watoto wa shule kufariki wakivuka ndio Serikali ya CCM inafikiria kujenga daraja

Enzi za Nyerere au Mwinyi ilikua rahisi mtoto wa mkulima maskini kutoboa Kama atazingatia elimu na kupasi vizuri.
Enzi zile hata interview zilikua fair kabisa, ukijibu vizuri unapewa kazi.
Huwezi kuniambia kwamba mtoto anayeandikia kwenye majivu uwanjani huko Kigoma, mtoto anayekwenda shule na mtumbwi unaoendeshwa na mtoto mwenzie atapambana kielimu Hadi awe sawa na mtoto anayesoma Feza schools aliyeanza kutumia laptop akiwa darasa la kwanza.
Hata Kama wa Kigoma atafika chuo, ngima itakua kupata kazi, wa Feza simu moja tu, anaajiriwa benki kuu au TANAPA, au Uhamiaji au TRA(Watoto waliosoma Feza huwezi kuwakuta Ni walimu au mabwana shamba )
Hata huyu wa Kigoma akianzisha biashara TRA watahakikisha analipa Kodi zote, Ila wa Feza, simu moja tu anatoa kontena au mzigo wa iPhone eapot bila kulipa ushuru.
Tukija kwenye kugombea ubunge, wajumbe wanahitaji kula na hawali mihogo.
Tukija kwenye teuzi......
Itaendelea........
 
Hii nchi ina maigizo mengi sana.
Tuliaminishwa tozo na pesa za uviko ni kwa ajili ya madarasa na zahanati.
Juzi tuna shuhudia watoto wakiandikia majivu nje. Bado huduma za afya ni tatizo. Wana kula kwa kwenda mbele.
 
Jamaa pesa ni kulipana posho na kununua mashangingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…