Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Walokuwa wanawatafutia sababu.
Mmnapokea misaada mingi sana bila sababu ya msingi.
Merely kwa sababu ya amani na kuheshimu haki za binadamu.
Ila mnavyojifanya much knows ndio hapo kalieni sasa mti
 
Kwahiyo zitto ndyo ambaye hafuati utawala wa sheria na haki za binaadamu? kama ndivyo basi sawa.
 
Ushauri wako ni nini kwa Serikali?
 
Kama haki za binadamu zenyewe ni za kuruhusu ushoga Bora wasepe tu na pesa zao.
 
Nani kamwambia hii serikali inashauriwa,

kazi yetu ni kuwakumbusha yakitokea tunawakumbusha tena kuwa tuliwakumbusha mkatudharau.
Unaishi nchi gani, au utaishi nchi gani hali ya uchumi wa Tz ukiporomoka, kama mnavyoamini.

Hata vile 2020 haiko mbali, msawaidie viongozi wa vyama vya upinzani kujipanga kuiondoa Serikali ya CCM na mbaya wao Rais Magufuli.

Lakini kwa jinsi viongozi wa upinzani wanavyoendesha siasa, ni ndoto kupata ridhaa ya WaTz, hata wakiruhusiwa mikutano ya hadhara, maana agenda zao kuu zitakuwa kuishambulia Serikali na kulilia Demokrasia na Katiba Mpya. Kero za wananchi je!

Isitoshe viongozi wa upinzani wameshindwa kuonesha tofauti ya uongozi kwenye majimbo na halmashauri wanaziongoza. Matokeo yake viongozi wa kuchaguliwa wanahama ati wananunuliwa.

Naamini muda uliobakia kufikia Uchaguzi Mkuu bado unatosha kwa vyama vya upinzani kujipanga. Hasa kwa CHADEMA kuzinadi Sera zake, kwa nguvu zote, zieleweke na kukubalika kwa wapiga kura.

Upande mwingine wafuasi wa vyama vya upinzani humu waachane na mada za kuizodoa Serikali tu, ila watumie muda wao mwingi kuzieneza Sera mbadala za maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi na Taifa.
 
Ila wasituingilie mambo yetu bhn.wawe honest.
 



"".................wanaofuata ni nchi za Scandinavia ambazo ni Sweden, Finland, Norway, Iceland. Canada, Marekani na Uingereza watamalizia. Tutabaki na mchina.""

hivi nchi za scandinavia zimeongezeka eeeh😎
 
Am just thinking of my mother, she's about to retire Na haya majibwa yamepitisha 25 Kwa 75% Na alivyo spender mamangu Na ccm die hard fan, lord have mercy! No wonder Joyce mapunjo alipotumbuliwa Tu ukatibu mkuu akajifia, dahh!
Mkuu kama mama ako ni spender, shukuru hii formula mpya ya kukokotoa mafao, itamsaidia sana

Maana itampa lamp sum ndogo ambayo ataitumbua kutokana na tabia yake ya ku-spend, lakini kila mwisho wa mwezi atakuwa anapata mshahara kama alivyokuwa anaupata akiwa kazini

Hii formula mpya itaumiza wale wenye mikakati ya kuwekeza
 
Sasa wewe unatakaje? Tukubali ushoga? Hakuna inchi iliyoendelea kwa kutegemea misaada tu.. Fanyeni kazi tuache kuombaomba
Tufanye kazi ipi? Je tufanye nini ili ushoga uishe nchini? Kuwafunga sio solution wakuu.
 
Acha kuponda watu,usiowajua.
 
Uko nje ya mada, mada ni nchi za magharibi kusitisha misaada sio uchaguzi.
 
"".................wanaofuata ni nchi za Scandinavia ambazo ni Sweden, Finland, Norway, Iceland. Canada, Marekani na Uingereza watamalizia. Tutabaki na mchina.""

hivi nchi za scandinavia zimeongezeka eeeh😎
Soma vizuri uwe unaangalia matumizi ya 'koma' na 'full stop'.
 
wewe unafikiri watu atujionei kinachondelea Zitto anaongea tu wengine tunaona tunakaa kimya tukiongea wote itakua balaa
 
Mkuu, Hivi EU na kina Scandinavia kuchangia 40% ya bajeti ya serikali yetu ni jambo linalokufanya upate hamasa ya kuandika hapa kama kwamba ndio mwisho wa taifa Tanzania?. Mimi nadhani ungekemea viongozi wetu walioukubali huo mpango wao wa DPC na zaidi sana ni kwa nini wanataka kusaidia nchi hizo 17 wakati kwao wana masikini wanaoshindwa kupata hata mlo wa mchana?.

Nchi hii haihitaji misaada ya namna hiyo na ni aibu kuendelea kupokea misaada kama hiyo maana masharti yake yanakufanya kuwa mtumwa kwao, Nafahamu jinsi hao hao unaowasifia wanavyowasimanga viongozi wetu wanapokwenda kutembea mabakuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…