Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Yaani unalilia msaada kama mtoto mdogo. Kwa hiyo uko tayari kutatuliwa marinda alimradi tu upewe msaada? Aisee.
Sijui unajaribu kuzuis ukweli usiongelewe? Pole sana. Budget ya Tz, yategemea zaidi ya 50% misaada/mikopo toka kwa wadau wa maendeleo toka nje.
Kujifanya eti hujali sio ajabu, LAKINI hiyo, haitofuta adha tutakayokuja pata watz, kutokana na kiburi cha makusudi kilichokithiri cha watawala wetu hata baada ya kushauriwa kiungwana kuhusu kuheshimu haki za binadamu na kuachana kuwakandamiza watz wenzao na kuheshimu katiba nasheria za nchi. Zimbabwe ya Mugabe ni mfano hai. Amen.
 
Mkuu, Hivi EU na kina Scandinavia kuchangia 40% ya bajeti ya serikali yetu ni jambo linalokufanya upate hamasa ya kuandika hapa kama kwamba ndio mwisho wa taifa Tanzania?. Mimi nadhani ungekemea viongozi wetu walioukubali huo mpango wao wa DPC na zaidi sana ni kwa nini wanataka kusaidia nchi hizo 17 wakati kwao wana masikini wanaoshindwa kupata hata mlo wa mchana?.

Nchi hii haihitaji misaada ya namna hiyo na ni aibu kuendelea kupokea misaada kama hiyo maana masharti yake yanakufanya kuwa mtumwa kwao, Nafahamu jinsi hao hao unaowasifia wanavyowasimanga viongozi wetu wanapokwenda kutembea mabakuli.
Hatuna namna aliyetangulia katangulia, 40% wanayotoa wazungu ndiyo pesa yenye uhakika, 60% ya pesa za ndani hata 30% yake tunashindwa kutimiza.
 
Kipindi cha Kikwete mlikua hamtaki tuwe ombaomba au mmesahau na je upo tayari mkuu kupewa msaada kwa masharti ya kuwa shoga tuje tukutolee barua?
Muulize Dr. Mpango kama serikali iko tayari kupewa msaada wa masharti, kama haiko tayari tusisikie kwenye bajeti anasema nusu yake tunategemea wahisani vinginevyo muache usanii.
 
Muulize Dr. Mpango kama serikali iko tayari kupewa msaada wa masharti, kama hayuko tayari tusisikie kwenye bajeti anasema nusu yake tunategemea wahisani.
Mpango akikubali vipi naruhusiwa kuja kutoa posa kwa mzee wako?
 
Hiyo haijalishi sisi hatuogopi chochote maana sisi ni matajiri sana ndiyo maana tunanunua ndege kwa keeshii na tunanunua korosho kwa keshiii
Hawa watu wana ushirikiano wa hali ya juu, hawana msaliamtume hasa linapokuja suala la haki za binadamu na utawala bora, ndio maana utakuta nchi nyingi zinazoongoza kwa utawala bora huwa ni kutoka nchi za EU na Scandinavia.

Kwa wasiojua nchi hizo huchangia 40% ya bajeti yetu, pia wana mpango wa pamoja wa kuisaidia Tanzania kimaendeleo unaojulikana kama Development Partners Group (DPG) unaohusisha nchi zaidi ya 17 nyingi zikiwa za EU na Scandinavia, UK na US, pamoja na mashirika makubwa matano ya kimataifa, WB, UN, European Commission, ADB na IMF.

Kutokana na mpango huo Tanzania hupokea wastani wa $2.5 billion zaidi ya trillion 6 kila mwaka.

Kutokana na ubabe na kiburi chetu WB wamezuia msaada wao leo Denmark wametunyima msaada na kumzuia balozi wao kututembelea kitendo kinachotafsiriwa kama mwanzo wa kuvunja uhusiano, wanaofuata ni nchi za Scandinavia ambazo ni Sweden, Finland, Norway, Iceland. Canada, Marekani na Uingereza watamalizia. Tutabaki na mchina.

Nchi hizi ni wadau wakubwa wa maendeleo yetu, ni wadau wakubwa kwenye sekta ya madini, utalii, gas nk. Tunapobeza umuhimu wao tutegemee kuzorota kwa uchumi pengine hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya Zimbabwe.
 
Hatuna namna aliyetangulia katangulia, 40% wanayotoa wazungu ndiyo pesa yenye uhakika, 60% ya pesa za ndani hata 30% yake tunashindwa kutimiza.
Tunashindwa kutimiza kwa sababu hatujajipanga kujiletea maendeleo wenyewe bila kuwategemea wahisani. Hata wao wanalijua hilo, tatizo letu kubwa ni ile kasumba waliyoturithisha wenyewe kwamba wao ni watu bora wenye akili baada ya mungu. Jiamini mtu wangu... kwa kasi hii ya JPM utasikia mengi, Kelele kama hizi zilikuwepo sana tu hata enzi za Nyerere.
 
God is our refuge and strengh , a very present help in trouble.
Therefore we will not fear,though the earth be removed,and though the mountains be carried into the midst of the see.........

God is in the midst of her,she shall not be moved:God shall help her,and that right early.

The Lord of hosts is with us,the God of Jacob is our refuge.
Dr mihogo hajambo?
 
Back
Top Bottom